Mkuu wa Wilaya ya Kongwa apiga marufuku wananchi kutumia nafaka kutengeneza pombe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amepiga marufuku matumizi ya nafaka kutengenezea pombe za kienyeji ili kujikinga na baa la njaa.

Ndejembi amesema kumekuwa na tabia ya wananchi kufanya sherehe zisizokuwa na tija ikiwemo zile za jando na ngoma za asili kwa kutumia nafaka.

Akizungumza na Idara ya Habari, Ndejembi amesema hivi sasa wilayani Kongwa kipo chakula cha kutosha majumbani, sokoni na kwenye maghala yanayotumika kuhifadhi chakula.

Amesema chakula kilichopo kikitumika vizuri kitawatosheleza wananchi mpaka pale watakapovuna mazao mengine katika msimu wa mavuno ujao.

“Kongwa chakula kipo cha kutosha, wanaosema hakuna chakula ni wafanyabiashara wanaotaka kuzua hofu ili wapandishe bei ya mazao na wanasiasa waliokosa ajenda,” alisema Ndejembi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hakuna sababu ya kuficha kama itatokea kuna upungufu wa chakula lakini kwa sasa hakuna upungufu wowote wa chakula wilayani Kongwa.

Ndejembi amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula yaliyopo Kibaigwa wilayani Kongwa ambako pia kuna soko la mahindi la kimataifa na kujiridhisha na chakula kilichopo.

“Mahindi yapo ya kutosha na kama unavyojua hili ni soko la Kimataifa inamaana kungekuwa na upungufu ungeanzia hapa,” alisema Ndejembi.

Chanzo: Mo Dewji Blog
 
Baa la njaa hakuna,tumetangaziwa,huyu mbona anazuia watu wasinywe kimpumu ili kuepuka njaa?

Mnatuchanganya
 
"Huu ni wakati wa wakulima kufaidi, uzeni chakula bei mnazotaka na sitaki kuona mtu yeyote wa serikali kuingilia bei, asietaka kununua akafe na njaa. Tena wenye ng'ombe wakija muuuzie debe moja kwa ng'ombe tatu."
Mtakatifu Rais Magufuli ...Simiyu
 
Ndio madhara ya kuropoka haya
 
Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amepiga marufuku matumizi ya nafaka kutengenezea pombe za kienyeji ili kujikinga na baa la njaa.

Ndejembi amesema kumekuwa na tabia ya wananchi kufanya sherehe zisizokuwa na tija ikiwemo zile za jando na ngoma za asili kwa kutumia nafaka.

Akizungumza na Idara ya Habari, Ndejembi amesema hivi sasa wilayani Kongwa kipo chakula cha kutosha majumbani, sokoni na kwenye maghala yanayotumika kuhifadhi chakula.

Amesema chakula kilichopo kikitumika vizuri kitawatosheleza wananchi mpaka pale watakapovuna mazao mengine katika msimu wa mavuno ujao.

“Kongwa chakula kipo cha kutosha, wanaosema hakuna chakula ni wafanyabiashara wanaotaka kuzua hofu ili wapandishe bei ya mazao na wanasiasa waliokosa ajenda,” alisema Ndejembi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hakuna sababu ya kuficha kama itatokea kuna upungufu wa chakula lakini kwa sasa hakuna upungufu wowote wa chakula wilayani Kongwa.

Ndejembi amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula yaliyopo Kibaigwa wilayani Kongwa ambako pia kuna soko la mahindi la kimataifa na kujiridhisha na chakula kilichopo.

“Mahindi yapo ya kutosha na kama unavyojua hili ni soko la Kimataifa inamaana kungekuwa na upungufu ungeanzia hapa,” alisema Ndejembi.

Chanzo: Mo Dewji Blog
Safi sana mkuu wa wilaya ila angalieni hizo marufuku marufuku zisizidi mpipaka
 
Pombe za kienyeji ni moja ya starehe chache zinazopatikana maeneo ya vijijini DC alitambue hilo.
 
DC naye aache kunywa bia, na afunge baa zote,bia zinatumia nafaka,haiwezekani uwepo ubaguzi kati ya wanaokunywa kangala na wanaokunywa bia,zote zinatumia nafaka
 
DC naye aache kunywa bia, na afunge baa zote,bia zinatumia nafaka,haiwezekani uwepo ubaguzi kati ya wanaokunywa kangala na wanaokunywa via,zote zinatumia nafaka
kweli waseme hakuna kunywa pombe tanzania nzima bora kuwahi nyumbani kufyatua ila kwa hali hii ukifyatua mmm sipati picha
 
Kongwa hii hii ninayoijua Mimi ndo haina njaa!!!!! Aisee nenda kijiji cha Machenje halafu urudi hapa utueleze ulichokutana nacho hapo..
 
huyo mkuu wa wilaya kapiga viroba nini??hivi hamsikilizi hata mwajiri wake??ninamshauri akasikilize hotuba ya mwajiri wake akiwa simiyu.
 
Kwani amelima yeye,Serikali itoe chakula cha msaada iache visingizio
 
Back
Top Bottom