Nina uhakika humu jf hawatakosekana waliopita skuli ya highlands hasa miaka ilee kuanzia sheikh.......choudry.......mpaka kimangale.........teh teh teh......
wewe umepita miaka ipi hapo highlands, mimi nimepita wakati wa choudry 1987 - 1990.
basi hapan shaka miaka hiyo utawakumbuka mwl.mwakangale -mtaalam wa geography,mrs sachu wa english,mwl umande physics,mwl.chalamila,mwl.musa mpambe wa choudry etc.....hebu tukumbushane mambo ya zamani hizo mfano wanafunzi waliovuma mfano bob reagan.............
umande amenifundisha physics, mdemu maths, etc. Bob reagan namkumbuka sana na nafikiri tulikua mwaka mmoja isipokua (steams) mikondo tofauti (kama unavyojua hii shule ilikua kubwa sana na nafikiri bado ni kubwa), sina uhakika kama alimaliza vizuri shule kwani alikua pasua kichwa sana. Wewe ulimaliza mwaka gani pale?
mie pale nimechomoka 1992...duh kweli mkuu umenikumbusha mbali sana mwl. Mdemu baada ya kumtaja ndo memory kibao zimerejea,huyu bob reagan mara ya mwisho nimekutana nae mitaa ya posta(dar) miaka ya 2000 katikati alirudishwa kutoka south akapokelewa segerea ,kwa sasa sijui alipo,..kwa kipindi hicho wacheza mpira kina yahaya mchata utawakumbuka,mechi kubwakubwa chuo cha kleruu.....sweet memory hebu kumbusha mambo mengine ya kipindi kile disco ruaha international etc.
Namkumbuka sana, amenifundisha Physics Form 3 na 4, alikua mzuri sana wa Physics. Nadhani alikua mtu wa mkoa wa Pwani kitu kama hicho.Mwl umande wa physics unamkumbuka?