Mkutano wa nchi wanachama wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UNCAC)

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
TAKUKURU.JPG

TAARIFA KWA UMMA

MKUTANO WA NCHI WANACHAMA WA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA (UNCAC)

Katika mkutano wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa yaani ‘Implementation review group meeting to United Nation Convention Against Corruption (UNCAC) unaofanyika Vienna, Austria kuanzia tarehe 20 – 24 Juni, 2016 ; Tanzania imechaguliwa kuwa nchi mojawapo kati ya nchi zitakazofanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkataba huo katika mzunguko wa pili (Second Review Cycle). Tanzania ni mojawapo ya nchi 115 zilizofanikiwa kumaliza ufuatiliaji wa kwanza uliohusisha utekelezaji wa UNCAC Ibara III na IV.

Mzunguko wa pili utahusisha ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkataba wa UNCAC Ibara II na V ambapo nchi ya Tanzania na Bahamas zimechaguliwa kufuatilia utekelezaji wa vifungu hivyo kwa nchi za Trinidad na Tobago. Katika Mzunguko wa kwanza Tanzania ilifanikiwa kufuatilia nchi ya Togo pamoja na Denmak.

Mkutano huu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa unaofanyika nchini Austria Tanzania imewakilishwa na Mhe. Robert Kahendeguza, Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa pamoja na watumishi wawili kutoka TAKUKURU Alfeo Silungwe , Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu na Stanley Luoga, Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa Mkurugenzi Mkuu.

Mafanikio haya ambayo Tanzania inaendelea kuyapata kimataifa ni kutokana dhamira ya dhati ya kupambana na Rushwa na utekelezaji mzuri wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa (UNCAC, 2003) ambapo Tanzania ilisaini Disemba 9, 2003.

IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

21 JUNI, 2016
 
Back
Top Bottom