Mkuu wa Mkoa aagiza zoezi la watumishi hewa kurudiwa upya

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana kilichojumuisha wazee , viongozi wa dini , watendaji wa umma na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo. Akisisitiza kuwa hajaridhishwa na uhakiki, hivyo akaagiza halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa watumishi.

“Siku ile ile nilipoapishwa kabla sijavuka geti kutoka nje ya Ikulu nilipiga simu na kuagiza halmashauri zote (Manispaa, Nkasi, Kalambo na Sumbawanga) kuanza uhakiki mara moja wasinisubiri hadi niripoti mkoani hapa,”alieleza.

Aliongeza kuwa aliporudi mkoani humo na kuripoti kazini katika siku yake ya kwanza ofisini alikabidhiwa kitabu chenye orodha ya watumishi wa umma wa halmashauri zote akielezwa kuwa hakuna mtumishi hewa katika mkoa wa Rukwa.

“Sikukubaliana nao nilikataa, nikaagiza ufanyike uhakiki mara moja ndipo wamepatikana watumishi hewa 18 na watumishi wengine 137 wapowapo tu wakiwa na taarifa zinazotia mashaka. Wote wamebainika kwenye hicho kitabu nilichokabidhiwa kikionesha hakuna mtumishi hewa,” alisisitiza.

Wakati huo huo Zelothe amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo, Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo hivi karibuni.

Pia ameagiza fedha hizo zilizolipwa kwa watumishi hao hewa na kuiingizia hasara kubwa Serikali zirudishwe mara moja.

Akifafanua alisema katika uhakiki huo, watumishi hewa tisa walibainika katika wilaya ya Nkasi, wanane katika Manispaa ya Sumbawanga na mmoja wilaya ya Sumbawanga wakati Kalambo ikiwa haina mtumishi hewa.

Uhakiki huo unatokana na maagizo aliyotoa Rais John Magufuli baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa aliowateua, aliwaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za wananchi na sio kwenda kufanya siasa.

Pia Rais Magufuli aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika orodha ya malipo ya mshahara wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.


Kwa hisani ya Habarileo
 
Huko nyuma nimewahi kusema, Inafaa Rais Magufuli aunde kikosi maalum ambacho ni independent ili kikafanye verification katika kila mikoa kuhakikisha kama repoti waliyoleta Wakuu wa Mikoa ni kweli au usanii. Haiwezekani Wakurugenzi ambao ni watengeneza wafanyakazi hewa eti wawe ndio watafuta wafanyakazi hewa.

Inashangaza Mkoa kama wa Shinyanga eti hauna wafanyakazi hewa. It's unthinkable and unjustifiable.

Maelezo zaidi yanapatikana katika thread/mada hii;
 
Nazani wengi wao ni wale waliofariki au kucha kazi lakini bado wapo kwenye payroll, Sasa mishahara yao jamaa wanaipiga.
Swali langu,je atakaye kamatwa ni yule aliyekula hela zao ama hao walio acha kaz? Maana kasema wakamatwe hao watumish hewa 18,,ndo cjamsoma hapo
 
Huyu afande ubongo umechoka,yaani wakamate hewa....au hajui maana halisi ya watumishi hewa...ukistaafu maana yake ubongo na misuli imechoka sasa baba watu mmemuongeza chance ya kuugua kisukari buree
 
Swali langu,je atakaye kamatwa ni yule aliyekula hela zao ama hao walio acha kaz? Maana kasema wakamatwe hao watumish hewa 18,,ndo cjamsoma hapo
Ila inawezakana kwa wale ambao walioacha kazi wakawa wanatumia mapugufu ya mfumo wenyewe na kuendelea kupokea mshahara kwa sababu ya kuchelewa ku update database yao na hasa kama mishahara inapitia bank moja kwa moja, Sasa nazani labda anazungumzia hawa.na hawa kuwatrace ni rahisi.
 
Yaani eti umetoka tu kuapishwa unanipigia simu kuanza kuniamuru nifanya hiki na kile!! Mimi nakutolea nje tu, nikusikilize nakujulia wapi? Nitahakiki vipi kama ni wewe? lbda kama hiyo simu siyo hizi za kawaida bali ni special channels of communication zinazonitambulisha kama mkuu wa mkoa
 
Hahha,watumishi hewa wanakamatwaje sasa..au hajui maana ya hewa(Ghost worker) au non exist worker
Nilitegemea Aseme wakamatwe waliotengeneza wafanyakazi hewa! Ha
Hahha,watumishi hewa wanakamatwaje sasa..au hajui maana ya hewa(Ghost worker) au non exist worker
Mkuu wa mkoa aliyewahi kuwa KAMANDA wa police hajui nini maana ya wafanyakazi hewa ni ajabu! Nilitegemea Aseme wakamatwe waliotengeneza wafanyakazi hewa na wala sio kukamata wafanyakazi hewa! Hapa ndio utaamini hajui hata alikuwa anasema au kuongea nini! Hivi vyeo vingine vinahitaji teuzi zake ziangalie weledi zaidi ya ukada
 
Ila inawezakana kwa wale ambao walioacha kazi wakawa wanatumia mapugufu ya mfumo wenyewe na kuendelea kupokea mshahara kwa sababu ya kuchelewa ku update database yao na hasa kama mishahara inapitia bank moja kwa moja, Sasa nazani labda anazungumzia hawa.na hawa kuwatrace ni rahisi.
Asa mkuu,kama mtu kaacha kaz,na document zake za kuacha kaz zpo.huon kama uongoz na utumish ndo wenye makosa? Maana ilibid wamtoe kwenye payroll...sidhan hata ww umeacha kaz,lkn mshahara ukiwa bado unaingia utaurudisha au kwenda kuripoti.
 
