RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda akishirikiana na Jeshi la Polisi ametoa siku 90 kwa wamiliki wa silaha kuziwasilisha vituo vya polisi ili kuhakikiwa upya.
Baada ya siku 90 msako mkubwa kuanza.
Chanzo: Habari leo
Baada ya siku 90 msako mkubwa kuanza.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa miezi mitatu kwa wakazi wote wa mkoa huo wanaomiliki silaha, wathibitishe uhalali wa umiliki wa silaha zao kwa mamlaka husika.
Mbali na uthibitishaji wa silaha, pia ameelezea nia yake ya kuanzisha mfumo maalumu wa kupongeza askari Polisi watakaofanya vizuri katika kupambana na majambazi, ambapo kila baada ya miezi mitatu, atamzawadia askari mmoja Sh milioni moja.
Makonda amesema hayo jana jijini Dare es Salaam, wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam. “Askari wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu nimeona niwatengenezee mfumo wa kuwapa motisha hivyo kila baada ya miezi mitatu, nitampongeza askari anayefanya vizuri kwa kumpatia kiasi cha Sh milioni moja,” alisema na kuongeza amechukua uwamuzi huo ili kuhakikisha Dar es Salaam inabaki salama.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuthibitisha uhalali wa umiliki wa silaha, vinginevyo kufikia Julai mwaka huu, hatua zitaanza kuchukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.
“Hatutamfumbia macho yeyote atakayekaidi, lengo letu ni kuona Jiji halikumbwi na matukio ya matumizi ya silaha hasa katika maeneo ya benki pamoja na maeneo mengine,” alisema Makonda.
Chanzo: Habari leo