GE2025 Mkuu wa Wilaya ya Ilala: Watanzania wenyewe wana hamu ya amani, hakuna Mtanzania mwenye hamu ya vurugu

GE2025 Mkuu wa Wilaya ya Ilala: Watanzania wenyewe wana hamu ya amani, hakuna Mtanzania mwenye hamu ya vurugu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam , amesema Watanzania kwa asili yao wana hamu ya kuishi kwa amani na siyo vurugu, akisisitiza kuwa baadhi ya kauli zinazohusiana na uvunjifu wa amani mara nyingi hazina mashiko.

“Watanzania wenyewe wana hamu ya amani, hakuna Mtanzania mwenye hamu ya vurugu. Hakuna mtu aliye tayari kwa ajili ya vurugu. Hizi ambazo tunaziona zinasemwa mara nyingi ni mtu tu unaweza ukaamua chumbani ukaandika unachokitaka wewe na unachokisikia,” amesema Mpogolo.

Amesisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayari kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na utulivu, na wananchi waendelee kujiandaa kushiriki bila hofu.

 
Ni kweli, Hakuna anaetaka vurugu, vurugu wanazileta wao viongozi kung'ang'ania madaraka hali watu hawawataki, wamechoka na vitimbi vyao
 
📌📌Madaraka ya kulevya🤣🤣🤣📌📌
 
Wanawafunika watanganyika na blanket la 'Amani', wao wanaiba na kugawana pesa na rasilimali za taifa.
Tumewashitukia!
 
Mpogolo ni mtu poa, ila vampire likikuuma lazima mfanane..
 
Back
Top Bottom