Utamkamata vipi labda mtumishi aliyeacha kazi ila maboss wake wanaendelea kula pesa zinazotengwa kama mshahara? Mimi nafikiri wa kukamatwa ni wale walioweka majina ya watumishi ambao hawapo kazini.
 
Hahha,watumishi hewa wanakamatwaje sasa..au hajui maana ya hewa(Ghost worker) au non exist worker
Hukusikia Rais Magufuli alisema kuna mtumishi alikuwa anapokea mishahara 17

Wewe unadhani hizo pesa za mishahara zilizokuwa zinalipwa zilikuwa zinaenda wapi?
 
Utamkamata vipi labda mtumishi aliyeacha kazi ila maboss wake wanaendelea kula pesa zinazotengwa kama mshahara? Mimi nafikiri wa kukamatwa ni wale walioweka majina ya watumishi ambao hawapo kazini.
Ndiyo maana hiyo.

Watakamatwa wale waliokuwa wanapokea pesa za majina ya watumishi ambao hawapo.
 
Hukusikia Rais Magufuli alisema kuna mtumishi alikuwa anapokea mishahara 17

Wewe unadhani hizo pesa za mishahara zinaenda wapi?
Mkuu,nichosema ni hv...wa kukamatwa ni huyo aliyetengeneza hayo majina ya watu 17 as if ni wafanyakazi,kumbe ni hewa(ghost worker au non exist worker).maana yake,kiuhalisia hao wafanyakaz hawapo
 
Kutokana na uzoefu wangu, Rukwa ina vigezo tosha vya kuwa na watumishi hewa unless kama ma- DED na wakuu wa idara wote mkoani ni makini!

Eneo la kwanza linalozalisha watumishi hewa ni pale mfanyakazi anapoajiriwa na kwenda kuripoti wakati keshaingizwa kwenye payroll! Baada ya muda, the same employee ana - struggle kuhama na wakati mwingine akishindwa anaweza kuacha hata kazi na kuingia mitini! Case kama hii ni very common kwa mikoa na remote districts including Rukwa na wilaya zake! Na ni kawaida sana kuona hawa watu wanaendelea kuwa kwenye payroll na kukinga salary wakati si ajabu anafanya kazi zake binafsi! Na wala msidhani pesa za Case kama hiyo zinapigwa na Halmashauri-- ni uzembe wao tu ndio unawaponza!

Case nyingine ya wafanyakazi hewa inaanzia Halmashauri!! Back then I was NMB Banker halafu nilikuwa mnoko balaa ( Watu wanaofuata taratibu Bongo tunawaita wanoko)! It's 2008 serikali ilikuwa imeajiri walimu wengi sana na wafanyakazi wa kada zingine-- cha kushangaza; over 90% ya waalimu waliokuja pale benki kufungua a/c walikuja wakiwa na introduction letters zisizo na picha lakini picha wameshika mkononi na hata yale mavitambulisho yao mabaya ya njano ya serikalini yale nayo walikuja nayo hayana picha lakini wana picha mkononi! Yaani huko Halmashauri walikuwa wanatoa barua na vitambulisho kama njugu-- and am sure kwa hali jinsi ilivyokuwa, walipewa hata wasio na sifa!

Na huu unoko wangu wa asili na ndo nilikuwa mwenye sauti pale kaunta-- watu nikawarudisha walikotoka na kuwataka warejee wakati ID na barua zao zikiwa na picha with a stamp across the photo to the letter and/or ID na signature iwe STRICTLY from signatories ! Msidhani kwamba niliwasumbua coz' every Department Head ni signatory anayetambulika benki! However, Walinipaka sana but sikuwa na namna!! So, inapotokea mass employment nayo inakuwa wakati muafaka wa watu wa wizarani na Halmashauri kutengeneza ghost employees!
 
Asa mkuu,kama mtu kaacha kaz,na document zake za kuacha kaz zpo.huon kama uongoz na utumish ndo wenye makosa? Maana ilibid wamtoe kwenye payroll...sidhan hata ww umeacha kaz,lkn mshahara ukiwa bado unaingia utaurudisha au kwenda kuripoti.
Uta take advantage ila inabidi ujiandae kuirudisha wenyewe wakikuambi rudisha maana siyo zako, ni sawa na mtu amekuingizia hela kwenye account yako kimakosa na wewe unaila tu bila kujua inatoka wapi kwa hiyo lazima uitapike.
 
Back
Top Bottom