Mlikuwa wapi kuwaunga mkono Zitto na Kafulila?

Mlikuwa wapi kuwaunga mkono Zitto na Kafulila?

Joined
Oct 30, 2014
Posts
24
Reaction score
10
Ndugu zangu kwa masikitiko makubwa tangu report ikabidhiwe kwa mwenyekiti wa (PAC) Mh.Zuberi Zitto Kabwe kumekuwa na utaratibu wa viongozi hasa wa CHADEMA kujitoa ufahamu kwa kuiunga hoja hii mkono baada ya kuona mambo yanakuwa mazuri kwa upande wa Kafulila na Zitto.

Wakati mjadala wa #Escrow unaibuliwa bungeni wabunge wengi wa upinzani na chama tawala hawakuwaunga mkono na walionekana kama watu walionunuliwa kisiasa Nakumbuka Kafulila alizungumza mara nyingi sana bungeni bila kupata sapoti ya wabunge wenzie wao walikiwa busy na Ukawa.

Wakati wabunge wa upinzani wakiwa busy na Ukawa hawakuona umuhimu wowote wa kuunganisha nguvu ya pamoja dhidi ya ufisadi hui wa wa akaunti ya #Escrow si Mkiti wa NccrMageuzi ndugu Mbatia wala Mkiti wa CHADEMA ndugu Mbowe .

Kinacho nishangaza sasa ni uthubutu wa Mbatia na media eti kuizungumzia #Escrow leo yeye na vibaraka wenzie kama #Joshua Nasary,Halima Mdee na Lissu mlikuwa wapi kupaza sauti ya pamoja tangu mwanzo wa sakata hili?

Mlitaka kuona Zitto na kafulila wameonesha failure katika harakati zao za ukombozi wa nchi dhidi ya Mafisadi?? Sasa aibu yenu Vijana wameonesha msimamo na heshima kubwa pamoja na kutukanwa,kufukuzwa,kudhalilishwa na hata kutishiwa maisha lakini bado wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya Taifa.

Taifa linawategemea pambaneni nasi tuko nyuma yenu kuwaunga mkono....No retreat No surrender Aluta continua!!A
 
bikira wa Kimasai


wewe hata bunge la BAJETI ukuangalia ungekuwa ulifatilia usingeandika haya, hata msemaji wa kambi ya upinzani aliliongelea hili suala WENJE alisema hii skendo ni kubwa kuliko EPA halima mdee wabunge wengi wa cuf MBATIA na wengne wengi tu waliliongelea kwa msisitizo mkubwa kabla ya kuandika fanya utafiti
 
Last edited by a moderator:
bikira wa Kimasai
Wewe ni mpuuzi kweli. Ulitaka wawabebe migongoni ndio ujue kuwa wameungwa mkono? Hii tabia ya kukurupuka toka usingizini na kupost vitu visivyo na msingi ikome mara moja. Unajitoa ufahamu sio?
 
Last edited by a moderator:
bikira wa Kimasai

Hauna akili kabisa, ulitaka Mbowe avue nguo na kujikata kata na viwembe ndo ujue kwamba aliunga mkono hoja ya Kafulila?
 
Last edited by a moderator:
Zitto atabaki kua Zitto tu .

Hakuna kijana/ mwanasiasa anayeibua maswala nyeti na yenye maslahi na watz kama Zitto. Anaweza kua kimya hata mwaka mmoja , ila akiibuka anaibuka na Jambo senstive.

Kwa hiyo Kaka hao wengine waache tu , wanasindikiza , sisi tunaelewa watu wenye nguvu .

Akili ndogo kushindana na Akili kubwa.
 
Walijua kuunga mkono ni kumkubali ZITTO kabwe wanayemtuhumu kutumiwa na CCM ambayo ameisimamia kidedea kuhusu ESCROW. Mimi nilishasema wapinzani hawana jipya.
 
wewe hata bunge la BAJETI ukuangalia ungekuwa ulifatilia usingeandika haya, hata msemaji wa kambi ya upinzani aliliongelea hili suala WENJE alisema hii skendo ni kubwa kuliko EPA halima mdee wabunge wengi wa cuf MBATIA na wengne wengi tu waliliongelea kwa msisitizo mkubwa kabla ya kuandikafanya utafiti
Mkuu achana na wakukurupuka huyo
 
Zitto amewafanya ,anawafanya na ataendelea kuwafanya wanachama wengi wa CDM wapumbavu.

