Mkuu wa Wilaya awazuia wananchi kuingia kwenye shamba la mgodi alioruhusu Rais Magufuli

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058

Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ameweka askari kuwazuia wananchi kuingia kwenye shamba la muwekezaji kuchimba dhahabu ambalo Rais Magufuli aliwaruhusu
Muwakilishi wa muwekezaji huyo ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi amesema shamba hilo analimiliki kisheria hivyo hawezi kuwapa wananchi
 
Hawa ndio unakuta walishakula pesa ya mwekezaji......

Yaani nashangaa eti wapiga dili , wapiga dili ndio hawa sasa wanaohujumu wananchi.....

Huyu atakuwa wa pili baada ya Gondwe kuwazuia wananchi na police kuingia mgodini......

Awamu hii nguvu ya pesa vs Matamko ya kukurupuka tutaona mengi sana .......
 
ngoja tuone
 
ngoja tuone
Kiongozi yeyote wa serikali iliyoko madarakani anayepingana na maagizo halali ya Raisi(mkuu wa serikali) ajue kabisa anavunja Katiba ya nchi Ibara ya 35 na sheria za Ajira ya Utumishi wa Umma. Hiyvo, anatakiwa yeye mwenyewe ajihuzuru au asubiri kutumbuliwa. Nilitoa mtazamo huu wa kisheria juu ya kauli ya Mafuru, watu walinipinga kimihemuko bila kuzingatia matakwa ya Katiba ya nchi na Sheria za Ajira ya Utumishi wa Umma. Kama taarifa hii ni ya kweli, huyo DC anatakiwa ajihuzuru au atumbuliwe.Hii ni kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hii.
 
Mkuu hiyo nimeipenda
 
Tyranny to Anarchy. .Sheria weka pembeni alafu tuinyoshe nchi ..Sasa mwisho itakua futa sheria kila mtu afanye anavyojua Mh. Rais kua makini la sivyo utaliangamiza ili basi
 
Kiongozi yeyote wa serikali iliyoko madarakani anayepingana na maagizo halali ya Raisi(mkuu wa serikali) ajue kabisa anavunja Katiba ya nchi Ibara ya 35 na sheria za Ajira ya Utumishi wa Umma. Hiyvo, anatakiwa yeye mwenyewe ajihuzuru au asubiri kutumbuliwa. Nilitoa mtazamo huu wa kisheria juu ya kauli ya Mafuru, watu walinipinga kimihemuko bila kuzingatia matakwa ya Katiba ya nchi na Sheria za Ajira ya Utumishi wa Umma. Kama taarifa hii ni ya kweli, huyo DC anatakiwa ajihuzuru au atumbuliwe.Hii ni kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hii.
vipi ikiwa hayo maagizo yanakiuka katiba?
 
Hilo swali zuri sana......

Amri inakuwa halali iwapo tu inakuwa imetolewa kwa kuzingatia sheria za nchi.

Kama Mkuu mwenyewe anatamka hadharani kuwa anaiweka pembeni Katiba ya nchi, kwa kuwa priority namba 1 kwake ni kuinyoosha nchi, ni dhahiri kuwa matamko yake mengi nayo yatakuwa batili........
 
Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ameweka askari kuwazuia wananchi kuingia kwenye shamba la muwekezaji kuchimba dhahabu ambalo Rais Magufuli aliwaruhusu
Muwakilishi wa muwekezaji huyo ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi amesema shamba hilo analimiliki kisheria hivyo hawezi kuwapa wananchi

Naona maafande kama wanaogopa vile
 
Mwekezaji gani tokea 1990 hajaendeleza uchimbaji.. amehodhi tu maeneo, huyo sio mwekezaji, leseni yake ifutwe haraka na eneo wapewe wananchi maskini..

Leseni yake inafutwa mara moja tu, from 1990 hajaendeleza hadi leo..? hapo unapoona kijiko hicho ni kuzuga tu sbb ameona wananchi na ITV wamefika ktk eneo hilo, hicho kijiko Caterpillar wameleta hapo kuzuga na kuonyesha wako busy, kumbe hakuna lolote..

