josegorofani
Senior Member
- Aug 19, 2015
- 197
- 69
Mkazi wa Tandale kwa Tumbo jijini Dar es Salaam, Salum Abdallah, maarufu ‘Dama’ (40) ambaye ni mlemavu wa miguu, amepandishwa kizimbanzi katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kubaka na kumwingilia kinyume cha maumbile binti mwenye umri wa miaka 12 (jina linahifadhiwa.)
Mbele ya Hakimu, Boniphace Lihamwike, Wakili wa Serikali Tumaini Mfikwa, alidai kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kwanza la kubaka Juni 6, mwaka huu eneo la Tandale.
Katika shtaka la pili mnamo tarehe iliyotajwa hapo juu mtuhumiwa huyo alimwingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Hekima wilayani Kinondoni.
“Mshtakiwa ulimbaka na kisha kumwingilia kinyume na maumbile binti huyo na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake,” alidai Wakili Mfikwa.
Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kosa hilo ambapo hakimu Lihamwike alisema shtaka hilo linadhamana kisheria, hivyo alimtaka mtuhumiwa awe na wadhamini wawili wa uhakika watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni 2.
Nje ya mahakama ilidaiwa kuwa mshitakiwa ni dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) ambapo alikuwa akimpakia mara nyingi mwanafunzi huyo na baadaye alitumia mwanya huo kumbaka.
Chanzo: Mtanzania