tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,115
Kauli iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma, juu ya kusubiri maandalizi ya siku 14 kwa wizara mbalimbali kutohamia huko hadi akamilishe maandalizi kadhaa imeniacha na sintofahamu. Akiongelea swala hilo mkuu huyo wa mkoa licha ya kuwaambia watu wa serikalini juu ya maandalizi hayo yatakayo chukua siku 14 ndipo waanze kuhamia Dodoma, alienda mbali zaid kwa kupiga marufuku kuuza nyumba au uwanja wowote!!!! Hadi hizo siku 14 zipite
Kwa mnaojua huu ni mwendo wa kukurupuka au ndio utendaji ulivyo mkuu wa mkoa anaweza akanizuia nisiuze nyumba yangu au uwanja wangu kisa maandalizi yake kwa serikali kuhamia Dodoma?? Mm kuhamia dodoma kunanihusu nn?? Uwanja wangu hati yangu maelekezo gani atakayotoa mkuu wa mkoa baada ya siku 14 yatakua mapya kwenye sheria ya ardhi?? Je anaenda kutunga sheria mpya ya umiliki wa ardhi??
Je mm nikiuza uwanja wangu halali nitakua nimevunja sheria gani ya ardhi??
Suruhisho !!
Kama mkuu wa mkoa anahofia watu kutapeliwa angetoa angalizo tu kwamba, wananchi iweni makin kipindi hiki mnaweza kutapeliwa fateni sheria za ardhi msiuziane maeneo kiholela na sio kupiga marufuku kufanya biashara. Maana kwa wengine ujenzi ndio biashara zetu!!!
Je ww unalionaje hili la mkuu wa mkoa kupiga marufuku kununua nyumba au uwanja hadi zipite siku 14 ni sawa?????