Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,853
Kutokana na ratiba iliyotangazwa mwaka jana ilitakiwa kufikia mwaka huu walau kuwe na wizara tatu ziwe tayari Dodoma
Kumekuwa na mikwamo katika hili...waziri mkuu ameweza kuhamia lakini kiuhalisia muda mwingi hakai huko, mambo mengi ya kiserikali bado yanafanyika Dar es salaam! Pengine hata mahitaji ya nyakati yamechangia
Zinaweza kutolewa sababu lukuki na visingizio si haba lakini kuna jambo muhimu sana halikuzingatiwa!!! Nalo si jingine bali ni mila na desturi! Matambiko mizimu na kuheshimu mambo ya
jadi
Pamoja na kuwa 'brainwashed' na imani na elimu ya wageni lakini bado mila na desturi zetu zina nguvu sana na yeyote aliyejaribu kuzidharau amepata habari yake
Dodoma pale mlimani kuna simulizi zisizokoma kuhusiana na hilo..japo watu wanasimuliana kwa kificho na kwa woga...wanasisitiza kuwa wazee wa mila mababu na mizimu hawakuombwa ruhusa, walitengwa na hawakushirikishwa ili watoe baraka na ruhusa! Wanasisitiza kuwa kuufanya mji fulani kuwa ndio kitovu na kuvikwa taji la mji mkuu wa nchi sio jambo dogo hata kidogo
Ni jambo linalohusika na mabilioni ya shilingi mwingiliano wa mila na tamaduni mbalimbali ndani na nje ya nchi, ni jambo ambayo maandalizi na utekelezaji wake unatakiwa kwenda sambamba kidunia na kiroho ....hili wanasema halikufanyika na kwa imani hata za kidini jambo lolote lisipopata baraka za kiroho katika ulimwengu usioonekana ni vigumu kutekelezeka hata katika ulimwengu wa nuru sayansi na technologia
Kama miradi ya kawaida kama madaraja barabara majengo viwanda nk vinafanyiwa matambiko sembuse mji mkuu?
Kuna kitu hakikutiliwa maanani kwenye mradi mzima wa kuhamia Dodoma..kitu hiki kikiendelea kudharauliwa kitaendelea kupukutisha watendaji wengi pale penye kitovu na kuhamia Dodoma kutabaki kuwa story za kufikirika