The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Kuna maneno maneno kwamba kiongozi wetu Mkuu ni mbabe na hasikilizi la mtu, anatisha wasaidizi wake na kadhalika.
Binafsi naamini huyu kiongozi ni afadhali kuliko mwingine yeyote aliyeonesha nia ya kuingia Magogoni katika mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa 2015.
Pia anakubalika sana kwa mazuri yake na anaungwa mkono na tulio wengi.
Hata hivyo ni vizuri tukawa wakweli kwamba kuna mambo hapaswi kufanya endapo nia yake thabiti ni kutaka kuikwamua Jamhuri yetu pendwa dhidi ya lindi la umasikini, rushwa na ubadhirifu.
1. Asikusudie sana kuumiza watu kwa kukomoa. Mfano kutamani watu waishi kama mashetani. Hii isipochekiwa kwa weledi itaumiza hata wasiohusika.
2. Asichague kupokea mazuri tu kama maneno pekee kutoka kwa washauri na wasaidizi wake.
Mfano mtambo unapogoma kufanya kazi kwa kukosa matengenezo sababu ya ukosefu wa fedha asimtishe mtu anayemwambia ukweli maana mwisho atadanganywa tu ili watu wasikose vibarua vyao.
Hapa kuna uvumi kwamba taasisi moja Wizara ya Mambo ya Ndani itashindwa kuwalipa maaskari wake stahiki halali na za kimsingi (wenzao taasisi nyingine pacha wanapewa) kwa sababu tu viongozi wa taasisi hiyo wanaogopa kueleza matumizi halisi kwa kuhofia kuambiwa kama hazitoshi waondoke. Fedha waliyotengewa kwenye bajeti haitoshi inasemekana.
3. Asipuuze kuwatumia jopo la ushauri lenye wataalamu tulilotangaziwa wakati wa kampeni. Naamini wakipewa nafasi hawa nchi itasonga bila vikwazo kama ilivyotokea kwenye sukari.
4. Ashughulikie kwa usawa matatizo ya ufisadi hata kama itawaumbua watoto wa watangulizi wake. Kama watu wamekosea hakuna namna nyingine.
5. Rushwa na ufisadi ulikuwa umeota mizizi sana na ili kuuondoa ni vizuri taasisi zinazompa taarifa zikasafishwa vizuri kuhakikisha zinaaminika.
6. Ni muhimu watumishi wakajengewa fikra za kufanya mazuri kwa ajili ya taifa pasipo kujali kuna camera za waandishi au la. Siyo lazima Mkuu wa Mkoa kurekodiwa anawakemea watumishi kwa maneno ya vijiweni ili kuonekana anafanya kazi.
.....