mkuu wa al-qaeda akamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mkuu wa al-qaeda akamatwa

Discussion in 'International Forum' started by OSOKONI, Mar 1, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,789
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa Al Qaeda akamatwa Misri

  Maofisa wa usalama nchini Misri wanasema wamemkamata mmoja wa wakuu wa mtandao wa al-Qaeda kwenye uwanja wa ndege wa Cairo, Saif al-Adel.

  [​IMG]

  Saif al Adel


  Alikamatwa pindi alipowasili kwenye ndege kutoka Pakistan.

  Maofisa hao waliwambia wandishi habari kua walifahamu kuhusu nia yake ya kujisalimisha, na kwamba jina lake halisi ni Mohammed Ibrahim Makkawi na alikua kwenye orodha ya abiria waliosafiria ndege hio.

  Mtu huyo ambaye zamani alikua nwanajeshi wa Misri akiwa wa ngazi ya kanali. Wakati mmoja alikua mkuu wa usalama wa Osama Bin Laden na pia anatakikana na Marekani kuhusianiana na mashambulio ya balozi za Marekani huko Afrika mashariki mnamo mwaka 1998.

  Halikadhalika anatuhumiwa kwa kuwapa mafunzo wapiganaji wa Kisomali walioshiriki mauwaji ya wanajeshi wa Marekani 18 mjini Mogadishu mwaka 1993 pamoja na washambuliaji walioshiriki shambulio kabambe la Marekani mwezi septemba mwaka 2001.

  Saif al-Adel yuko msitari wa mbele kwenye orodha ya shirika la kijasusi la Marekani FBI ambapo Marekani imetoa zawadi ya dola milioni 5 za Kimarekani kwa habari yoyote itakayowawezesha kumkamata au hata kumuua.

  Maofisa wa usalama wamliambia shirika la habari la Misri, Mena kua Saif Adel alizuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Cairo alipowasili leo jumatano baada ya safari yake kutoka Pakistan akipitia Dubai.

  Kamanda huyu wa vikosi vya Misri ambaye alihudumu katika vikosi maalum, ana umri ulio kati ya miaka 50 hivi na alikwenda kushiriki vita nchini Afghanistan mwaka 1980 akijiunga na kundi la Mujahidin dhidi ya vikosi vya Urussi.

  Tangu mwaka 1987 amekua akisakwa na wakuu wa Misri alipotuhumiwa kwa kutaka kuunda tawi la kijeshi la kundi la Al Jihad nchini Misri kwa nia ya kuiondoa madarakani serikali ya Misri.

  Baadaye Saif al-Adel alijiunga na al-Qaeda na moja kwa moja kua mkuu wa usalama wa Osama Bin Laden. Aliridhi majukumu mengi yaliyokua yakishikiliwa na Kamanda wa jeshi Mohammed Atef alipofariki kufuatia shambulio la Wamarekani mwezi novemba mwaka 2001.

  Baada ya uvamizi wa Marekani wa Afghanistan mwaka 2001, inaaminika kua Saif al-Adel alikimbilia nchini Iran pamoja na Saad Bin Laden, mwanawe kiongozi wa al-Qaeda leader marehemu Osama Bin Laden.

  Nchini Iran inasemekana kua walizuiliwa na wakuu wa serikali ya mapinduzi ya Iran ingawa wakuu hao walikanusha habari za kuwemo nchini mwao.

  Zimekuepo tetesi kua Saif aliteuliwa kama kiongozi wa mda wa al-Qaeda baada ya kifo cha Osama Bin Laden mwezi May mwaka jana katika mji wa Abbottabad huko magharibi mwa Pakistani.
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hongereni
   
 3. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  al qaeda ndo inapotea hivyo-mmoja mmoja hadi wote waishe
   
 4. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni Ayman Al-Zawahiri, huyo sio mkuu
   
 5. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkwewe Osama ataendelea kuwa kiongozi wa kutetea wanao onewa na ubeberu wa kimagharibi.

  Saif kama angekuwa hataki kushikwa wala wasingempata. Kaji salimisha mwenyewe. Sababu iliyo mfanya akimbie Misri ni serkali ya Mubarak. Naye hayuko. Ameona bora arudi kwao. Anajiamini kuwa aweza kutoa msaada wa kuisukuma Misri kuelekea kwenye amani ya kudumu.

  Huko Misri bado kuna wengi ambao wanamkubali. Hasa baada ya bunge la chini kunyakuliwa na Islamic Brotherhood.

  Tuone watamfanya nini.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ilianzishwa na wamarekani, kazi yake ya kuwachongea waarabu against dunia imeisha sasa ndio wana phase out, wakimaliza watahamia kutuibia rasilimali sasa
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  jamaa ni kaka wa obama?wamefanana.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  One day at a time. One al qaeda at a time. Inshaaalah, watamaliza tu hawa.
   
 9. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  umekosea-haijaanzishwa na usa-ila ilipewa momentum na usa-for a specific reason,wakaja kuwa na motives tofauti-then wakatofautiana
   
Loading...