Paul Medald
Member
- Jun 3, 2022
- 41
- 70
Mkuu wa jeshi la Uingereza: "Lazima tuwe tayari kupigana tena Ulaya".
Barua ya Kamanda ilitumwa kwa askari na maafisa wote wa Jeshi la Uingereza, pamoja na watumishi wa umma. Image caption: Barua ya Kamanda ilitumwa kwa askari na maafisa wote wa Jeshi la Uingereza, pamoja na watumishi wa umma.
Mkuu mpya wa Jeshi la Uingereza, Patrick Sanders, ametangaza kwa wanajeshi kwamba lazima wawe tayari kwa vita vipya barani Ulaya.
BBC imepata risala iliyosambazwa kwa barua kwa jeshi la Uingereza.
"Sasa ni muhimu kuunda jeshi ambalo linaweza kupigana pamoja na washirika wetu na kuishinda Urusi katika mapigano," Sanders alisema.
Kulingana na yeye, kazi kubwa sasa ni kuongeza kasi ya kisasa ya vikosi vya jeshi la Uingereza ili kuimarisha NATO na kutoruhusu Urusi kusonga mbele zaidi katika eneo la Ulaya.
"Sisi ni kizazi kinachopaswa kuandaa jeshi kupigana tena Ulaya," Sanders alisema katika waraka.
Kulingana na kamanda huyo, yeye ndiye mkuu wa majeshi tangu 1941 kuliongoza jeshi la Uingereza katika vita vya ardhini vilivyohusisha nguvu ya bara huko ulaya.
Patrick Sanders alichukua wadhifa wa mkuu wa wafanyikazi mnamo Jumatatu, Juni 13.
"Uvamizi wa Urusi kwa Ukraine unasisitiza dhamira yetu ya msingi - kutetea Uingereza na kuwa tayari kupigana na kushinda vita vya ardhini - na kuimarisha hitaji la kuzuia uchokozi wa Urusi kwa tishio la nguvu zetu."