Mkwamo AGM ya UNA Tanzania

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
UNA Leaders.png

Asasi ya Umoja wa Mataifa iliyosajiliwa Tanzania, maarufu kama United Nations Association of Tanzania (UNA Tanzania), taasisi yenye jukumu la kuzileta kazi za Umoja wa Mataifa karibu na Watazania, imepanga mkutano mkuu wa mwaka 2018 ufanyike tarehe 21 Aprili mwaka huu, huku zaidi ya asilimia 40 ya wajumbe halali wa mkutano huo wakitelekezwa.

Mkutano huo ambao, kwa mujibu wa Katiba unapaswa kufanyika kila mwaka, kwa mara ya mwisho ilifanyika Mei 2016, siku ambayo Mwenyekiti wa Bodi mpya ya UNA Tanzania pamoja na Bodi yake walisimikwa.

Mkutano wa Mwaka huu utakuwa na ajenda yenye vipengele nane. Vipengele hivyo ni: Kifungua; kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2016; Taarifa ya utendaji kazi ya mwaka 2016 na 2017; Taarifa ya fedha ya mwaka 2016 na 2017; Mpango mkakati wa mwaka 2018-2022; Taarufa za kazi za matawi; Mengineyo; na Kufunga.

Tangu 2016 mpaka sasa, hakuna mrejesho wowote wa taarifa za kiutendaji na kifedha ambao umewahi kufanywa na Bodi ya UNA Tanzania kwa kutoa taarifa kwa wanachama kwa mujibu wa Katiba.

Kwa mujibu wa nakala ya barua ya mwaliko kwa “wanachama walioko matawini” aliyonayo mwandishi, mkutano mkuu wa mwaka huu “utafanyika tarehe 21 Aprili 2018, kwenye ukumbi wa British Council, jijini Dar es Salaam, tangu saa 3.00 asubuhi.”

Hata hivyo, ibara ya X(15)(c) ya Katiba ya UNA Tanzania, toleo la 2014, inatamka kuwa, “Mkutano Mkuu wa Mwaka utafanyika kati ya Januari na Machi.”

Barua ya mwaliko iliyo na kichwa cha maneno “Mwaliko wa Kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka” imesainiwa na Katibu Mkuu wa UNA Tanzania, Reynald Maeda. Kisha, ofisi ya Katibu Mkuu ikasambaza barua hiyo kwa njia ya barua pepe kwenda kwa wanachama wachache waliochaguliwa kwa utaratibu usiojulikana kikatiba.

Pamoja na kusambazwa kwa barua hiyo rasmi ya mwaliko kwa wanachama wachache waliochaguliwa kisiri, Ofisi ya Katibu Mkuu imeandika barua pepe kwa wanachama hao kutoa ufafanuzi wa ziada kuhusu utaratibu wa kuendesha Mkutani Mkuu ujao.

“Uwakilishi wa wanachama walioko matawini usizidi wanachama watatu,” inasema Ofisi ya Katibu Mkuu katika barua pepe iliyosindikiza barua ya mwaliko.

Hata hivyo, ibara ya X(17)(a) ya Katiba ya UNA Tanzania, toleo la 2014, inasema kuwa kila tawi litawakilishwa na wanachama wasiozidi watano wenye haki ya kupiga kura. Kwa upande mwingine, ibara ya X(17)(b) inaelekeza kuwa mbali na wanachama watano wenye haki ya kupiga kura, tawi linaweza kuwakilishwa na wanachama wengine wasiozidi watano wasio na haki ya kupiga kura.

Taasisi ya UNA Tanzania inayo matawi saba. Yaani, tawi la Kagera, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Temeke na Zanzibar. Ofisi ya Katibu Mkuu haijapeleka mwaliko wa Mkutano Mkuu ujao kwa baadhi ya viongozi wakuu na wanachama wa matawi haya, na hakuna sababu zozote zilizotolewa.

Barua ya kuwaalika wajumbe wa Mkutano Mkuu imetumwa kimya kimya kwa wajumbe wachache tu, kupitia akaunti zao za barua pepe, tena bila kutaja ajenda za Mkutano Mkuu wala kiambatanisho chochote cha ripoti utendaji na fedha zinazopaswa kujadiliwa katika mkutano huo.

Hata hivyo, Katiba ya UNA Tanzania toleo la 2014, kwenye ibara ya X(15)(d) inasema kwamba, “mwaliko wa maandishi ukitaja dhamira ya kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka, pamoja na nakala ya ajenda, vitatumwa kwa kila mwanachama wa taasisi ya UNA Tanzania.”

Kwa sababu ya matakwa haya ya kikatiba, ulijengeka utamaduni wa kuhakikisha kwamba mialiko ya Mikutano Mikuu inatumwa kwa wanachama wote na kubandikwa kwenye tovuti ya UNA Tanzania. Hata hivyo, mwaka huu, mambo haya mawili hayajafanyika.

Barua pepe iliyoandikwa na ofisi ya Katibu Mkuu inasema kwamba, kwa wajumbe waalikwa wanaotoka kwenye matawi yaliyo nje ya Dar es Salaam, taasisi itabeba gharama za kujikimu kwa siku mbili, kiasi cha TZS 65,000/= kwa siku; kwamba, itawarudishia nauli ya basi baada ya kuwasilisha tiketi halisi ya basi; kwamba, italipa nauli kutoka ukumbini mpaka kituo cha basi, kiasi cha TZS 20,000/=; na kwamba, italipa nauli kutoka kituo cha basi mpaka ukumbini, kiasi cha TZS 20,000/=.

Kisha ofisi ya Katibu Mkuu inamalizia mwongozo wake kwa kusema kwamba, kwa wajumbe waalikwa wanaotoka kwenye matawi yaliyoko ndani ya Mkoa wa Dar Es Salaam kama vile tawi la Temeke, taasisi italipa nauli kutoka ukumbini mpaka kituo cha basi, kiasi cha TZS 20,000/=; na pia nauli ya kutoka nyumbani kuja ukumbini, kiasi cha TZS 20,000/= pekee.

Kwa mujibu wa bajeti hii, na kwa kuzingatia kwamba kuna matawi saba, ambayo kikatiba yanapaswa kutuma wajumba wa lazima wasiozidi watano, ni wazi kwamba bajeti ya mkutano mzima sio zaidi ya TZS 12 milioni. Miaka miwili ya maandalizi ingetosha kutafita fedha hii kwa ufanisi kusudi Mkutano Mkuu wenye uwakilishi mpana na wajumbe makini ufanyike.

Kiutawala, UNA Tanzania inavyo vyombo vitatu vya maamuzi. Mkutano Mkuu ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi. Mkutano Mkuu unapokuwa hauko kazini, madaraka ya taasisi yanakuwa mikononi mwa Bodi inayoongozwa na Mwenyekiti. Na Bodi inapokuwa haiko kazini, madaraka yote ya taasisi yanakuwa mikononi mwa Sekretariati, inayoongozwa na Katibu Mkuu.

Sekretariati inaendesha shughuli za kila siku za taasisi na inao wajibu wa kuitisha Mkutani wa Bodi kila inapobidi; Bodi inapaswa kukutana kila baada ya miezi mitatu na inao wajibu wa kuitisha Mkutani Mkuu kila inapobidi; na Mkutano Mkuu unapaswa kufanyika kila baada ya mwaka mmoja ili kutathmini utendaji wa mwaka uliopita na kuweka mikakati ya mwaka ujao.

Hivyo, Bodi kushindwa kuitisha Mkutano Mkuu wa mwaka kwa wakati ni jaribio la kupora madaraka ya wajumbe wa mkutano Mkuu, kuwanyima fursa ya kuweka dira ya taasisi, na hivyo kuididimiza taasisi.

Tangu 2016 mpaka 2019, wajumbe muhimu wa Bodi ya UNA Tanzania ni Mwenyekiti Malli Sillesi, Makamu Mwenyekiti Benedict Kikove, Katibu Mkuu Reynald Maeda, Naibu Katibu Mkuu Sarah Edgar, Ibrahim Bakari, Subira Bawji, Lilian Kwimage, Jamila Ally, Ally Hamisi, na Erick Thomas. Tayari mjumbe mmoja amejiuzulu kwa sababu ya kukerwa na mwenendo wa Mwenyekiti.

Mwandishi alimtafuta kwa simu Mwenyekiti wa UNA Tanzania, Malli Sillesi, ili afafanue utata unaoyagubika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2018, lakini Sillesi akasema maswali yote aulizwe Katibu Mkuu anayefanya maandalizi ya Mkutano huo.

Naye Katibu Mkuu wa UNA Tanzania, Reynald Maeda, alipotafutwa kwa simu, alikataa kujibu maswali aliyoulizwa kwa maelezo kwamba, msemaji mkuu wa taasisi ni Mwenyekiti.

Ibara ya IX(14)(a)(i) ya Katiba ya UNA Tanzania, toleo la 2014, inamtambua Mwenyekiti kama msemaji mkuu wa taasisi.

Kwa viwango vyovyote vile, huu ni mkwamo wa kitaasisi unaopaswa kushughulikiwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu ujao, hasa wale wenye mapenzi mema na tasisi ya UNA Tanzania.

====================APPENDICES=======================
UNA AGM Invitation.png

UNA Invitation Letter-2.png

UNA AGM Invitation-3.png
 
HAKUNA TAASISI WEZI KAMA HII. NIMEKUWA MWANACHAMA TANGU A LEVEL MPAKA DEGREE, LAKINI WANAKULA PESA TU WALA SIONI MAANA YAKE.
 
Mama Amon
.
Bee!
Mie Katibu wa Tawi, hata kualikwa hakuna?
Roho inaniuma sana!

Halafu sisi watu tuliookoka hatupendi haya....

Namwomba Mungu huyu Mwenyekiti apigwe na radi, haki ya Mungu...
 
Back
Top Bottom