Mkuu wa Kituo Polisi adaiwa kumjeruhi mwananchi Mkuu; hi sasa hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Kituo Polisi adaiwa kumjeruhi mwananchi Mkuu; hi sasa hatari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lifeofmshaba, May 22, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu wa Kituo Cha Polisi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makambako wilayani Njombe, ASP Mshana Mjema, anadaiwa kumjeruhi mwananchi mmoja kwa kumpiga virungu na kumsababishia madhara makubwa mwilini.

  Mwananchi aliyejeruhiwa ni Zakaria Mgihilwa (50) mkazi wa Makambako, ambaye alitakiwa na mkuu huyo wa polisi amuuzie kipande cha shamba katika eneo la Kipagamo nje kidogo ya mji huo.
  Hata hivyo, ASP Mjema alikanusha madai hayo, huku akisema yeye sio msemaji wa masuala yanayohusu utendaji wa kila siku wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

  Mgihiliwa anasema makubaliano ya kuuziana shamba hilo, yalifanywa kwa ushirikiano baina ya Meneja wa Pride Makambako, aliyemtaja kwa jina la Mariam Ntobi na ASP Mjema, kwa makubaliano ya malipo ya Sh. 100,000. Mgihilwa alisema baada ya makubaliano hayo, alipewa kiasi cha Sh. 50,000 ikiwa ni nusu ya makubaliano hayo, na kupewa ahadi ya kulipwa kiasi kilichobaki baada ya wiki mbili.

  Hata hivyo, anasema baada ya wiki mbili kupita aliamua kumfuata ASP Mjema ofisini kwake kwa ajili ya kukamilisha ahadi hiyo, lakini hakuweza kukutana na mdeni wake na kuamua kujiandaa kwa siku ya pili.Alisema siku ya pili mapema alfajiri aliamshwa na kelele za mabinti zake waliokuwa wakilalamikia hatua ya Mkuu huyo wa Polisi kutaka kuingia chumbani kwao kwa nguvu akidai kumtafuta baba yao.

  “Niliposikia hali hiyo, nilikurupuka na kuamua kutoka nje ya chumba changu na mara moja nilikutana na ASP Mjema ambaye alioneaka kuwa mwenye hasira na ambaye alinitaka kutoka nje kwa nguvu,” alisema Mgihilwa.

  Alisema alipohoji kwa nini anatakiwa kutoka nje akiwa na taulo, wakati alikuwa hajui ana kosa gani, na kuomba apewe muda wa kuvaa suruali, alipigwa na kirungu cha polisi na kulazimika kulala chini.

  “Huyu jamaa alionyesha ukatili wa hali ya juu, alinipiga kwa fimbo kama mtoto mdogo, huku akiniburuza akiwa na askari mmoja wa kitengo cha usalama barabarani (Trafiki) aitwaye Chrisant,” alisema huku akitokwa na machozi.

  Alisema alidhalilishwa vya kutosha mbele ya watoto wa kike, huku akiondolewa nyumbani kwake kwa kuburuzwa kama mzigo wa kuni, huku akiwa tayari ameumizwa na kupelekwa kituo cha polisi, ambako alifungiwa mahabusu bila kupewa huduma ya aina yeyote ya matibabu.

  Mgihilwa alisema jamaa zake wa karibu walifika katika kituo hicho cha polisi na kuomba apewe dhamana, lakini askari waliokuwa zamu waligoma kufanya lolote kwa maelezo kwamba OCS huyo alizuia dhamana yake, akidai anataka kumuonyesha kwamba yeye ni nani Makambako.

  Alisema baadaye alipofanikiwa kupata dhamana alikataliwa kata kata kupewa fomu maalum ya matibabu PF 3, hatua iliyomkosesha huduma za afya, hivyo kulazimika kumtumia afisa mmoja wa Tume ya Haki na Amani ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, ambaye alifanikisha kupewa PF3.

  “Baada ya hapo, nilifanikiwa kupelekwa hospitali, lakini ilibainika kwamba mahali ambapo ningeweza kupatiwa tiba ya uhakika kutokana na maumivu makubwa ni Hospitali ya Ilembula, nikolazwa kwa muda na kutokana na kukosa fedha na uzito wa gharama, nilirudishwa nyumbani,” alisema Mgihilwa.

  Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa polisi wilaya ya Njombe kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai OC CID ASP Kamugisha, ambaye alichukua taarifa za mlalamikaji huyo kwa ajili ya hatua za kisheria.

  Hata hivyo, siku mbili baadaye alilifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SAPC Evaristo Mangala kwa hatua zaidi.

  Alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi, SAPC Mangala alikiri kupokea malalamiko ya mwananchi huyo, huku akionyesha masikitiko yake na kusema alimuagiza Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa
  Mkoa huo (RCO) SSP Mwaisyeba, ili alifuatilie na baadaye amfahamishe aweze kuchukua hatua za haraka.

  Alisema tayari ameagiza kufuatiliwa kwa suala hilo haraka, ili haki iweze kutendeka kwani matukio ya aina hiyo yanapunguza heshma ya polisi kwa jamii.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  polisi wanaendelea kutesa na kuua rais wasio na hatia
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Alianza zombe, wakafuata polisi wa arusha (raia kwenye gas station+maandamano ya chadema), kisha OCD wa kigoma na sasa njombe, sijui kesho ni zamu ya wapi/nani..............................
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  polisi wanaendeleza ubabe wao dhidi ya raia no wonder wale wa Nzega waliamua kuua askari ni kwa mabo yao haya haya wanajiona wako juu ya sheria ila their day will come when we will be free na utawala wa sheria utakuwepo
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ila Zombe alikuwa jiwe hasa ila side B ndiyo ilkuwa mbaya. Hawa wengine wao hawana side A wala B wote ni wabaya tu wanaua watu na kuwa nyasa nyasa bila sababu na mara nyingi ni kuwaonea tutageuka Misri na Tunisia kuwaonyesha wao si lolote. Oh wengine watasema Uhaini
   
Loading...