Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mkutano ulioitishwa na viongozi wa mtaa wa Onjuvatian kata ya Sokoni One jijini Arusha umevunjika baada ya viongozi hao kushindwa kusoma mapato na matumizi ya fedha zao na pia kuwaonyesha risiti za vitu vilivyonunuliwa kwa fedha za michango yao.
Kabla ya mkutano huo kuvunjika wananchi hao waliwataka viongozi kuwasomea mapato na matumizi ya fedha zao walizochanga kwa muda wa miaka miwili na pia kuwaonyesha risiti ya manunuzi jambo ambalo licha ya viongozi hao kushindwa kulitekeleza walionyesha risiti bandia hali iliyoibua hasira kwa wananchi hao.
Baada ya hekaheka Mwenyekiti anayetuhumiwa Bw,Joseph Kimaro alikiri kutenda makosa hayo na akawaomba wananchi hao wamsamehe na kumpa muda wa kurekebisha makosa ombi ambalo hata hivyo wananchi hao walilikataa