Mkuu wa Mkoa ashtakiwa kwa Rais Kikwete

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, Brown Ole Suye, amemshtaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Ole Kone, kwa kuchochea mgogoro wa ardhi kwenye shamba lake.

Akizungumza na Mwananchi jana, Ole Suye alisema amefikia hatua hiyo kwa kumpelekea barua Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ili amuonye au kumwajibisha Dk Kone kutokana na kutaka kuvunja amani wilayani Simanjiro.

Katika barua hiyo, ambayo Mwananchi imeiona Dk Kone amepewa nakala yake sambamba na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Dk Kone pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

“Nimemwandikia rais barua ya malalamiko na nina imani ameipata...Kone amekuwa mchochezi wa mgogoro wa ardhi kwenye shamba langu lenye ukubwa wa hekta 3,425 ambazo nilikabidhiwa kihalali tangu mwaka 1978,” alisema Ole Suye.

Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa, licha ya kupata hati miliki ya shamba hilo, baadhi ya viongozi wa siasa akiwamo Dk Kone, kuanzia mwaka 2010 wameibuka na kudai kuwa ardhi anayomiliki sio halali.

“Wamekuwa wakivamia shamba langu na kuharibu mali, washtakiwa wamekuwa wakikamatwa, lakini hawajafikishwa mahakamani licha ya kufunguliwa mashauri mawili tofauti,” alisema.

Pia, Ole Suye alimuomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Mashtaka, kumsaidia kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani ili kukomesha uvamizi wa shamba lake.

Alisema shamba hilo lililopo Kijiji cha Loiborsoit nyumbani kwa Dk Kone, tangu kuanza vurugu hizo mwaka jana, ameshindwa kuliendeleza kutokana na uvamizi ambao umekuwa ukifanywa na wananchi kwa shinikizo la kisiasa.

Mwenyekiti huyo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mbunge wa Simanjiro, Christopha Ole Sendeka, alisema shamba hilo ambalo ni kati ya mashamba 34 yaliyotolewa kwa watu mbalimbali mwaka 1978, amepata mwekezaji ambaye watashirikiana kuwekeza zaidi ya Sh3 bilioni.

“Pale kwenye shamba langu Oldupai Seed Company Ltd, nashindwa kupanua kazi zangu na tulipanga na mwekezaji kuanzisha ranchi, wamekuwa wakiweka vizingiti kwanza wanapinga kufanya mabadiliko ya matumizi ya ardhi, lakini baada ya kukubaliwa na serikali ndio uvamizi umeshamiri,” alisema.

Alishangazwa na Mkuu huyo wa mkoa kumpinga Mtanzania kumiliki eneo hilo, wakati kuna mashamba 33 yanamilikiwa na watu mbalimbali wakiwamo toka nje ya nchi na hawasumbuliwi.

Hata hivyo, Dk Kone amekuwa akikanusha kuchochea vurugu, huku akimtupia lawama Ole Suye kuwa ndiye mwenye matatizo kutokana na kutofuata sheria na kutotumia shamba hilo kwa muda mrefu.
 
kumbe nao huwa wanashtakiana!!!na anamshtaki ili kikwete amfanye nini sasa!
 
Ole Suye = Ole Kone

ukikata ole pande zote mbili inabakia Suye=Kone

kata "e" pande zote mbili: Suy=Kon sasa tukiwaynganisha inakuja kichina yaani SuyKon.

Hapa kwa utabiri wangu hakuna tatizo wala ugomvi maana nyota ya kichina imekubali: Suykon.
 
It won't make any difference wanashitakiana kwa mwenzao mnadhani atafanya nini?!
 
Mungu siyo Athumani!! Chanzo cha matatizo yasiyokwisha Simanjiro karibu kitajulikana. Land grabbers wengi sana wenye vyeo vikubwa serikalini waanze kutajana na kurudisha ardhi ya wananchi. Labda kwa kufanya hivyo, wataacha kutumia remote control kuchagua viongozi wa vijiji, kata na hata wabunge ili walinde mashamba yao na mali nyingize kama vitalu vya uwindaji, madini etc. Vita vya kiuchumi vina gharama kubwa sana. Every one whats to be sanctified kumbe ni jambazi kuliko mwenzake. Stay tuned....
 
Back
Top Bottom