Mkuu wa mkoa, wilaya wamkimbia Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa mkoa, wilaya wamkimbia Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Dec 12, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]


  na Grace Macha, Hai  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Norman Sigalla, juzi walimkimbia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, katika shughuli za upandaji miti na uzinduzi wa usafi wa mji mdogo wa Bomang'ombe yaliko makao makuu ya wilaya, ikiwa ni sehemu ya sherehe za jubilee ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Mbowe.


  Viongozi hao wakuu wa serikali, awali walikubali na kuthibitisha kushiriki tukio hilo la kimaendeleo juzi, lakini wote wakatoweka muda mfupi kabla ya kuanza kwa shughuli za upandaji miti na usafi.
  Tukio hilo lililoonekana kuwasononesha wananchi wengi waliojitokeza katika shughuli hizo, lilimsikitisha Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai (CHADEMA), aliyewataka viongozi na watendaji wa serikali nchini kuacha kuchanganya shughuli za maendeleo ya wananchi na masuala ya siasa na waelewe kuwa nafasi hizo wamepewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.


  Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema kuwa suala la utunzaji wa mazingira halina itikadi kwani linawanufaisha wananchi wote, hivyo inashangaza kwa viongozi hao kukwepa kushiriki.
  Mbowe aliandaa na kuratibu zoezi hilo linalogharimu sh milioni 300, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwake, jumla ya miti 10,000 ilipandwa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Bomang'ombe pamoja na kugawa vifaa vya usafi na trekta lenye tela kwa ajili ya kukusanyia taka.

  "Nadhani huu ni mkakati wa makusudi kujaribu kunidhoofisha, wanafikiri wakishiriki watanijenga kisiasa au wanahisi wataniongezea umaarufu, jambo ambalo si sahihi kwani Mbowe kama ni umaarufu ninao wa kutosha wala siwezi kuwategemea wao wanijenge," alisema Mbowe.

  Hata hivyo, mbunge huyo alielezea kupata faraja kutokana na mwitikio wa wananchi waliojitokeza kushiriki kupanda miti na kusafisha mji na kuongeza kuwa anaamini malengo ya kuufanya mji wa Bomang'ombe kuwa safi yatafanikiwa huku akiahidi kukabiliana na yeyote atakayejaribu kurejesha nyuma harakati hizo.

  Akihojiwa na Tanzania Daima juu ya hatua yake ya kutoonekana katika shughuli hizo dakika za mwisho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Gama, alikiri kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo lakini alishindwa kuhudhuria baada ya kupata maelezo ya kitaifa yakimtaka akapokee Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukishuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro ulikopandishwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.

  Alisema kuwa kutokana na nia njema aliyokuwa nayo, baada ya kupata udhuru huo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Sigalla, akamwakilishe kwenye hafla hiyo lakini naye alishindwa baada ya muda mfupi kabla ya kuanza kwa shughuli hizo juzi asubuhi kuitwa mjini Dodoma.

  Juhudi za kumpata Sigalla kupitia simu yake ya kiganjani kujua, ikiwa baada ya kupata udhuru alimwagiza kiongozi mwingine akamwakilishe ziligonga mwamba baada ya simu hiyo kuita muda mrefu bila kupokewa.

  Zoezi hilo la kupanda miti na kufanya usafi kwenye dampo la Green Belt liliwashirikisha wananchi wa Wilaya ya Hai, wabunge 15 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasei na Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafar Michael, pamoja na baadhi ya madiwani kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

  Aidha, Mbowe aliongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Lambo uliopo Kijiji cha Nshara ambapo jumla ya sh milioni 30 zilipatikana katika hafla hiyo iliyotanguliwa na ibada iliyoongozwa na Sheikh Yusuf Lyasenga, ambapo mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Bakwata mkoani Kilimanjaro, Sheikh Rashid Mallya.

