Mkuu wa wilaya amuunga mkono kamanda G Lema

Mkuu wa wilaya amuunga mkono kamanda G Lema

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
25,975
Reaction score
25,289
MKUU wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, ametangaza kuifungua Shule ya Sekondari Korona iliyopo Njiro kwa Msolwa ambayo juzi ilifungwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi likiwamo tatizo la usafiri na ukosefu wa miundombinu.

Pamoja na uamuazi huo, mkuu huyo wa wilaya jana alitangaza kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo, John Mbise, ambaye hakuwapo shuleni hapo licha ya kupewa taarifa za ugeni huo.

Aidha, amemuagiza Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji, Violet Kiwowoza, hadi jana majira ya saa sita awe amewasilisha barua ya kutenguliwa cheo kwa mkuu huyo wa shule ofisini kwake na awe amebandika matokeo ya kidato cha pili shuleni hapo.

Pia amemuagiza mkurugenzi kuwasilisha mchanganuo wa shule hiyo kuwa ya bweni. Alisema ameifungua shule hiyo kwa kuwa Lema hakufuata taratibu za kuifunga, lakini alikiri kuwa shule hiyo ina matatizo mengi ambayo alisema kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na uzembe wa watendaji na viongozi wa Idara ya Elimu.

“Tusiigeuze hoja hii kama ni matatizo ya mbunge na kuleta siasa, lakini ni wajibu kuwajibishana watendaji kutokana na uzembe, hata maji yamekatwa eti kwa kushindwa kulipa bili ya sh 300,000. Hii ni aibu kwa jiji, wakaguzi wa elimu siku zote walikuwa wapi hadi haya yote yanatokea?’’ alihoji Mongela.

Mongela aliwatahadharisha watendaji wa serikali kuwa wasishangae siku za usoni kumuona akiungana na Mbunge Lema katika kushinikiza baadhi ya mambo kufanyika kwa ufanisi kama inavyohitajika.

“Mimi nadhani japo wengine wanachukia Lema kushinda kesi yake, lakini nadhani Mungu ndiye alipanga hivyo, ili aje kufichua mambo haya, kwani sisi japo tungeyabaini lakini ingechukua muda mwingi,’’ alisema Mongela.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake baada ya uamuzi wa mkuu wa wilaya, Mbunge Lema alisema yeye kama mbunge alikuwa anatambua kuwa sheria hazimruhusu kufanya hivyo, lakini kama mtetezi wa wananchi wa Arusha alilazimika kuchukua uamuzi huo ili kuwasaidia wanafunzi ambao kwa wiki tatu sasa hawapati masomo na wana shida ya usafiri na matatizo ya maji.

Source: Tanzania Daima

note :Ukiishi nyumba moja na makamanda na wewe ni kamanda

cc : Kiranja Mkuu
 
John Mongella (DC), ni mmoja kati ya viongozi vijana wachache wenye "AKILI" ndani ya ccm!!! yuko tofauti sana na kina........
 
MKUU wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, ametangaza kuifungua Shule ya Sekondari Korona iliyopo Njiro kwa Msolwa ambayo juzi ilifungwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi likiwamo tatizo la usafiri na ukosefu wa miundombinu.

Pamoja na uamuazi huo, mkuu huyo wa wilaya jana alitangaza kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo, John Mbise, ambaye hakuwapo shuleni hapo licha ya kupewa taarifa za ugeni huo.

Aidha, amemuagiza Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji, Violet Kiwowoza, hadi jana majira ya saa sita awe amewasilisha barua ya kutenguliwa cheo kwa mkuu huyo wa shule ofisini kwake na awe amebandika matokeo ya kidato cha pili shuleni hapo.
Wakuu shule hiyo ipo kama kilometa mbili kutoka Njiro Kwa Msola, haipo kwa Msola, kadhalika ofisa elimu anaitwa Mlowasa. Siyo kama hapo penye red.
Wazo langu. Ni muhimu sasa halmashauri ya jiji ije na mpango wa kuzipatia mabasi shule za pembezoni maana wanafunzi wanateseka sana. Ama basi watoto hawa wapangiwe shule zilizopo kwenye kata zao.
 
Gamba watamuundia zengwe.
kafanya vema dc huyo wa arusha ni tofauti na ma dc wengine. Njoo iramba umwone dc anavyoserebuka na bia tu mara misigiri mara kwa mrembo wake yule mwalimu. Basi vurugu tu shule ya lulumba imegeuka danguro yeye yupo tu
 
Naungana na wengine kumpongeza mtoto wa mama mongela na Kamanda Lema.
 
