Mkwawa University: Wanafunzi hewa watafuna mil. 66/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkwawa University: Wanafunzi hewa watafuna mil. 66/-

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nngu007, Jan 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Asha Bani - Mwanahalisi

  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mkubwa katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa, uliotokana na kuwalipa wanafunzi hewa zaidi ya 37 fedha kutoka Bodi ya Mikopo nchini kwa mwaka 2010.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema waliwaita watendaji wa chuo hicho jana kujieleza na kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili, ikiwamo matumizi mabaya yasiyofuata sheria ya manunuzi katika nyanja mbalimbali yanayofikia sh bilioni 1.2 .


  Zitto alisema wamebaini kuwa uongozi wa chuo hicho umeingiza majina hewa ya wanafunzi ambao wamelipwa sh milioni 66.


  Alisema njia waliyokuwa wakiitumia kuingiza majina hayo ni mengine kubadilisha herufi za majina ya mwisho au mwanzo ya mwanafunzi husika, hivyo kuonekana si yule aliyepewa fedha.


  Mwenyekiti huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wana vielelezo vingi vinavyoonyesha majina ya wahusika kufanyiwa mchezo kwa lengo la uongozi wa chuo hicho kujinufaisha.


  "Hii ni hatari sana, majina ya wanafunzi 37 wanalipwa fedha za umma huku wanafunzi wengine katika vyuo mbalimbali wakiwa wanakimbizana na askari polisi wanapigwa huku chuo hiki kikiwa kinafuja fedha kwa kufanya mambo yasiyo ya maana kwa taifa," alisema Zitto.


  Mbali na wanafunzi hewa, kamati pia ilibaini chuo hicho kuajiri wafanyakazi hewa ambao hawakutajwa idadi yao, ambao kila mwezi wanaingiziwa kiasi cha sh milioni 1.4 zikiwa ni mishahara.


  Zitto alitolea mfano wa majina mawili ya wafanyakazi ambao ni Francis Kiama na Damas Kadewele walioonekana kushiriki kwenye ubadhirifu lakini hadi sasa wapo kwenye ofisi za umma wakiendelea kulipwa fedha za walipa kodi ilhali wamefanya madudu.


  "Huyu Kiama Francis kila sehemu zenye ubadhirifu wa fedha jina lake limo, anatajwa na CAG alishauri, lakini ninyi mmechukua hatua gani? Badala yake mnamwamisha kitengo, huo ni mzaha, kwa kuwa mnatumia fedha za umma vibaya," alisema Zitto.


  Maswali hayo ya Zitto yaliwafanya baadhi ya watendaji waliohudhuria kikao hicho kupata wakati mgumu wa kuyatolea ufanunuzi, hivyo kukiri kufanya uzembe kwenye utendaji kazi.


  Watendaji hao walisema bahati mbaya risiti za utunzaji wa kumbukumbu zimepotea na kuomba wasamehewe na kamati hiyo.


  Akijibu tuhuma hizo, Mkuu wa Chuo hicho, Christopher Enock, alikiri kufanyika kwa uzembe wa kutotunza risiti huku akidai kuwa chuo kilikuwa kichanga, hivyo hakikuweza kutunza kumbukumbu zozote.


  Utetezi huo ulimkera Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, ambaye alitoa karipio kwa kuwaambia watendaji hao hataki kusikia kauli hiyo.


  Awali Zitto alitaka kujua sababu za kutofuata sheria ya manunuzi mbalimbali yakiwamo ya dawa zilizogharimu kiasi cha sh milioni 267 na manunuzi mengine yakiwa na jumla ya sh milioni 504.


  Zitto alihoji sababu ya kutotumia sheria ya manunuzi katika ujenzi wa chuo hicho ambapo kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) jumla ya sh milioni 717 zilitumika katika ujenzi usiozingatia sheria hiyo.


  Mapendekezo baada ya kubaini ubadhirifu

  Zitto alisema kamati imeamua kuunda tume itakayoongozwa na Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibara na Khamisi Khalifa na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Kawawa ili kuchunguza tuhuma hizo.

  Aidha, alisema kutokana na shaka waliyoipata katika chuo hicho, itawalazimu kufanya uchunguzi katika vyuo vingine vinavyopata mikopo kutoka serikalini na kubaini vyuo ambavyo havifuati taratibu za manunuzi.


  Kutokana na hali hiyo, aliyemwakilisha mkuu wa bodi, Profesa Rwekaza Mukandara, aliyejitambulisha kuwa ni Profesa Stella Bhalakusesa, amesema hakufurahishwa na hatua hiyo na kwamba na wao watalifuatilia kwa ukaribu kuona mwisho wake.