  Mbunge huyo wa Hai kwa vipindi viwili tofauti alichangia sh milioni tano, wakati kada maarufu wa CCM , Mustafa Sabodo, ambaye hakuweza kushiriki shughuli hiyo kwa maelezo kuwa yuko India kwa matibabu alichangia sh milioni tano. Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alichangia sh milioni 4.5 ikiwa ni gharama ya mazulia.

  Wengine waliochangia ni mbunge wa viti maalumu, Leticia Nyerere sh milioni moja, huku wabunge wengine kwa pamoja wakichangia sh milioni tano na kaka wa mbunge huyo wa Hai, Twalib Mbowe, akichangia sh milioni tano.

  Mbowe alizindua ofisi ya Taasisi ya Kusimamia Mpango wa Maendeleo ya Wilaya ya Hai ( HAKIDI) ambapo kupitia taasisi hiyo anatarajia kutengeneza ajira zaidi ya 5,000 katika kipindi cha miaka mitano kwenye sekta ya utalii na kilimo.

  Source Tanzania Daima.

  Alisema kuwa tayari HAKIDI imekwisha kutoa mafunzo kwa vijana 450 kwenye sekta ya utalii, ambao walipewa ujuzi katika upandishaji wageni Mlima Kilimanjaro na tayari 200 wamekwisha kupata ajira kwenye makampuni mbalimbali ya uwakala wa utalii.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


   
 2. S

  Seacliff Senior Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Watanzania wengi wako tayari kushiriki kwenye shughuli ambazo zinawaletea maendeleo kwenye maeneo yao, matatizo makubwa ni kwamba baadhi ya viongozi wetu wanashindwa kutofautisha siasa na wajibu wao kwa raia.

  Mheshimiwa Mbowe anatuonyesha mfano wa kuigwa na kama wabunge wengine wa vyama vyote wangeiga hili, nchi yetu ingefika mbali.

  Hongera Mheshimiwa Mbowe na tunakusihi usife moyo kwa yanayofanywa na hawa cowards wachache, wenye lengo la kujaza matumbo yao badala ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
   
 3. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hawa viongozi wa chama tawala ni wajinga kweli walipewa madaraka kwa kutumia kanuni zipi? yaani wao kushiriki na mbunge wa jimbo tayari wamekuwa CHEDEMA? Hawa sio viongozi wa wananchi isipokuwa wako pale kutetea ulaji hili jambo limenishangaza sana
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Watanzania watazidi kuipa credits CDM, si kwasababu ni wapinzani tuu, bali kwa sababu jamaa wanatenda zaidi ya kuzungumza, pale CCM zaidi ya Filikunjombe sijamwona mwingine mwenye nia ya dhati ya kusaidia wapiga kura wake
   
 5. m

  massai JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza wananchi wa HAI kwa muitikio wao katika kuleta maendeleo,agamba akili hiyo hawana labda majungu na wizi ndio utaona wamejazana mpaka nafasi hakuna tena.ingekua ni masuala ya kusaini mkataba flani wenye mabilioni wasingekosa alakini kuhusu majukumu yakuleta maendeleo kusaidia jamii wala hawawezi kuja,uhuru uliletwa na watu sio mwenge waache kutuletea us.......nge wao.inaudhi sana.
   
 6. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba hawawezi kushiriki kwenye shughuri za maendeleo,wao maendeleo yao ni ya mdomoni tu kutoa ahadi lukuki utekelezaji 0 basi hiyo ndio kazi waliobakiza.
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sigalla ni Mkinga ingetangazwa posho mapema angetokea
   
 8. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jaman nchi hii ni ya visa...acha hao viongoz watunze ajira zao...wakionekana tu kesho ajira kwa heri
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  shughuli zozozte zilizoandaliwa na serikali au ccm huwa zina posho.
  mbowe aliandaa sh ngapi kama posho?
  ccm mkono mtupu haulambwi.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kwikwikwikwi labda wameogopa kibarua kitaota nyasi
   
Loading...