Mliopata kazi maofisini mlipataje?

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
4,824
5,561
Nimezunguka sana natafuta kazi nimekosa,nilianza na vogezo stahili kulingana na elimu yangu sijaweza fanikiwa mpaka kazi zs kibarua nazo nakosa.

Nikiangalia maofisini nawakuta vijana wakike na wakiume wa umri wangu wapo mofisini.

Ndugu zangu nyinyi uwa mnapataje kazi?
 
Sometimes graduates wengi wanatafuta kazi ktk taasisi kubwa mfano TRA, TPA, TANESCO, VODACOM, TCRA, TIGO, HESLB, NSSF, NHIF n.k


Huko unakuta ndo kila siku wapo, mtu amesoma accounting au IT unapomueleza aanze kazi SACCOS au secondary kama it officer au accountant anakuwa hataki au anataka kama ni shule basi Feza boys. That is a big challenge.

Pia ujuzi wa mambo ni mdogo kwa wengi pamoja na vyeti walivyonavyo

MUHIMU : Pia kazi sio nyingi sana so usijilaumu kama tayari umefanya part yako vizuri. Keep pushing kuna muda vitu vitajibu tu don't give up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimezunguka sana natafuta kazi nimekosa,nilianza na vogezo stahili kulingana na elimu yangu sijaweza fanikiwa mpaka kazi zs kibarua nazo nakosa.

Nikiangalia maofisini nawakuta vijana wakike na wakiume wa umri wangu wapo mofisini.

Ndugu zangu nyinyi uwa mnapataje kazi?
Pole sana. Kila mtu hupitia hiyo hali anapotafuta kazi kwa muda mrefu bila mafanikio. Hata hao unaowaona wapo maofisini wengi wao pia wamesota kama wewe. Siku yako itafika tu na wewe utakuwa miongoni mwa hao unaowatamani.
 
Nina mpenzi kaenda kwenye interview juzi kaulizwa maswali mawili tu baada ya jina lake kuonekana linaendana na moja ya mtumishi wa pale

'Una ndugu yako anafanyakazi hapa
Kajibu ndio
Ni ndugu yako kivipi
Kamuelezea pale
Kaandika andika alivyojua kamruhusu aondoke
Juzi kapigiwa simu kaelekweza baadhi ya mambo yakufanya na kaambiwa tarehe 1 mwezi wa pili inabidi akaanze kazi
Kwa hiyo wenzangu na Mimi tusio na wajomba kwenye vitengo tutasugua sana tujipange
Ananiambia walikuwa nyomi kwenye interview




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta bila kuchoka. Kuna mdau hapo juu pia kaeleza anzia taasisi ndogo hata kwa ku-volunteer jijenge pata experience juhudi na nidhamu yako itakufikisha! pale unapotaka.
Lakini kukumbuka pia siku hizi watu wengi wanasoma na kufikia level za degree na masters tofauti na miaka ya nyuma hivyo ushindani unakua mkubwa kwenye soko la ajira.
Kwa hiyo mbali na degree yako una kitu gani cha ziada??? Ukiweza jiongezee short courses zinazohusu profession yako, ongeza knowledge ya IT ambayo itakua useful kwenye field yako, fanya management/leadership course....nawekea mkazo kwenye kufanya kazi za kujitolea (volunteer) na ukijitolea omba recommendation letter, zitakusaidia sana!!
Kwa kufanya hivyo hapo juu CV yako itakua tofauti na itakuongezea nafasi zaidi ya kupata ajira haraka.
Lakini katika yote hayo muweke Mungu kwanza. Kila application unayotuma iombee na ombea wale watakaopitia application Mungu ni mwaminifu Sana atasikia na atakupa kazi nzuri aliokuandalia.
All the best!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taaisis binafsi kazi nyingi kama sio zote ni za kujuana. Taasisi binafsi nyingi kazi zake hua hazitangazwi kwa umma. Mfano, angalia CRDB, hakuna siku nimeona wametangaza kazi kwa miaka 4 au 5 iliyopita ila kila siku wanaajiri watu wapya, hujiulizi wao hao watu wanawapataje? Taaisis nyingi binafsi ziko hivyo.

Taaisi za umma, hapa kuna mambo mawili, la kwanza, kazi nyingi kwa sasa kwa taasisi za umma nyingi zinatangazwa utumishi, ili upate kazi pale unatakiwa kua na uwezo binafsi na sio vyeti, maana kazi inatangazwa moja waombaji 2000, wote mna vyeti sawa.

Taasisi chache za umma ambazo bado zinaajiri zenyewe kazi zake hua zinatangazwa kwa watu wote wa nje na ndani au wakatangaza wa ndani tu(hapa wana nia ya kuajiri watu wao tu), hivyo kama uko ndani unapata kazi kiurahisi, kama uko nje pia unaweza kupata kama hizo kazi zimetangazwa hivyo.

Changamoto.
1. Vijana wengi mna vyeti vizuri ila hamna vitu vya ziada kichwani, mnajua tu mambo ya shule tu, nje ya shule hamjui kitu, ikitangazaa kazi iwe ya taaisis binafsi au ya serikali na ikawa na usawa, mkafanyishwa intelligence test wengi hua mnapukutishwa hapo hata kama mna vyeti vizuri. Mjitahidi kujiongezea maarifa, maarifa sio ya shuleni tu.

Jambo la pili, ukosefu wa ajira, serikali kwa miaka 3 tu imeajiri watu si zaidi ya elfu 7 kwa takwimu za utumishi, walioomba kazi ni kama laki 6, unaweza kuona wastani au uwezekano wa mtu kupata kazi serikalini ulivyo.

Tuombe serikali iboreshe mazingira ya kujiajiri ili iwe ajira nyingi zile zinamezwa na sekta binafsi.

Kwa wewe, nikushauri komaa utumishi utapata kazi. Sekta binafsi kujuana ni kwingi sana.
 
Nina mpenzi kaenda kwenye interview juzi kaulizwa maswali mawili tu baada ya jina lake kuonekana linaendana na moja ya mtumishi wa pale

'Una ndugu yako anafanyakazi hapa
Kajibu ndio
Ni ndugu yako kivipi
Kamuelezea pale
Kaandika andika alivyojua kamruhusu aondoke
Juzi kapigiwa simu kaelekweza baadhi ya mambo yakufanya na kaambiwa tarehe 1 mwezi wa pili inabidi akaanze kazi
Kwa hiyo wenzangu na Mimi tusio na wajomba kwenye vitengo tutasugua sana tujipange
Ananiambia walikuwa nyomi kwenye interview




Sent using Jamii Forums mobile app
Looh

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom