nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Na Asha Bani - Mwanahalisi
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mkubwa katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa, uliotokana na kuwalipa wanafunzi hewa zaidi ya 37 fedha kutoka Bodi ya Mikopo nchini kwa mwaka 2010.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema waliwaita watendaji wa chuo hicho jana kujieleza na kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili, ikiwamo matumizi mabaya yasiyofuata sheria ya manunuzi katika nyanja mbalimbali yanayofikia sh bilioni 1.2 .
Zitto alisema wamebaini kuwa uongozi wa chuo hicho umeingiza majina hewa ya wanafunzi ambao wamelipwa sh milioni 66.
Alisema njia waliyokuwa wakiitumia kuingiza majina hayo ni mengine kubadilisha herufi za majina ya mwisho au mwanzo ya mwanafunzi husika, hivyo kuonekana si yule aliyepewa fedha.
Mwenyekiti huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wana vielelezo vingi vinavyoonyesha majina ya wahusika kufanyiwa mchezo kwa lengo la uongozi wa chuo hicho kujinufaisha.
"Hii ni hatari sana, majina ya wanafunzi 37 wanalipwa fedha za umma huku wanafunzi wengine katika vyuo mbalimbali wakiwa wanakimbizana na askari polisi wanapigwa huku chuo hiki kikiwa kinafuja fedha kwa kufanya mambo yasiyo ya maana kwa taifa," alisema Zitto.
Mbali na wanafunzi hewa, kamati pia ilibaini chuo hicho kuajiri wafanyakazi hewa ambao hawakutajwa idadi yao, ambao kila mwezi wanaingiziwa kiasi cha sh milioni 1.4 zikiwa ni mishahara.
Zitto alitolea mfano wa majina mawili ya wafanyakazi ambao ni Francis Kiama na Damas Kadewele walioonekana kushiriki kwenye ubadhirifu lakini hadi sasa wapo kwenye ofisi za umma wakiendelea kulipwa fedha za walipa kodi ilhali wamefanya madudu.
"Huyu Kiama Francis kila sehemu zenye ubadhirifu wa fedha jina lake limo, anatajwa na CAG alishauri, lakini ninyi mmechukua hatua gani? Badala yake mnamwamisha kitengo, huo ni mzaha, kwa kuwa mnatumia fedha za umma vibaya," alisema Zitto.
Maswali hayo ya Zitto yaliwafanya baadhi ya watendaji waliohudhuria kikao hicho kupata wakati mgumu wa kuyatolea ufanunuzi, hivyo kukiri kufanya uzembe kwenye utendaji kazi.
Watendaji hao walisema bahati mbaya risiti za utunzaji wa kumbukumbu zimepotea na kuomba wasamehewe na kamati hiyo.
Akijibu tuhuma hizo, Mkuu wa Chuo hicho, Christopher Enock, alikiri kufanyika kwa uzembe wa kutotunza risiti huku akidai kuwa chuo kilikuwa kichanga, hivyo hakikuweza kutunza kumbukumbu zozote.
Utetezi huo ulimkera Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, ambaye alitoa karipio kwa kuwaambia watendaji hao hataki kusikia kauli hiyo.
Awali Zitto alitaka kujua sababu za kutofuata sheria ya manunuzi mbalimbali yakiwamo ya dawa zilizogharimu kiasi cha sh milioni 267 na manunuzi mengine yakiwa na jumla ya sh milioni 504.
Zitto alihoji sababu ya kutotumia sheria ya manunuzi katika ujenzi wa chuo hicho ambapo kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) jumla ya sh milioni 717 zilitumika katika ujenzi usiozingatia sheria hiyo.
Mapendekezo baada ya kubaini ubadhirifu
Zitto alisema kamati imeamua kuunda tume itakayoongozwa na Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibara na Khamisi Khalifa na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Kawawa ili kuchunguza tuhuma hizo.
Aidha, alisema kutokana na shaka waliyoipata katika chuo hicho, itawalazimu kufanya uchunguzi katika vyuo vingine vinavyopata mikopo kutoka serikalini na kubaini vyuo ambavyo havifuati taratibu za manunuzi.
Kutokana na hali hiyo, aliyemwakilisha mkuu wa bodi, Profesa Rwekaza Mukandara, aliyejitambulisha kuwa ni Profesa Stella Bhalakusesa, amesema hakufurahishwa na hatua hiyo na kwamba na wao watalifuatilia kwa ukaribu kuona mwisho wake.
Baada ya kumalizika kikao hicho, mkuu wa chuo aliwakimbia waandishi wa habari kutokana na kutotaka kuelezea yaliyojiri na sababu za kufikiwa kwa hatua hiyo, ambapo waandishi walimfuata hadi nje ya jengo la kumbi za Bunge.