Mkuu wa Wilaya Ya Chato

Jun 7, 2013
63
7
Mkuu wa wilaya aingilia zoezi la upigaji kura baada ya kufika kituoni na kuamrisha msimamiz wa uchaguzi kuondoka kwa sababu alikuwa anazuia watu kupigia kura mtu zaidi ya mmoja na kumzuia mkuu huyo kuwapigia kura wafanya kazi wake wa shambani na ndani zaidi ya sita ambao baada ya msimamizi na mawakala kuwahoji watu wote sita walikiri kujua kusoma na kuandka na hivyo kumtaka mkuu wa wilaya Bwana Lodrick Mpogolo kutokuwapigia kura

Kuona hivyo mkuu wa wilaya huyo aling'aka na kutoa lugha za vitisho " mnanifahamu mimi ni nani hapa wilayani? Nitakumaliza kijana" , wakala alipokomaa mkuu huyo wa wilaya alitoa kitambulisho cha Ukuu wa wilaya na kisha kulazimisha kuwapigia kura watu wake na kumtoa msimamizi aliyekula kiapo na kulete msimamizi mwingine asiye na kiapo kuendelea na usimamizi wa kituo hicho katika kijiji cha Rubambangwe kitongoji cha mlimani ambapo ni nyumbani kwao Mh. Magufuli.

Naomba Mh. Hawa Ghasia ajue hili na aishauri mamlaka ya uteuzi wa mkuu huyu wa wilaya aidha kumsimamisha au kumpa onyo kali kwani kitendo alicho kifanya mkuu huyo wa wilaya si tu kilivuruga uchaguzi kituoni hapo bali pa kilikuwa kinakiuka kanuni na maadili ya utumishi wa umma na kitendo hiki kinamuondolea sifa mkuu huyo. Makamanda wenye mtandao vizuri iwekeni hewani kule FB na JF
 
Huyu atapromotiwa kwa kukitetea chama, Unaifahamu sababu ya mahita kupewa u- IGP na Mkapa?
 
...makabila ya wapi hayo!ukuu wa wilaya wa ushikaji,ukawa upumbavu kama huo pelekeni mahakamani haraka.
 
chato kumekucha, huwezi kuzuia mvua kunyesha, maeneo yote hali si nzuri kwa ccm, kuanzia Muganza, Kibehe, Chato mpaka Buseresere, na hata Katoro CDM na ukawa wamefanya vizuri
 
Ngoja nicheki na comrade Shigela Aloyce, nasikia alichafua hali ya hewa kijijini kwa magufuri hadi wakamtengenezea ajali ya gari!
 
.... Wanainchi Wa Huko Wamelala Sana, Angechezea Kichapo Tu. Kwani Shiling Ngapi?
 
hakika wananchi walimuogopa kwa sababu ya ukuu wake huyu jamaa kwa bada ya kuanza kutoa matkeo kuna mtendaj mmoja alitaka kuchakachua vijana wakazingira ofisi yote wakaanza kuishambulia kwa mawe
 
hakika wananchi walimuogopa kwa sababu ya ukuu wake huyu jamaa kwa bada ya kuanza kutoa matkeo kuna mtendaj mmoja alitaka kuchakachua vijana wakazingira ofisi yote wakaanza kuishambulia kwa mawe
Matokeo ya uchaguzi kitongoji / kijiji hicho yalikuwaje?
Magamba hayafai kabisa kwa kuvunja taratibu.
 
Back
Top Bottom