Wadau habari...... Ni jambo jema kumsifia mtu kwenye Jamii pale ambapo anakuwa amefanya jambo jema na la manufaa kwa Jamii kwa Ujumla. Katika maisha yangu ya kutumikaa Watanzania nimekuwa kwa karibu sana nikivutiwa na mienendo ya CEOs kadhaa hapa Bongo kwa jinsi walivyozinyanyua Taasisi zao kutoka hatua moja hadi nyingine kuelekea kilele cha mafanikio.
1. Charles Kimei - CRDB, napata faraja kuwa na watendaji wazawa kama huyu wenye mafanikio makubwa katika Taasisi zao. Sote tunajua huyu mzee aliikuta wapi CRDB na sasa wako wapi. Naamini ni mwalimu mzuri na Role mode kwa Vijana wengi wenye nia na kiu ya kuwa Viongozi mahiri wa Taasisi zao.
2. Nehemia Kyando Mchechu - NHC, kwangu mimi pamoja na yote yanayomkabili kwa sasa bado ni hero. Majengo ya NHC miaka saba iliyopita yalikuwa kama majumba ya makumbusho, Uwekezaji mpya ulisita nk nk nk. Lakini mpaka sasa sote tunaiona bendera ya NHC inavyopepea majengo yote yakiwa yamenakshiwa vizuri, miradi mipya yenye mandhari za kuvutia nk nk
3. Mzee Dau - NSSF, ukiweka kando ile kshfa ya udini iliyosemwa sana na wadau ndani ya NSSF hakuna baya jingine ambalo naweza kuwasemea NSSF chini ya Mzee Dau. Uwekezaji wa haja umefanywa na huyu Mzee mfano, UDOM, Kigamboni Bridge nk nk ambavyo kwa hakika vitabaki kuwa Ishara ya kudumu na fahari kwa Taifa zima. Mzee Dau popote ulipo tambua vijana tuliona na tutaiga mema yako yote.
4. ............ Ongezeeni Orodha tuendelee kujifunza kwa wakubwa wetu wadau. ni CEO yupi kwako ni ni mfano wa Kuigwa. Karibuni.