Mkuu wa Wilaya Arusha tuondolee hawa Wezi

kijenge

Senior Member
Mar 9, 2012
179
164
Serikali ya mtaa Kijenge kusini inayoundwa na CCM imeanzisha sungu sungu na kuchukua hela ya ulinzi, Matokeo yake maduka manne yamevunjwa na watu wanakabwa na kuporwa simu na hela Wakati wa uongozi wa CHADEMA hapakuwa na sungu sungu na hakuna mtu aliye wahi ibiwa.

Tunaomba mkuu wa Wilaya aje tumweleze kero yetu kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
 
Hiyo ni kweli kabisa kuna jamaa kavunjiwa kaibiwa computer na monitor na camera njia ya kuingia ziga,wamevunja kwa mama ngijo na maduka mawili eneo la msikitini Ccm hoyeee.Inajirudia enzi za Nkya akiwa mwenyekiti yeye na genge lake.
 
Nikweli Uizii na vibaka haukuwepo tangu sungusungu imeanza imekuwa shida.Nahili genge enzi za Nkya akiwa mwenyekiti ndio lilisababisha Ccm kuchukiwa wanaiba wao wanakamata vijana wanaotoka Mirerani na hela zao, wanawasingizia wezi ili wahongwe.
 
Nadhani hili tatizo (sungusungu) Limeanzishwa nchi nzima. Masaki-Dar es salaam hakukua na sungusungu lakini siku za hivi karibuni serikali ya mtaa imeanzisha kikundi cha sungusungu ambao hawaonekani lakini S/mtaa wanatoza malipo kwa kila nyumba na kiwango cha chini ni 50,000 na cha juu ni 150,000.
 
Huyo dc ni msikivu saaana! naamin kama taarifa hiz zitamfikia basi atalitatua kwa wakati!
 
Sio mpka uibiwe ndio useme alioibiwa ni jamaa yangu wa karibu amefungua sehemu ya kurekodi hajamaliza hata wiki wamempora,na Amelipa hela ya sungusungu.Walivunja kwake na kwa jirani yake.

Shida ni kuokota vijana wasio waadilifu au vijana ambao ni vibaka na kuwapa hiyo kazi....

Upo mtaa huku ninapo ishi walianzisha Sungusungu matokeo yake Nguo zilizokuwa zimeanikwa usiku walikuwa wanaiba, wizi wa vitu uliongezeka na wale waliokuwa wanatoka disko usiku walikuwa wanachapwa viboko, wangine wanaombwa rushwa na wengine walikuwa wanalazimishwa na wao kusaidia kulinda usiku Hadi asubuhi kwa lazima...
 
Kwa hiyo Vijana wa Lema wameanza kazi boss wao akiwa Nairobi. Kazi itaonekana
 
Back
Top Bottom