Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

isupilo

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
303
1,254
Mara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.

Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happynes Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura

Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe

Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.
 
Utawala wa nchi za afrika siyo shida hiyo .happy piga kazi kisarawe wapate maendeleo
 
Isitoshe sio baba yake wa kumzaa shida iko wapi hapo?. Tatizo tunalolikataa wananchi ni kubeba mtu asiyebebeka...huyo dada anayo elimu nzuri tu...

Neno conflict of interest hutumiwa ktk mazingira kama haya!

Ni kama issue za tenders, huwezi kuipa tender kampuni yako, au kumfanyia interview mwanao!

Anyway Magufuli sio wa kwanza!

Nyerere alikuwa na ndugu Kibao ktk uongozi! Mkapa alikuwa na washkaji wa kutosha, the same kwa kikwete ambaye hata ndugu walikula position!

Si sawa Ila alichofanya is not uncommon!
 
Back
Top Bottom