Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Katika muendelezo wa matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya wakuu wa wilaya nchini, mkuu wa Wilaya ya Njombe mama Msafiri amemuweka ndani mwenyekiti wataa wa Buguruni iliyo katika wilaya hiyo baada ya Mabishano yaliyotokea katika kikao.
Mabishano hayo yalitokea baada ya mwenyekiti wa mtaa kuhoji uhalali wa mkuu wa wilaya kushinikiza, Mwenyekiti huyo ang'olewe katika kiti hicho wakati bado kuna kesi mahakamani. Kuwekwa ndani kwa Mwenyekiti huyo kuliambatana na kunaswa kibao.
Siku hizi imekuwa hali ya kawaida ya Wakuu wa wilaya kutumia mabavu pale wanaposhindwa hoja.
Ni muhimi kwa Wizara yenye dhamana Na TAMISEMI ikawa makini na viongozi wa aina hii, wanaonea watu na wanasababisha hasira ya wananchi dhidi ya serikali yao. Hili tukio la mama msafiri lichunguzwe na hatua stahiki dhidi yake zichukuliwe.
Ibara ya Tisa ya katiba inakataza aina yoyote ya uonevu katika nchi hii, kwa hiyo ni matumaini yangu haki itatendeka!
Chini nimeambatanisha Sauti ya Majibizano yaliyopelekea Mwenyekiti huyo kuwekwa ndani!