Mkuu wa wailaya ana uwezo wa kufukuza walimu , hii nimeijua leo
 
Sasa amefungua hiyo shule ili kinanani wakasome?kama shule inatakiwa iwe na wanafunz 1500 au 2000. Yenyewe inawanafunz hata robo ya robo hawafiki. Hiyo shule suluhu ni boding tu.wao wanazunguka zunguka ila ukweli wana ujua hawataki kumpa lema ushind wake wanahisi watakua wamempaisha sana lakini mnyonge mnyongeni hakiyake mumpe ee!
 
John Mongella (DC), ni mmoja kati ya viongozi vijana wachache wenye "AKILI" ndani ya ccm!!! yuko tofauti sana na kina........

Jf ni mahali tunapoweza kuongea/kujadili kwa uhuru, bila kificho, hapa hapendwi mtu, hachukiwi mtu! Kwa wale wanaoponda au kupondwa Jf wajiangalie upya!

Viva Jf!!!!!!
 
Mongela aliwatahadharisha watendaji wa serikali kuwa wasishangae siku za usoni kumuona akiungana na Mbunge Lema katika kushinikiza baadhi ya mambo kufanyika kwa ufanisi kama inavyohitajika.
WAMEJUA KUWA WANANCHI WAMEYACHOKA MAOVU YAO.

kafanya vema dc huyo wa arusha ni tofauti na ma dc wengine. Njoo iramba umwone dc anavyoserebuka na bia tu mara misigiri mara kwa mrembo wake yule mwalimu. Basi vurugu tu shule ya lulumba imegeuka danguro yeye yupo tu

Kwani tabia za aliyemteua kuwa DC zikoje? "Ndege wa manyoya yanayofanana huruka pamoja"
 
Total Confusion!! Hebu soma gazeti la habari leo! Sijui kati ya haya magazeti mawili ni lipi limeandika ukweli.
http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8589-dc-atengua-amri-ya-mbunge-lema
Kama kweli mkuu wa wilaya katengua maamuzi ya Lema, basi ni dhahiri Lema alikurupuka. Hakufuata taratibu, au hakujua taratibu zilivyo. Jana niliweka post hii hapa kwenye thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanafunzi-kuendelea-kusoma-korona-sec-7.html:
Sijui kama kiprotoko mbunge anayo amri ya kufunga shule. Lets see what will happen, lakini sidhani kama mbunge ana mamlaka ya kufunga shule. Itachekesha pale mkuu wa wilaya atakapokuja kuamrisha watoto waendelee na masomo hapohapo.
Lema anatakiwa kujifunza mifumo ya kiutawala ili asifanye maamuzi ambayo mwisho wa siku yatamdharirisha.
 
Safi sana DC na safi kabisa kwa Kamanda Lema.
 
Mambo mengine hayahitaji siasa wala protokali.ni kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka hayo mengine yafuate.kaza buti kamanda lema hapo ndo kwaanza safari inaanza tunasubiri kwa hamu mambo mengi mazito bungeni,,.,
 
kafanya vema dc huyo wa arusha ni tofauti na ma dc wengine. Njoo iramba umwone dc anavyoserebuka na bia tu mara misigiri mara kwa mrembo wake yule mwalimu. Basi vurugu tu shule ya lulumba imegeuka danguro yeye yupo tu

kaka huyo bwana sijamfahamu vema,ana mrembo wake wapi vile,mana mie mrembo wangu simuelewi sku hz kaka,mara trip za huku na kule.
 
Total Confusion!! Hebu soma gazeti la habari leo! Sijui kati ya haya magazeti mawili ni lipi limeandika ukweli.
http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8589-dc-atengua-amri-ya-mbunge-lema
Kama kweli mkuu wa wilaya katengua maamuzi ya Lema, basi ni dhahiri Lema alikurupuka. Hakufuata taratibu, au hakujua taratibu zilivyo. Jana niliweka post hii hapa kwenye thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wanafunzi-kuendelea-kusoma-korona-sec-7.html:

Lema anatakiwa kujifunza mifumo ya kiutawala ili asifanye maamuzi ambayo mwisho wa siku yatamdharirisha.

Kwahiyo wewe umeliamini gazeti lipi?
Habari leo au Tanzania daima?
 
Back
Top Bottom