Habari za kusikitisha ni kwamba katika kipindi cha mwezi mmoja kumetokea matukio ya UJAMBAZI mawili na kusababisha maafa na majeruhi ya watu 9 katika mkoa wa Tanga.
Jana usiku wa tarehe 20/04. kumetokea tukio la kijambazi mjini Tanga katika bakery ya Central iliyokuwepo Tanga Mjini.
Majambazi waliingia ndani ya bakery na kuwalaza watu wote chini. Walidai pesa na kupewa shillingi millioni 2. Baada ya kupata pesa hizo wakaamua kuwapiga risasi watu waliolala chini kwa kuchagua yupi wamuue.
Watu wa 4 walifariki dunia hapohapo. Wawili wakiwa wafanyakazi na 2 wanunuzi wa mikate.
Jambo la kusikitisha ni kwamba tukio kama hili lilitokea petrol station mwezi mmoja nyuma na kuwapiga mapanga wafanyakazi wote.
Huku polisi wakiwa busy kushughulikia watu wanaosafirisha mirungi na sukari za magendo, mji wa Tanga umekua hauna usalama.
Imefika wakati wananchi wengi kuomba vibali vya bastola. Jee mkuu wa mkoa anafanya nini?
Magufuli atumbue jipu ikiwa wananchi wa Tanga wanauliwa bila ya hatia.
Isiwe kukusanya kodi wakati matukio ya ujambazi kwenye mkoa uliokua kimya unanyima wananchi usalama.
Wengi wanasema, majeshi na mapolisi wanashirikiana na majambazi, je kwanini hawa wanaofanya vitendo hivi hawakamatwi?
Hakika tukio la jana limewakera wananchi wengi sana. Haijawahi kutokea kuuliwa watu 4 katika tukio la kijambazi.