Mkuu wa wilaya avunja uongozi wa club ya Stand United

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
346
Jana mkuu wa wilaya ya Shinyanga mjini amevunja kile alichokiita ni uongozi wa club ya stand united, mkuu huyo wa wilaya alichukua uamuzi huo mara baada ya kuitisha kile yeye alichokiita mkutano wa wanachama na wadau wa club ya stand united.

Maamuzi hayo yalifuatia kutokea kwa malalamiko mengi ya wanachama wa club ya stand katika ofisi yake kua tim hiyo imeuzwa, pamoja na madai mengine mengi. Mkuu huyo wa wilaya alichukua uamuzi wa kuitisha mkutano ili kulitafutia ufumbuzi swala hilo, na ndipo majawabu yakaja kua nikuvunja uongozi uliopo pamoja na kuunda kamati yampito itakayo ratibu mchakato mzima wa kupata uongozi mwingine.

Swali la kujiuliza,,! Mkuu wa wilaya kapata wapi mamlaka ya kisheria kuvunja uongozi wa tim??

Pili hao aliowaita yeye kua wanachama wa stand waliompelekea malalamiko kawathibitisha vipi kua ni wanachama halali wa stand united?
Mimi nadhani ipo haja kwa watawala wetu watambue mipaka ya majukumu yao, pamoja na hekima juu ya utatuzi wa migogoro katika jamii wanazosimamia.

Zipo mamlaka zinazosimamia maswala ya soka, amabazo ni FIFA, CAF na TFF.

Mkuu wa wilaya hana mamlaka ya kutatua mgogoro wowote unaohusu soka hana kabisa, tukumbuke Ndolanga aliwahi kutolewa na serikali lakini kilichofuata ni nchi yetu kuenguliwa katika uanachama wa FIFA, sasa huyu mkuu wa wilaya minazani kapotoshwa, mpaka kufikia hatua ya kutangaza kuvunja uongozi tena uliopo kihalali.

Naomba mamlaka husika zilikemee vikali swala hili, kwani linaweza kuleta balaa katika soka letu si Shinyanga tu hata sehemu yeyote katika nchi yetu, sijawahi kuona mgogoro utokee simba au yanga, halafu mkuu wa mkoa au wailaya aingilie kati, iweje leo Shinyanga kuna nini naomba kuwasilisha.
 
Ungeweka na historia ya timu, ukaweka pia namna viongozi wanavyotuhumiwa kuuza timu na majibu yao, ukaenda mbali zaidi kutueleza hao walioenda kwa mkuu wa wilaya kwa kawaida na taratibu wanatakiwa waanzie wapi na hapo wanapoanzia mamlaka yao yakoje. Hii ni taarifa ya juu juu mno mkuu tayari umeshaanza kumlaumu mkuu wa wilaya. Mi nachoona mkuu wa wilaya kachukua tafadhali pengine kuna dalili za uvunjifu wa amani clubuni hapo
 
Ungeweka na historia ya timu, ukaweka pia namna viongozi wanavyotuhumiwa kuuza timu na majibu yao, ukaenda mbali zaidi kutueleza hao walioenda kwa mkuu wa wilaya kwa kawaida na taratibu wanatakiwa waanzie wapi na hapo wanapoanzia mamlaka yao yakoje. Hii ni taarifa ya juu juu mno mkuu tayari umeshaanza kumlaumu mkuu wa wilaya. Mi nachoona mkuu wa wilaya kachukua tafadhali pengine kuna dalili za uvunjifu wa amani clubuni hapo
mkuu, uongozi wa club ya stand united upo kihalali chini ya katiba yao, madai ya mkuu wa wilaya kua kapelekewa malalamiko juu ya kuuzwa kwa tim hiyo hayana ukweli, stand united inawanachama wasiozidi sabini walio hai, na inamisimu miwili katika ligi kuu, sasa wamefika sehemu wamebadili katiba yao nakuamua kua kampuni na sitimu ya wanachama, na walifuata taratibu zote za soka ikiwa nipamoja nakuzitaarifu mamlaka zinazohusika na soka, na zikabariki, lakini leo watu wachache wamekwenda kumdanganya yule mama kua tuna mgogoro, tim imeuzwa sasa sijui imeuzwa wapi, cha zaidi hapo tim hiyo ilianzishwa na wapiga debe wa pale stand, sasa leo walopeleka malalamiko hata hawajawahi hata kukatisha tiketi pale stand nihayo tu.
 
Basi kama ni ya kweli hayo mama anajipanga kiaina si unajua tena mambo ya mjengoni. Cha msingi toeni taarifa katika mamlaka zilizobariki hiyo michakato yenu ya kuwa kampuni ikiwa ni pamoja na Chama cha soka wilaya, mkoa, na taifa. Kama hampati majibu yanayoeleweka sheria zipo fungueni kesi mtandewa haki.
 
Wakati wa kikao na mkuu wa (w) mngemweleza taratibu namna sahihi ya ufumbuzi wa mgogoro na kuwa vyombo vinavyoshughulikia soka viwepo pale yeye awe kama mwalikwa na mshauri, maana kuna sheria za michezo na katiba zake ambazo pengine zimekiukwa au hazijafuatwa
 
Tatizo wakuu wa wilaya hawana kazi ya kufanya ndio maana wanakuwa hivyo.
 
Ungeweka na historia ya timu, ukaweka pia namna viongozi wanavyotuhumiwa kuuza timu na majibu yao, ukaenda mbali zaidi kutueleza hao walioenda kwa mkuu wa wilaya kwa kawaida na taratibu wanatakiwa waanzie wapi na hapo wanapoanzia mamlaka yao yakoje. Hii ni taarifa ya juu juu mno mkuu tayari umeshaanza kumlaumu mkuu wa wilaya. Mi nachoona mkuu wa wilaya kachukua tafadhali pengine kuna dalili za uvunjifu wa amani clubuni hapo[/QUOTE
Wanagombea hela za ufadhili hapo, nasikia Stand United wana ufadhili mnono
 
Kama kweli MKUU wa wilaya amevunja uongoz uliopo basi haya ni moja ya maajabu ya dunia
Yule mama nazani hajui majukumu yake ni yapi.
leo tupo Mwanza kukamilisha ligi kwa kucheza na toto afrika cha ajabu kaleta watu wake ili wasimamie mapato, lakinisimamizi wakituo kagoma kuatambua na akasema hayo yalofanyika Shinyanga hayatambui, anachotambua ni uongozi wa siku zote
 
Mwenye CV ya huyo mama atuwekee hapa...itasaidia kutambua ni kwanini anafanya hayo maamuzi ya kifedhuli.
 
Back
Top Bottom