Mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mwenyekiti wa mtaa aliyechaguliwa na wananchi sawa?

IRINGA MOJA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
503
229
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari Azam Tv na kuona habari ambayo inakichwa cha habari cha "Kibarua chaota nyasi kikaoni" ambako mkuu wa wilaya kamfukuza kazi mwenyekiti wa mtaa katika moja ya mitaa ya Dar katika kikao kilichokuwa na lengo la kutoa elimu ya mambo ya kodi kilichoratibiwa na TRA huku mkuu wa wilaya ya Ilala akiwa mgeni rasmi. Sababu ya kufukuzwa mwenyekiti huyo ni mkuu huyo wa wilaya kuhisi amezihakiwa na kufanyiwa utani katika majukumu yake ya kikazi na mwenyekiti huyo.

Kwa hali hii hivi inakuwaje mtu aliyechaguliwa na mamia U maelfu ya watu akafukuzwa kiholela hivo na mtu aliyeteuliwa kwa fadhila za mtu mmoja?
 
Tanzania nilikupenda sana ila inaonekana kuna watu walikuoenda zaidi

Pumzika kwa amani nchi yangu
 
Bashite kaacha kuwatisha na kuwafukuza kazi hadharani wateule wa wananchi. Sasa kazi hiyo inafanywa na Wakuu wa Wilaya...
 
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari Azam Tv na kuona habari ambayo inakichwa cha habari cha "Kibarua chaota nyasi kikaoni" ambako mkuu wa wilaya kamfukuza kazi mwenyekiti wa mtaa katika moja ya mitaa ya Dar katika kikao kilichokuwa na lengo la kutoa elimu ya mambo ya kodi kilichoratibiwa na TRA huku mkuu wa wilaya ya Ilala akiwa mgeni rasmi. Sababu ya kufukuzwa mwenyekiti huyo ni mkuu huyo wa wilaya kuhisi amezihakiwa na kufanyiwa utani katika majukumu yake ya kikazi na mwenyekiti huyo.

Kwa hali hii hivi inakuwaje mtu aliyechaguliwa na mamia U maelfu ya watu akafukuzwa kiholela hivo na mtu aliyeteuliwa kwa fadhila za mtu mmoja?

Mkuu hebu fafanua vizuri hapo, amefukuzwa kazi au ameondolewa kwenye hicho kikao? Maana kimamlaka mkuu wa wilaya hana uwezo wa kumfukuza kazi kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi kupitia tume ya uchaguzi.
 
Bashite kaacha kuwatisha na kuwafukuza kazi hadharani wateule wa wananchi. Sasa kazi hiyo inafanywa na Wakuu wa Wilaya...
Mbali ya busara ya mwenyekiti kuomba radhi hadharani, kilichoniuma zaidi ni umri wa mkuu wa wilaya na vile alivyokuwa anamfokea hadharani huyo mwenyekiti ambaye kiumri kamzidi
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa linaloikabili serikali ya awamu ya 5 kwa wateule wa Rais kuvimba kichwa na kuamini kuwa wao wapo juu kuliko wawakilishi wa wananchi ambao wameingia madarakani kwa kura za wananchi.

Kiburi chote wanapata kutoka kwa huyo huyo aliyewateua........

Refer speech ya Mkulu pale Ubungo alipomwambia RC wa Dar kuwa asisikilize maneno ya mtandaoni na badala yake achape kazi. jambo lililomwengezea kiburi mkuu huyo wa mkoa.........
 
Mkuu hebu fafanua vizuri hapo, amefukuzwa kazi au ameondolewa kwenye hicho kikao? Maana kimamlaka mkuu wa wilaya hana uwezo wa kumfukuza kazi kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi kupitia tume ya uchaguzi.
trifa inasema "kibarua chaota nyasi kikaoni". Mkuu kwa jinsi mambo yanavyoenda awamu hii yote yanawezekana
 
Mbali ya busara ya mwenyekiti kuomba radhi hadharani, kilichoniuma zaidi ni umri wa mkuu wa wilaya na vile alivyokuwa anamfokea hadharani huyo mwenyekiti ambaye kiumri kamzidi
Inauma sana! Hata hivyo Kiongozi huo atapata LAANA, kama aliyoipata Bosi wake Bashnet, aliyewadhalilisha Wazee hadharani...
 
Hili ni jipya sijui kama linawezekana ,kimsingi inawezekana kumutoa nje ya Kikao ila kumfukuza kazi inakigugumizi sana kama ni kwa kosa hilo sio zaidi haiwezekani ,wenye Mamlaka ya kumkataa Waliempigia kura ni Wapiga kura yaani Wananchi napo ziwepo sababu mhimu si kwa ushabiki tu wala chuki binafsi
 
Nakubaliana na hoja zako, kimsingi utaratibu ulioainisha ndio haswa unapaswa kufuatwa
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa linaloikabili serikali ya awamu ya 5 kwa wateule wa Rais kuvimba kichwa na kuamini kuwa wao wapo juu kuliko wawakilishi wa wananchi ambao wameingia madarakani kwa kura za wananchi.

Kiburi chote wanapata kutoka kwa huyo huyo aliyewateua........

Refer speech ya Mkulu pale Ubungo alipomwambia RC wa Dar kuwa asisikilize maneno ya mtandaoni na badala yake achape kazi. jambo lililomwengezea kiburi mkuu huyo wa mkoa.........
Kweli kabisa,Rais ndio chanzo cha hayataki yote,Ni wazi kabisa,anaupiga vita utawala bora wa sheria na haki.Tanzania inaelekea wapi??
 
Hili ni jipya sijui kama linawezekana ,kimsingi inawezekana kumutoa nje ya Kikao ila kumfukuza kazi inakigugumizi sana kama ni kwa kosa hilo sio zaidi haiwezekani ,wenye Mamlaka ya kumkataa Waliempigia kura ni Wapiga kura yaani Wananchi napo ziwepo sababu mhimu si kwa ushabiki tu wala chuki binafsi
Siamini hii stori mkuu wa wilaya gani asiyejua mipaka ya kazi yake kiasi hicho
 
Mkuu wa wilaya ya Ilala. Yule mzee ametia huruma kweli kweli alipokua anaomba msamaha
Halafu yule dada anamfokea balaaa(DC Sofia Mjema)
 
Hilo ndiyo tatizo kubwa linaloikabili serikali ya awamu ya 5 kwa wateule wa Rais kuvimba kichwa na kuamini kuwa wao wapo juu kuliko wawakilishi wa wananchi ambao wameingia madarakani kwa kura za wananchi.

Kiburi chote wanapata kutoka kwa huyo huyo aliyewateua........

Refer speech ya Mkulu pale Ubungo alipomwambia RC wa Dar kuwa asisikilize maneno ya mtandaoni na badala yake achape kazi. jambo lililomwengezea kiburi mkuu huyo wa mkoa.........
muache achape kazi RC bora kuwai kutokea tanzania huwezi kosa jina lake
 
Huyo dada amemfokea yule mzee hadi huruma,,,utadhani atakuwa D.C. maisha yake yote
 
Mkuu wa wilaya ya Ilala. Yule mzee ametia huruma kweli kweli alipokua anaomba msamaha
Halafu yule dada anamfokea balaaa(DC Sofia Mjema)
Aliyefanya hivyo ni DC wa ilala? Huyu ni DC mzoefu halafu ni kada wa ccm hivi kweli hajui mipaka ya serikali na chama cha siasa? Huyo mwenyekiti wa chama gani?
 
Back
Top Bottom