Mkutano wa Rais Magufuli na viongozi wa dini wawatia kiwewe UKAWA na ACT-Wazalendo, wahaha kukutana nao

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Vyama vinaavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na ACT-Wazalendo vimeomba kukutana na Vingozi wa Madhehebu ya Dini.

Lengo la Maombi hayo ya UKAWA na ACT-Wazalendo yametajwa kuwa ni kutaka kuwatumia Viongozi hao kuwashawishi Wamumini wao ambao kimsingi ndiyo mtaji wa Uhai wa Vyama vya Siasa kupitia Sanduku la kura waendelee kuwaamini.

Wamefikia uamuzi huo baada ya kuingiwa hofu ya kupoteza wafuasi kwa kasi baada ya Mkutano wa Viongozi wa Dini na Rais Magufuli pale ikulu kuonekana kuyaunganisha Madhehebu na Dini zote na kuongea lughs moja ya kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano.

Sababu nyingine ya maombi ya Viongozi hao wa Vyama vya Siasa kutaka kukutana na Viongoxi wa Dini imetajwa kuwa ni kuwaomba radhi kufuatia baadhi ya Wanachama wa Vyama hivyo kuwashambulia kwa Matusi na Kebehi za kila aina kufuatia baada ya Viongozi hao kwenda Ikulu kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pomba Magufuli.

Habari zilizothibitika zinatanabahisha kuwa tofauti na ilivyokuwa kwa Viongozi hao wa Dini kwenda Ikulu wote kwa pamoja bila kujali wanatoka taasisi gani au Dini gani, Ratiba ya UKAWA na ACT-Wazalendo inaonesha watakutana na Viongozi hao Kila Taasisi kwa nyakati tofauti.

Zipo taarifa kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwagawa kimtazamo na kuusambaratisha Umoja na Mshikamano wao walioonekana kuujenga siku za hivi karibuni na hasa baada ya kuwa wamekutana kwa pamoja takribani Taasisi zote

Katibu Mwenezi wa ACT-Wazalendo Taifa, Ado Shaibu ndiye aliyeteuliwa na vyama washirika wa Makubaliano hayo kuzifikia Taasisi za Dini kwa njia ya kuziandikia barua za Maombi ya kutaka kukutana na Vyama hivyo.

Taarifa Zaidi zinasema mpaka sasa Taasisi ya 'CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA'-CCT Dodoma tayari wamepokea barua ya Maombi hayo kupitia kwa Katibu wa Taasisi hiyo aliyetambulika kwa jina moja la CHILEDYA.

CCT inayoundwa na Madhehebu ya Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moravian, Anglikana, 'African Inland Church'-AIC, Baptist, Psybetarian na Mennonite. Aidha Dhehebu la T.A.G ambalo Kiongozi wake Mkuu ni Barnabas Mtokambali nalo limepokea barua kutoka kwa Mratibu ADO Shaibu ila kwa mashari kuwa majibu watayapata pindi atakapowasili nchini Askofu mtokambali ambaye hadi wanapewa barua alikuwa nchini Marekani kikazi.

TAG ni mwanachama wa Christian Pentecoste Church Of Tanzania(CPCT) , taasisi ambayo kwa mujibu wa Chanzo cha Habari imeshindwa kufikiwa na Mratibu Ado Shaibu kwa madai kwamba hawajui Ofisi zake zilipo.

Hata hivyo barua kwa CPCT itawasilishwa kwa Mchungaji kiongozi wa T.A.G Kawe ambaye ndiye Katibu mkuu wa CPCT. Ndugu Mputa wa Msikiti wa Ghadir karibu na Kituo cha Polisi cha Kigogo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Maulana Sheikh Hemed Jalala amekiri kupokeda barua ya Viongozi ho wa Ukawa na ACT-Wazalendo kwa ajili ya kukutana nao tarehe 21/02/2019. kwa mujibu wa bwana Mputa, Sheikh Jalala alikuwa safarini na haijajulikana kama amesharudi aua la.

Viongozi hao wa Vyama vya upinzani ambao wameamua kukutana na Viongozi wa Taasisi za Dini kwa nyakati tofauti kwa lengo tajwa hapo juu, wamepelekea baraua baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) lakini mpaka tarehe 15/02/2019 sasa 10:00 jioni walikuwa hawajapokea majibu ya barua yao kukubaliwa au kukataliwa.

