Mlio katika Mahusiano yenu na Wazoefu ( Wabobezi ) je, hili lina ukweli wowote?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kwamba ukirejea Nyumbani Kwako au ukikutana tu na Mkeo au Mpenzi wako na ukaona amechangamka sana huku amezidisha Mahaba ( Upendo ) Kwako hapa ina maanisha ametoka Kukusaliti au anaenda Kukusaliti au kuna Bonge la Mzinga anaenda Kukupiga hivyo anakuandaa Kisaikolojia.

Majibu yenu ni muhimu sana tena mkiyawahisha Usiku ( muda ) huu itapendeza zaidi ili Karatasi na Kalamu ya Kuandika Barua ya Talaka viwe Standby au nijipe Mazoezi ya Kukomaza zaidi Viganja vyangu vya Mikono tayari kwa Kutua Mashavuni au Usoni au hata Kisogoni mwa Mtu kwa Hasira zangu Kali za Kipemba.
 
Alafu kuna mtu mmoja alisema ambao hawajaoa wasiwe wanachangia mada za ndoa maana hawajui yaliyoko kwenye ndoa. Hiv kama walio oa wenyewe ndio wana akili kama hizi unategemea nin hapo?

Nirudi kwenye mada: Usipende kuwa negativity sana kwenye ndoa yako utaivunja alafu uje ujutie
 
Bwana ndogo usifanye mambo kwa kuhisi vitakusumbua sana fanya uchunguzi pata uhakika then fanya maamuzi huo ndio uwanaume
 
Ukiwa umeamua kuoa tena kwa kufanya selection na kupata Choice uitakayo Basi jifunze kumuamini Mkeo kwa hali yoyote ile..,
Kuwa na Mashaka kwa Mkeo na akagundua kutaongeza Mashaka katika mahusiano yenu na kupelekea kupunguza Upendo!!!
 
Back
Top Bottom