Zitto ana uwezo yule ..tena saana .. sijawahi kumuundermine Zitto ..

Kwanza tumshkuru saana ,mpaka leo nguvu waliyonayo upinzani /hususani vijana Genesis yake ilianza kwa Zitto Kabwe.
 
Zitto atabaki kua Zitto tu .
Hakuna kijana/ mwanasiasa anayeibua maswala nyeti na yenye maslahi na watz kama Zitto..
Anaweza kua kimya hata mwaka mmoja , ila akiibuka anaibuka na Jambo senstive.

Kwa hiyo Kaka hao wengine waache tu , wanasindikiza , sisi tunaelewa watu wenye nguvu .

Akili ndogo kushindana na Akili kubwa.

Kuibua mambo yepi? Hili la escrow liliibuliwa na gazeti la THE CITIZEN, na kupelekwa bungeni na kafulila,huyo zitto wako kakutana nalo huko kwa sababu ya kamati ya pac tu,Acha kubwabwaja ovyo! Hebu twambie majina ya uswis yapo wapi? Aliibua kumbe anataka mgao tu ili azimishwe ndo maana hadi kesho yupo kimya
 
Mnaishia kuwaona wenzenu wapuuzi,Naendelea kusimaia ukweli na ukweli siku zote unauma sasa nyie tukaneni lakini msg sent......Mmeumbuka

Naona unajitahidi kuonesha umiliki wa scandle ya escrow account kuwa ni wa Zitto. Pole,Hukuona mjadala wa Bunge la Bajeti ambapo ndo Kafulila alilivalia suala hili njuga, Kambi ya Upinzani ktka bajet mbadala za Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, suala hili lilishikiwa bango na wabunge wengi wa upinzani, waliolazimisha suala hili liende cag na pccb ni kambi ya upinzani waki- backup Kafulila, Zitto analiongelea sana kwa mamlaka kama Mwenyekiti wa pac ambao ndio watakaosoma ripoti hiyo,

Support kafulila kutoka kwa Viongozi wa kambi yake haupimiki, naomba umuulize yeye kafulila, kwa hiyo unachojaribu kukifanya, nakushauri rudi katafakari upya! Na unapoamua kuwa Muongi fanyia Uongo wako utafiti wa kutosha, na Muongo anapaswa kuwa na kumbukumbu. Na kwa watu wenye akili kama zako wanahitaji deliverence,Kick unazowatafutia watu hazina tija.Acha kazi wanazofanya kwa manufaa ya Taifa ziwe Appreciated na wananchi wenyewe kwani wataziona!
 
bikira wa Kimasai Ideally unaonyesha tu jinsi ulivyo MFITINISHI . Yaani tabia ya KUSUTANA. Badala yakumpongeza kafulila kwakuibua hoja ambayo inaleta matokeo CHANYA. wewe una create MAJUNGU NA FITINA. unachoangalia wewe tu ni mahusiano ya kisisa yalivyokuwa baina ya hawa wanasiasa na ushabiki wako.
 
Last edited by a moderator:
Walijua kuunga mkono ni kumkubali ZITTO kabwe wanayemtuhumu kutumiwa na CCM ambayo ameisimamia kidedea kuhusu ESCROW. Mimi nilishasema wapinzani hawana jipya.

Unaweza Kutwambia hoja ya Mabilion ya Uswis ipo wapi sasa? Alivyovuta tu mshiko toka kwa mafisadi kakaa kimya hadi sasa! MUULIZENI UZINDUZI WA GENGE LAKE LA ACT UPO LINI?
 
Walijua kuunga mkono ni kumkubali ZITTO kabwe wanayemtuhumu kutumiwa na CCM ambayo ameisimamia kidedea kuhusu ESCROW. Mimi nilishasema wapinzani hawana jipya.

Je! hii hoja iliibuliwa na Zitto au Kafulila? mbona mnayempigia chepuo hapa ni Zitto na si Kafulila? kajipangeni upya,mnachokifanya hakina tija yoyote kwa taifa hili,mnatunga uongo na kuanza kuushabikia, huku mkijisahau na kutoka nje ya mstari. Hizi ni akili za Kiroboto!
 
Post zingine bana, uchonganishi tupu!
 
Back
Top Bottom