Wakati Viongozi hao wa Vyama vya Upinzani wakihaha kutaka kuonana na Viongozi wa dini kwa kile kinachodaiwa kuwa ni baada ya kuingiwa hofu ya kukosa wafuasi kutokana na Viongozi hao ambao ndiyo wenye wapiga kura kuonesha Dhahiri Shahiri kuwa wanaunga mkono Kazi nzuri ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais , Dkt. John Pombe Magufuli, umetokea mtafaruku baina ya Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo , Doroth Semu (0784500862) na Mwenykiti wa Ngome ya Wazee ya Chama hicho Hamad Rajab Tao (0755949221) baaba ya SEMU kumkatalia RAJAB asiitishe mkutano wa Wandishi wa Habari ili kuwalaumu Viongozi wa Dini kwa kitendo chao cha kukubali Mwaliko wa Rais ikulu jijini Dar es Salaam mwezi uliopita karibuni.

Sehemu ya taarifa iliyotarajiwa kutoleawa na Ngome ya Wazee wa ACT-Wazalendo kwa Wandishi wa Habari ilitolewa kama barua kwenye gazeti ala Mwananachi la tarehe 30/01/2019 ukurasa wa 11 yenye kichwa cha habari "VIONGOZI WA DINI WAMETUANGUSHA". SEMU alichukua hatua ya kukatalia Mkutano kwa vile kufanya hivyo kungeweza kuzorotesha Mpango wa kukutana na Viongozi hao.

Tafakuri yangu: Vyama vya siasa vina haki ya kukutana na Viongozi wa dini ili kubadilishana mawazo lakini Kwanini watumie muda mwingi na gharama kubwa kukutana na Viongozi hao kwa nyakati tiofauti? kwanini wasifanye kama ilivyokuwa Taasisi zote za dini zilivykutana pale ikulu na Rais ? Hofu ya Viongozi hao wa vyama vya siasa kukosa Wafuasi eti kwa sababu Vipongozi wa Dini wamekutana na Rais inatokana na nini?

Viongozi wa dini muwe makini, kugawanywa huku vikundi vikundi hakuna afya kwenye Taasisi zenu na hata kwa taifa. Mnagawanywa ili mfarakanishwe ndani ya Taasisi, baina ya Taasisi na Tasisi au hata na Serikali. Ingependeza kama mngewashauri hao Viongozi wa Vyama vya siasa wawaite wote kwa pamoja kama Serikali ilivofanya ili muweze kuwa na mrengo mmoja wa mawazo kwa mstakabali wa Amani na mshikamano wa Taifa letu.

Jumatatu njema.
 
Unahangaika sana kwani wao hawana haki ya kukutana na viongozi wa dini, mbona wakati Magufuli akikutana nao ikulu hukusema anakiwewe anataka kuwatumia au anataka kutubu kwa serikali yake kuhusishwa na shambulio la Lissu? Sometimes try to think positively.
 
Wapinzani tulichemka pale tulipoonesha mihemuko na kuanza kuwakashifu Viongozi wa dini, tutakuwa na kazi sana kujisafisha
 
angalia nilichokiandika kwenye tafakuri
Na wewe soma tena nilichokujibu umeandika as if CCM tu ndio wenye haki ya kukutana na viongozi wa dini wakati ni juzi tu mmetoka kuwakashifu maaskofu, acheni kuwafanya watu wajinga mkifikiri hawajui kinachoendelea.

Unahangaika sana kwani wao hawana haki ya kukutana na viongozi wa dini, mbona wakati Magufuli akikutana nao ikulu hukusema anakiwewe anataka kuwatumia au anataka kutubu kwa serikali yake kuhusishwa na shambulio la Lissu? Sometimes try to think positively.
 
Wapinzani tulichemka pale tulipoonesha mihemuko na kuanza kuwakashifu Viongozi wa dini, tutakuwa na kazi sana kujisafisha
Kwani CCM mara ngapi imewakashifu viongozi wa dini, unakumbuka mwaka jana waraka ulipotoka mliwaambiaje maaskofu, mara ngapi wamemtukana Gwajima, mara ngapi wamemkashifu Kakobe, ina maana walipoitwa ikulu Magufuli alikuwa anatubu? acheni kuwafanya watanzania wajinga.
 
