NFRA yaja na mizani ya Kidijitali kupima mazao, kuondoa wasiwasi wa vipimo, kuongeza ufanisi wa kutunza kumbukumbu

informer 06

Member
May 11, 2024
44
26
Wakala wa Uhifadhi wa Chakula Nchini (NFRA) umeanza rasmi kutumia mfumo wa kidijitali katika kupima mazao ya nafaka, hatua ambayo imeelezwa kuwa itakuwa na tija kwa pande zote mbili ikiwemo wakulima kuondoa wasiwasi wa vipimo pale wanapouza mazao yao kwenye mamlaka hiyo.

Hatua hiyo imeelezwa na Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt.Andrew Komba ambaye katika maonesho ya wakulima na wafugaji, Wavuvi viwanja vya Nane nane Nzuguni jijini Dodoma yaliyoanza Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 8, 2024.
IMG_5602.jpeg

Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt.Andrew Komba

Ambapo amesema utaratibu huo unalenga kumuwezesha Mkulima kuwa na uhakika katika vipimo anapouza mazao yake NFRA jambo ambalo amedai kuwa ni hatua yenye tija.

"Wakulima wameipokea mizani hii vizuri wakiamini kwamba inawawezesha kupata kiwango sahihi wanachotuuzia na sisi kwetu inatupa kumbukumbu sahihi kwa sababu inaingiza taarifa katika mfumo ambao unatumika katika suala zima la kuhifadhi ."amesema Dkt. Komba

Aidha amesema ,Wakala huo una jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula .

Ambapo Dkt.Komba amebainisha wazi kuwa ili kulitekeleza jukumu hilo, NFRA wamekuwa wakinunua na kukusanya chakula na kuhifadhi vizuri kwa utaratibu wa kuhakikisha afya na usalama wa mlaji.

"Kwa hili kuhakikisha chakula kinakuwa salama wakati wote, tunatumia maghala na vihenge katika kuhifadhi chakula,lakini pia tunawafundisha wakulima kuhifadhi chakula wanacholima katika hali ya usalama badala ya kuhifadhi kizamani."amesema Dkt.Komba

Amesema chakula wanachohifadhi kinalenga kuisaidia jamii pale panapotokea uhaba wa chakula na hivyo kutumia akiba hiyo kukidhi mahitaji.
IMG_5604.jpeg


IMG_5603.jpeg
 
Back
Top Bottom