GE2025 Chalamila, Muliro waibuka Kitambaa Cheupe Sinza, Awataka Watanzania Kudumisha Amani Katika Siku ya Uchaguzi

GE2025 Chalamila, Muliro waibuka Kitambaa Cheupe Sinza, Awataka Watanzania Kudumisha Amani Katika Siku ya Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaagiza Watanzania kulinda amani ya nchi, hususan leo Oktoba 29, 2025, wakati wa zoezi la kupiga kura, akisisitiza kuwa migogoro ya kisiasa inaweza kuathiri sana uchumi na shughuli nyingine za Taifa.

Akizungumza katika eneo la “Kitambaa Cheupe” Club, Sinza, Chalamila alisema vijana walio wengi hawajalala si kwa sababu ya vurugu au wizi, bali kutokana na majukumu ya kifamilia, biashara, na fursa nzuri za kiuchumi zilizopo.

Amewahimiza wananchi wasiogope askari wanaoonekana katika maeneo mbalimbali, akibainisha kuwa wako ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Alieleza mfano wa eneo hilo, akisema endapo kutakuwa na vurugu, biashara zinaweza kufungwa kwa siku tatu hadi wiki moja, hali inayoharibu uchumi na taswira ya nchi.

Chalamila pia alisisitiza kuwa migogoro ya kisiasa haipaswi kuingilia biashara, na kuwa wale wanaohamasisha maandamano hawako nchini bali Marekani na nchi nyingine, hivyo waliopo Dar es Salaam wanapaswa kuendelea na kazi zao bila kuathirika.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema usalama umeimarishwa jijini Dar es Salaam wakati wote wa Uchaguzi Mkuu leo Oktoba 29, 2025.

Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanatekeleza haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu.

Amesisitiza wananchi kujitokeza kupiga kura kwa utulivu na baada ya kupiga kura kurudi majumbani au kuendelea na shughuli zao za kila siku.
 
Back
Top Bottom