Viongozi wa dini msikubali kukutana na hawa wahuni, na hawana locus maana si watawala, waambieni wahudhurie tu kanisani au misikitini kwenye ibada
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Hawa wapinzani lazima kuna mkono wa kibeberu. Jpm anakutana na viogozi wa dini kama rais na mkuu wa serikali sio kama ccm ili kupata maridhiano kuhusu mipango ya serikali na mstakabali wa taifa. Sasa ukawa na act sijui wanataka kuwaambia nini viongozi wa dini..ni eneo jipya na hatari la kufanya siasa wapinzani.
 
Mnaohaha ni nyie! Anye kuku akinya bata kaharisha! Jiwe mbona alikutana nao na ukawa hawakuongea kitu? Ukawa kukutana nao ndio imekuwa nongwa? Tulieni hivyo hivyo hii inaitwa kutesa kwa zamu!
 
TataMadiba, Very poor presentation.

Kama wameomba kuonana na viongozi wa dini, ni haki yao. Hakuna shetia iliyovunjwa. Na hakuna wa kuwapangia waonane nao wapi na kwa namna gani.

Tujifunze kutumia akili vizuri. Ilitosha tu kusema wameomba kukutana na viongozi wa dini. Mengine uliyotaandika ni upuuzi mtupu.
 
Wapinzani tulichemka pale tulipoonesha mihemuko na kuanza kuwakashifu Viongozi wa dini, tutakuwa na kazi sana kujisafisha
Sijaona kama kulikuwa na taarifa rasmi ya vyama vya upinzani juu ya viongozi wa dini kukutana na Mh. Rais.

Tuwe na akili, uelewa na werevu pia. Tuwe na uwezo wa kutofautisha kauli ya mtu mmoja mmoja na taarifa rasmi. Mtu mmoja akiwa mwanachama wa chama cha upinzani, akanena neno baya dhidi ya Mh. Rais au kiongozi wa dini haimaanishi kuwa basi chama kile ambacho huyo aliyetoa kauli hiyo ni mwanachama wake, kimetoa kauli.

Mara ngapi wanaCCM wamewasema vibaya viongozi wa dini? Je, maneno yao hayo mabaya ni kauli ya CCM?

Naamini vyama vya upinzani kama wamefanya hivyo, watakuwa wamefanya vizuri zaidi kuliko hata ilivyofanya ofisi ya Rais. Hawa wameziandikia taasisi, na taasisi hizo zitaamua ziwakilishwe na nani. Maana yake watapata nafasi ya kujadiliana na wale wanaounga mkono fikra zao, na wale wanaozipinga. Hiyo itajuwa ni tofauti na ule mkutano wa Rais ambapo kutokana na maelezo ya viongozi wa dini wenyewe, waliohudhuria walichaguliwa watu wanaojulikana kuwa na mlengo wa kuunga mkono chochote kile, kiwe kibaya au kizuri, alimradi kimefanywa na serikali.

Ukitaka kupata maoni ya kweli, usichague watu ili hata na wale wasiokubaliana nawe, nao waje, uwasikie hoja zao.
 
Viongozi wa dini msikubali kukutana na hawa wahuni, na hawana locus maana si watawala, waambieni wahudhurie tu kanisani au misikitini kwenye ibada
Haya ni maoni yako. Bahati mbaya hayawezi kupokelewa kwa sababu viongozi wa dini, wengi wao ni watu wenye akili na busara, siyo rahisi kwao kuchukua ushauri ambao hauna weledi.
 
Wapinzani tulichemka pale tulipoonesha mihemuko na kuanza kuwakashifu Viongozi wa dini, tutakuwa na kazi sana kujisafisha

Ni hivi, viongozi wa dini sio miungu hivyo walikuwa wanakumbushwa wajibu wao wa kukemea maovu. Hakuna barua yoyote ya kiofisi iliyowatusi viongozi wa dini, kama ipo iweke hapa. Na kile walichoambiwa hakitakoma mpaka watimize wajibu wao wa kukemea maovu. Hakuna kiongozi wa dini anayewapangia waumini wake wampigie nani kura kwani kura ni siri.
 
Mmeishiwa propaganda kumhusu lissu sasa mmerudi kwa viongozi wa dini na ukawa. Korosho zimerudishwa kwa wananchi huko kusini, badala ya kumshauri kichaa wenu mmekalia kutunga uongo kila siku
 
Back
Top Bottom