Maeneo kama haya ni mengi na hayaendelezwi, dawa ni kufuta leseni na kuwapa watu wenye uwezo na nia ya kuchimba madini..
 
Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ameweka askari kuwazuia wananchi kuingia kwenye shamba la muwekezaji kuchimba dhahabu ambalo Rais Magufuli aliwaruhusu
Muwakilishi wa muwekezaji huyo ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi amesema shamba hilo analimiliki kisheria hivyo hawezi kuwapa wananchi

Ninacho kiona hapa ni watu kumnukuu vibaya mh rais na kutumia nukuu hiyo kunyang'anya haki halali kabisa za wengine, mgodi alio uongelea mh rais ni mgodi uliopo shinyanga/simiyu kama sijakosea na sio huu wa misungwi ,kila mgodi una historia yake , maana kama ndio hivyo hao wananchi wavamie na KIWILA,ACACIA,GEITA GGM,TULAWAKA.NK maana hata hao wawekezaji walio wekeza huko hawakukuta pori tupu walikuta wananchi wakiwemo tayari .kuweni makini na siasa uchwara hazijengi bali zina bomoa.
 
lkn kwa huu mgodi ni sahihi. tokea 1990 mwekezaj hayupo yaan miaka 26. hii sio halali. huenda hawa ndo wapiga dili tunaowasema
 
Mwekezaji gani tokea 1990 hajaendeleza uchimbaji.. amehodhi tu maeneo, huyo sio mwekezaji, leseni yake ifutwe haraka na eneo wapewe wananchi maskini..

Leseni yake inafutwa mara moja tu, from 1990 hajaendeleza hadi leo..? hapo unapoona kijiko hicho ni kuzuga tu sbb ameona wananchi na ITV wamefika ktk eneo hilo, hicho kijiko Caterpillar wameleta hapo kuzuga na kuonyesha wako busy, kumbe hakuna lolote..

Maeneo kama haya ni mengi na hayaendelezwi, dawa ni kufuta leseni na kuwapa watu wenye uwezo na nia ya kuchimba madini..

Ishikokela. Watu wameumizwa na kudhulumika kisa dalali wa kibongo anayetamfuta.mwekezaji.

Wapewe wananchi
 
Ninacho kiona hapa ni watu kumnukuu vibaya mh rais na kutumia nukuu hiyo kunyang'anya haki halali kabisa za wengine, mgodi alio uongelea mh rais ni mgodi uliopo shinyanga/simiyu kama sijakosea na sio huu wa misungwi ,kila mgodi una historia yake , maana kama ndio hivyo hao wananchi wavamie na KIWILA,ACACIA,GEITA GGM,TULAWAKA.NK maana hata hao wawekezaji walio wekeza huko hawakukuta pori tupu walikuta wananchi wakiwemo tayari .kuweni makini na siasa uchwara hazijengi bali zina bomoa.
Nimekuelewa mkuu. Safi.
 
Hawa ndio unakuta walishakula pesa ya mwekezaji......

Yaani nashangaa eti wapiga dili , wapiga dili ndio hawa sasa wanaohujumu wananchi.....

Huyu atakuwa wa pili baada ya Gondwe kuwazuia wananchi na police kuingia mgodini......

Awamu hii nguvu ya pesa vs Matamko ya kukurupuka tutaona mengi sana .......
sheria Ina nguvu kuliko matamko
 
hawa maafande wa ruvu jkt veeepe??? kocha akipuliza kipyenga wanamwelewa, akipiga refa naye wanamwelewa kweli hii timu itashuka daraja mwaka huu.
Magu kasema wananchi wasibughuziwe jamaa wakafyata mkia japo hawana kama kara jeremiah, leo cd kasema kamata wamechezesha mikia.
 
Back
Top Bottom