Mkutano wa 37 wa SADC: Kwaniini Rais Magufuli Amekwepa Kuhudhuria?

Kama mabilion yanamfuata hapa nyumbani kutoka kwa mamilionea na nchi kuu mbalimbali kumsifu kwa kuendesha nchi vizuri kuliko hata hizo nchi zenye exposure nyingi , what else do you need,aende for Tourism? Tayari anawakilishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachia madeni ya Serikali labda na yeye ana madeni yake binafsi anayakimbia huko nje wasije kumkamata yeye.

Tumuache anyooshe nchi kwanza.
 
mimi labda niseme tu kuwa ,kama washauri wa rais wapo ,hadhi yao iwepalepale na wakimshauri jambo afate ,maana ni shida misimamo mingine siyo ,wakiamua kumtenga itakuwaje? mi naamini washauri wapo na wanampqa ushauri unaofaaa ila ni ujeuri wake tu. sidhani kama kubaki ndani tu ni tija
 
Heshima Kwenu,

Kuna Mkutano wa 37 wa SADC, Ushirikiano wa Maendeleo wa Nchi za Kusini mwa Afrika unaoendelea mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.
Wakuu wa nchi mbalimbali wanachama wa umoja huo wanahudhuria.

Ni jambo linaloshangaza na pengine kukera kwa tabia ya Rais wetu, Mh. John Magufuli kukwepa vikao na mikutano ya kimataifa ambayo wakuu wa nchi hualikwa kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo. Vikao hivi ni sehemu ya darasa kwa wakuu wa nchi hujifunza na kubadilishana uzoefu.

Mkutano wa SADC unahusu Afrika na unafanyika Afrika, Rais ana kisingizio gani kukwepa na kumtuma Makamu wake Mh.Mama Samia? Kuna dharura? Kuna hofu ya kupinduliwa?
Halafu tuna bahati kwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC anatoka Tanzania, Mama Stagomena Tax Bamwenda.

Rais anakosa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na marais wenzake kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe hata hujui mkutano unahusu nini. Ulitakiwa ufuatilie ujue agenda kwanza kabla ya kuja na lawama. Mi najua pamoja na issue nyingine kuna kujadili usalama na Tz kukabidhi uenyekiti wa kamati ya usalama kwa Swaziland

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi labda niseme tu kuwa ,kama washauri wa rais wapo ,hadhi yao iwepalepale na wakimshauri jambo afate ,maana ni shida misimamo mingine siyo ,wakiamua kumtenga itakuwaje? mi naamini washauri wapo na wanampqa ushauri unaofaaa ila ni ujeuri wake tu. sidhani kama kubaki ndani tu ni tija
Mkuu sio afate, ni "afuate"

Kadhalika jifunze punctuation. Koma (,) huja baada ya neno na si kabla ya neno

Sasa kama jambo dogo tu hujui, vipi uzungumzie kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wetu kaamua kupambana na wazungu wanyonyaji, kwa kipindi hiki lazima anawindwa, usalama wake unaweza kuwa mashakani katika mazingira kama hayo, tumpe muda amalize mission yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom