Mkuu wa Wilaya ya Same ndugu Herman Kapufi ni Jipu atumbuliwe

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
15,417
Kuna mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Nasuro jirani na shule ya sekondari Islamic Kirinjiko ambapo mtu mmoja anayejiita mwekezaji aitwaye Isaya Malongoza alivamia kijiji hicho na kuzungusha uzio kuzunguka nyumba za wakaazi wa kijiji hicho ukubwa ekari 100 huku nyumba za wakazi wa kijiji hicho na maboma ya mifugo yao yakiwa ndani ya uzio huo.

Mwekezaji huyo pia ameharibu mazao ya wakazi wa kijiji hicho na kuwazuia kuendelea na shughuli za kilimo jambo ambalo limewaweka wakazi hao katika wakati mgumu.

mgogoro huo ambao unaonekana kulelewa na mkuu wa Wilaya same ulianza mwaka 2013 mpaka sasa haujapatiwa ufumbuzi pamoja na wakazi hao kuhusisha ofisi ya taasisi ya kuzuia Rushwa Wilaya ya Same.

Pamoja jitihada za Mkurugenzi wa Wilaya ya Same kutaka kutatua mgogoro huo lakini amekuwa akikwamishwa na Mkuu wa Wilaya.

Hivi sasa wakazi wa kijiji hicho wameandika barua kwa Mkuu wa mkoa ndugu Mecky Sadick lakini bado hawajajibiwa.

Wakazi hao sasa wanataka kumuona Waziri wa Ardhi ndugu William Lukuvi

Nitaambatanisha nakala za barua za mgogoro huu kwani niko huku kijijini sijapata Photo Copy.

Asha1.jpeg
Asha2.jpeg
Asha3.jpeg
Asha4.jpeg
Asha5.jpeg
 
Tukishirikiana hivi kwa kutumia mamlaka tuliyopewa ya kuwa walinzi wa mali na amali zetu wenyewe kabla ya kwenda kwa vyombo vingine vya ulinzi tutafika kwenye pwani ya ahadi...bravo Mtambuzi...ujumbe umefika!
 
Herman Kapufi-SAME, Lemrus Kipuyo-ROMBO,Shaib Ndemanga-MWANGA,Charles Mlingwa-SIHA,Novatus Makunga-MOSHI,Anton Mtaka alikuwa HAI.
 
bado kuna taarifa ya vikao nitaiweka hapa ambayo iliamuliwa muwekezaji huyo aondoke katika eneo hilo
 
lakini amekuwa akikingiwa kifua na mkuu wa wilaya kwa kile kinachoonekana kupewa mlungula na mwekezaji huyo mvamizi
 
Huyu jamaa kupelekwa Geita ni kuendelea kumlinda alitakiwa atumbuliwe kabisa, hata sijui kama JPM hajapata hizi taarifa?
Huu mgogoro ameulea mpaka sasa umeshafika kwa waziri wa ardhi acha tuendelee kupambana mpaka kitaeleweka.
 
Hermani Imaculatha Kapufi amedumaza sana maendeleo ya Same kwa kushirikiana na mafisadi wanaojiita wawekezaji. Amesababisha migogoro mingi ya ardhi ikiwemo ule wa wamasai wa Ruvu waliomchana live mbele ya mkuu wa mkoa kuwa alipewa rushwa ya mil.5, ameshirikiana na Willy enterprises kutorosha madini huko SHENGENA. Inasemekana Willy Enterprises ndiye alifadhili kampeni zake za kuwania ubunge huko kwao Katavi. Kwa kweli JPM alitakiwa amtumbue kabisa huyu jamaa na si kumpeleka Geita. Kazi kupiga vibonzo visivyo na maana tu!
 
Back
Top Bottom