  Baada ya kumalizika kikao hicho, mkuu wa chuo aliwakimbia waandishi wa habari kutokana na kutotaka kuelezea yaliyojiri na sababu za kufikiwa kwa hatua hiyo, ambapo waandishi walimfuata hadi nje ya jengo la kumbi za Bunge.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndio Maana kila mtu anapata anapata pesa ya petroli akiwa wizarani kula hela za wanafunzi hewa... yaaani hizo Milioni 66 kila mwaka
   
 3. p

  peter mlokota Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli mungu hayupo kwa wizi huu
  kwan watu wamejaa pepo za kitajiri tu ili wajambishe kitaa
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Serikali legelege ya jk!
  Na bado
   
 5. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Inauma tena inakera mno.Kuna wanafunzi hapa Mkwawa wanaishi kwa taabu mno kumbe Prof anakula pesa kifisadi.Chuo hata bado hakijajitosheleza kimiundombinu hasa kwa vifaa vya kujifunzia na majengo halafu eti unaskia mkuu wa chuo anabwia pesa.Kama wasomi wanaona kula pesa ndo jambo la maana basi wahamie kwenye siasa ambako hela huliwa kilaini.OVYO KABISA
   
 6. N

  NDWAARI New Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bajeti ya mkwawa kukukataliwa na kamati ya bunge ni swala la kuipongeza kamati hiyo kwani inafanya kazi ipazavyo..lakini isiishie hapo lazima walioiandaa wawajibishwe kwani walikuwa wana lengo la kuibia serekali.....mkwawa kuna uvujaji wa fedha wa aina nyingi hehu wadau fuatilieni hillo. Inasikitisha kuona prof anawakimbia waandishi wa habari..
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hahahahah
  jamaa wanasema wasamehewe,jaman,jaman,jamaniii!
  HEBU TUJIULIZE HAWA WAFANYAO UBADHILIFU HUWA WANACHUKULIWA HATUA GANI?
   
 8. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  naomba nchi hii ingegeuka kuwa China.
   
 9. d

  davidie JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi inayofanana na shamba kubwa la miti ambalo linashambuliwa na mchwa mwishoweshamba litateketea, maskini nchi yetu!!
   
 10. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sina hata cha kusema.
   
 11. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwani ndo mnagundua leo kuwa kuna uwizi?
   
 12. s

  sojak Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Its too late,but sheria ichukue mkondo wake na muelewe kwamba ufisadi kila kona ktk sekta za umma.take care
   
 13. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,245
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  :eyebrows:Haya mbona ya kawaida! Mkwawa ni kataasisi kadogo sana,
  kuna uozo sehemu nyingi kubwa kubwa tu lakini kama hawaoni vile!
  kamati ya Bunge isitafute SIFA za KIJINGA!
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ukiongeza na zile 91 za yule dada wa bodi unakopesha wanafunzi wangapi? Wanachuo wakigoma wanaitiwa mbwa wa jk. Ukombozi unakuja, upo mpakani mwa nchi.
   
 15. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,245
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Mhhhh, kwanza Tz hakuna Waandishi wa Habari wale Ni
  "WAANDISI wa HABARI" ndo maana hata vijiswali wanavyouliza vinapandana!
  ukisoma Tanzania Daima ya 26/01/2012 utaona mkanganyiko wa habari
  juu ya Mkwawa! Hivi mkuu wa Chuo anaitwa CHRISTOPHER Enock?
  Naghambire, very stupid aise!

   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,732
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  Serikali legelege..
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  hizi kamati za kudumu za bunge zinatakiwa ziongezewe nguvu za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafakisha mahakamani wezi kama hawa na kuchukua hatua papo hapo kama kuwasimamisha kazi watuhumiwa
   
 18. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inatia aibu kwa Mwandishi wa habari hata hajui jina la Mkuu wa chuo. Hivi huyu Christopher Enock ni nani na yuko wapi? Kwa nini jina lake liandikwe kama mkuu wa chuo wakati mkuu wa chuo anafahamika? Duh, aibu
   
 19. LACHERO

  LACHERO JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 434
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 60
  :hatari::hatari::hatari:
   
 20. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya matatizo mengine ni ya kujitakia tu na kuto kwenda na wakati. Pesa zinapigishwa misele kutoka wizara, kwenda point A, point B point C point D, kabla hazijamfikia mlengwa, hii situation ilikuwa enzi zile! ambazo mambo ya benki kulikuwa hamna, ndio pesa ilibidi zifanye hizi safari.
  Leo, wizara, mfano ya elimu inajua ni wanafunzi wangapi wapepangwa katika kila chuo (ndio hata hapa situation ya ulaji ipo), hence kwa nini watume pesa chuoni ambapo zitamungunywa na hawa viongozi? Pesa za shule, sawa ndio zitaenda huko direct, lakini za maintenance ya student, kwa nini zisitumwe straight kwa student?
  Hii ishu ya "ghost" workers/beneficiary au student inabidi ifanyiwe kazi....
   
Loading...