Mlima Kilimanjaro ingekuwa inawezekana ungehamishiwa Chato

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Ukifuatilia mwenendo ni kwamba Mt Kilimanjaro ungeweza kuhamishwa kwenda Chato ungehamishwa muhula huu. Tumeshaona mbuga za kutengeneza, uwanja malazimisho ya mashirika ya uma kama CRDB kujenga majengo, NHC kujenga majengo na mengineyo maajabu tutaona mengi sana kipindi hiki.

Bahati mbaya kuna viongozi wa nchi jirani ambao hawajawahi kufika makao makuu Dodoma lakini wamefika Chato. Hivi Nyerere angekuwepo angesema nini na Butiama yake masikini?. Nchi ambayo Nyerere kaiacha imeanza kuwa ya kikanda na maendeleo na kibaya zaidi ni mawaziri badala ya kufuata budget wamekuwa kwenye mikakati ya kujipendekeza kufanya miradi Chato ambayo haina tija.

Uwanja wa KIA ambao ndiyo unaleta watalii ungeweza kupanuliwa kwanza na Rais akatumia helkopta kutoka airport ya Mwanza lakini amefanya nchi ni kama yake binafsi na yeye ndiye aamue pesa itumike vipi!

Tanzania tunakazi tuombee nchi yetu sana.
 
Huyu ni raisi wa wanyonge.

Wanyonge ni watu walionyimwa fursa kwa lazima na serikali za CCM, waliolazimishiwa elimu duni na ya kimagumashi na serikali za CCM, waliolazimishiwa umaskini na serikali za CCM, na wanaoendeshwa kama watumwa na kuswagwa kama makondoo na serikali ya awamu ya tano ya Magufuli.
 
Bakini na Kilimanjaro, Chato yetu Kuna ziwa Victoria!
Kama hii ni ajenda ya CHADEMA wenzangu naona mimi hapa nitatofautiana maana nasisi tuliosahauliwa siku nyingi tunataka maendeleo Kama wengine waliowahi kidogo nchini!
Mnakaa mnajiliwaza na mtu anayefikiri kuwa maendeleo ni vitu badala ya watu.

Hata mpewe milima na mito, mjengewe madaraja, na maghorofa ya kariakoo yajengwe kijijini huko, bila kujielimisha, kujitambua, kupambana kutetea haki zenu, pamoja na kuwa huru kifikra na kisiasa, bado mtakuwa chini tu.

Punda elfu moja hutawaliwa na binadamu mmoja na huyu binadamu humchinja punda yoyote saa akiamua. Hivyo hivyo, mtu mmoja aliyeelimika, anayejitambua na anayejua haki zake, aliye huru kifikra na kisiasa, atawatawala watu maelfu wanaojivika ujinga na upumbavu wa kuabudu vitu badala ya kujijenga kiuchumi, kielimu, kiafya, kifikra, na wanaojua kufungua na kutumia fursa.
 
Mnakaa mnajiliwaza na mpumbavu wenu anayefikiri kuwa maendeleo ni vitu badala ya watu. Hata mpewe milima na mito, mjengewe madaraja, na maghorofa ya kariakoo yajengwe kijijini huko, bila kujielimisha, kujitambua, kupambana kutetea haki zenu, pamoja na kuwa huru kifikra na kisiasa, bado mtakuwa chini tu.

Punda elfu moja hutawaliwa na binadamu mmoja na huyu binadamu humchinja punda yoyote saa akiamua. Hivyo hivyo, mtu mmoja aliyeelimika, anayejitambua na anayejua haki zake, aliye huru kifikra na kisiasa, atawatawala watu maelfu wanaojivika ujinga na upumbavu wa kuabudu vitu badala ya kujijenga kiuchumi, kielimu, kiafya, kifikra, na wanaojua kufungua na kutumia fursa.
Unamzidi elimu nani, lofa mkubwa, wewe unayepotosha ukombozi halisi wa nchi kwa kung'ang'ania 'nonissues' na kuharibu umoja miongoni mwa 'combatants'!?
Chato pia wanamageuzi wapo lakini huwapati unapoanza kujaribu kutaka kuwapumbaza wabakie karne ya 19 wakati wewe kwenu mnaishi kwenye 'future world'!
 
Bakini na Kilimanjaro, Chato yetu Kuna ziwa Victoria!
Kama hii ni ajenda ya CHADEMA wenzangu naona mimi hapa nitatofautiana maana nasisi tuliosahauliwa siku nyingi tunataka maendeleo Kama wengine waliowahi kidogo nchini!
AKILI ZA WASUKUMA!!
 
Mabutu aliweka kila kitu lakini imerudi pori maana maendeleo ni watu
 
Bakini na Kilimanjaro, Chato yetu Kuna ziwa Victoria!
Kama hii ni ajenda ya CHADEMA wenzangu naona mimi hapa nitatofautiana maana nasisi tuliosahauliwa siku nyingi tunataka maendeleo Kama wengine waliowahi kidogo nchini!

[/QUOT
Wenyeji wa mkoa wa Dar ni wazaramo, dar ina kila kitu lakini wazaramo bado ni maskini.

Kwanini bado ni maskini????? Jibu ukilipata basi litakusaidia kwenda chato na kumshauri mfalme jinsi ya kuwakwamua watu wake.
 
Bakini na Kilimanjaro, Chato yetu Kuna ziwa Victoria!
Kama hii ni ajenda ya CHADEMA wenzangu naona mimi hapa nitatofautiana maana nasisi tuliosahauliwa siku nyingi tunataka maendeleo Kama wengine waliowahi kidogo nchini!
Mbona kwetu Kilwa tuko nyuma zaidi na hatuletewi kitu wala kuzungumziwa popote?
 
Nimesikia kuna mpango wa kuwahamishia Sokwe kwenda kwenye mbuga, moja ipo Kagera na nyingine nimesahau! Nina kila sababu za kuamini suala la Sokwe kupelekwa kwenye hizo mbuga ni kutuandaa kisaikojia, ili hapo baadae wengine wakipelekwa Burigi Chato ionakenae ni jambo la kawaida, lakini kimsingi mpango huu unalenga kupeleka sokwe Chato!
 
Bakini na Kilimanjaro, Chato yetu Kuna ziwa Victoria!
Kama hii ni ajenda ya CHADEMA wenzangu naona mimi hapa nitatofautiana maana nasisi tuliosahauliwa siku nyingi tunataka maendeleo Kama wengine waliowahi kidogo nchini!
Bila kusoma maendeleo mtalazimisha lakini yatawakataa. Someni kwa bidii. Na kama ni huko Chato ili muendelee achaneni na imani za kishirikina.
 
Back
Top Bottom