Mkuu wa Wilaya ya Kilombero apiga marufuku kufanya sherehe bila kibali...

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,911
Mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo amepiga marufuku mtu yeyote kufanya sherehe bila kibali kutoka kwa mtendaji wa eneo husika ikiwa ni pamoja na kuuza chakula kiholela kama njia ya kuthibiti utumiaji hovyo wa chakula.

Ihunyo amesema ameamua kupiga marufuku hiyo ili kuthibiti utumiaji hovyo wa chakula kilichopatikana msimu huu wa mavuno na kujikinga na baa la njaa katika wilaya yake.

Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilombero akiongea leo kwenye kikao cha baraza la madiwani la mji wa Ifakara Ihunyo amesema serikali yake ya wilaya imejipanga kuhakikisha sherehe zisizo za lazima hazifanyiki na kuwataka Watendaji na Madiwani kushirikiana kukemea vitendo hivyo.

Mbali na hilo Diwani wa Kata ya Viwanja Stini amelalamika ucheleweshaji wa fedha kutoka serikali kuu na kudai jambo hilo linakuwa linakwamisha mipango ya maendeleo katika halmshauri hiyo na kata zake.

Awali kabla ya kikao hicho kuanza Mbunge viti maalum mkoa wa Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mchungaji Getruda Lwakatare aliapishwa kuwa mjumbe kamili wa baraza hilo la madiwani.

My take:

Hawa wakuu wa wilaya wamekuwa kama mzigo kwa wananchi. kwa maagizo yasiyo isha na hii yote hii ni kutokana hawajui machungu ya kuchaguliwa na wananchi.

na ndio maana wamekuwa walopokaji isivyo kawaida.
Kama imgewezekana hii nafasi ya ukuu wa wilaya ingefutwa kabisa kwa sababu hamna kitu wanacho wasaidia wananchi.

Embe fikiria kwa akili ya kawaida tu.mtu ukitaka kumuwekea mtoto happy birthday. mkuu wa wilaya anakuambia hadi ukachukue kibali serikalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo sheria zipo nchi nzima.. Sema watu hawazitekelezi tuu...

Na kuwaletea usumbufu watu wengine...


Cc: mahondaw
 
Hapa yuko sahihi, huu utaratibu upo sana kwetu huku.

Una sherehe ya aina yoyote ile ni lazima uende kwa mtendaji akupe Kibali (hawezi akakunyima) hii itakulinda pindi litokeapo tatizo hapo penye sherehe na tukumbuke sherehe zingine zinakwenda mpaka usiku lolote linaweza kutokea.
 
Nasema kila siku, nchi hii ukifikiria saaaana, unaweza kunywa sumu utangulie kwa Baba. Hawa ndio Sizonje anawapenda

Sent From Kisana Kiki Iphone
 
Back
Top Bottom