Kauli za kupishana kwa jambo moja lililopo eneo moja la kazi ni mzigo kwa taifa. Hili limewezekana hapa Dar juzi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni aliwaambia walimu wasiotosheka na mshahara waondoke waende unakotosha. Pia akawaagiza walimu wasiwafungie wanafunzi waliochelewa mageti. Jana mkuu wa mkoa kawatahadharisha wanafunzi kutoitumia fursa ya elimu bure vibaya.
Huu ni mpishano wa kauli. Mkuu wa mkoa anahamasisha na mkuu wa wilaya anawatisha watoa elimu na kuwatetea wanafunzi wazembe na wavivu.
Naamini, kwa mpishano huu wa kauli Dar itaangukia pua kitaaluma mwaka huu.
Walimu hii siyo mara yao ya kwanza kuisikia kauli hii kwani iliwahi tolewa na Mwamtumu Mahiza akiwa naibu waziri wa elimu na mwisho wa siku kapotezwa kwenye medani za siasa. Sasa sijui na huyu anayewatisha walimu eti wapishe ilihali wana haki za msingi kudai mshahara unaotosha sijui kajipangaje kukabiliana na walimu pindi wakiamsha hisia zao.