Mkurugenzi wa zamani wa ATCL, David Mattaka apandishwa kizimbani

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,769
22,592
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuisababishia hasara Serikali kupitia ukodishaji wa ndege.

Wakili Mkuu wa Serikali, Timon Vitalis akishirikiana na mawakili wa Takukuru, Joseph Kiula na Stanley Luoga waliwataja washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa ni Ofisa Mtendaji Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Ramadhan Mlinga na Mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka.

Wakili Vitalis alidai kuwa Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL zilizopo wilayani Ilala, Mattaka alitumia vibaya madaraka kwa kutia saini mkataba wa ukodishaji wa ndege A320-214 iliyotengenezwa kwa namba 630 baina ya Wallis Trading Inc na ATCL.

Alidai alifanya hivyo bila ya kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma na taratibu za zabuni kwenye mchakato huo.

Pia, alidai Oktoba 27, 2007 alitumia vibaya madaraka yake kwa kutia saini cheti cha kuruhusu mchakato wa ukodishaji wa ndege hiyo bila ya kufuata ushauri wa kiufundi aliopewa na kuisababishia Serikali hasara ya dola 772,402.08 za Marekani zilizolipwa kwa kampuni ya Aeromantenimiento,S. A kama gharama za huduma ya matengenezo.

Kuhusu Mattaka, wakili huyo alidai Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kumpa dhamana na kwamba, anaweza kuomba kudhaminiwa kupitia Mahakama Kuu.

Washtakiwa Mlinga na Bertha wanadaiwa kuwa Machi 19, 2008 katika ofisi za PPRA walighushi muhtasari wa kikao cha siku ukionyesha mamlaka hiyo ilijadili maombi ya ATCL juu ya kuidhinishwa kwa mkataba huo.

Washtakiwa hao walikubaliwa dhamana kwa kuwa shtaka linalowakabili linadhaminika. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 29.
 
Huyo Mkurugenzi PPRA wanamuonea tuu,Doctor aghushi muhtasari wa kikao haingii akilini.Pia kazi yao ni kutoa ushauri tuu juu ya manunuzi.Bora ingeshtakiwa bodi ya atcl
 
Ati analia.........

Mataka.jpg
 
Dah,kila kona ni wizi mtupu.hivi kwanini serikali inajishughulisha zaidi na kukata matawi badala ikate shina na mizizi yake?maana kuna watu wa ngazi za juu ndo waliobariki wizi huu.
 
Awamu ya wapenda sifa..kama mnamshtaki tu then hatuoni maendelea wala changes zozote kwenye hio kampuni ya atcl basi hakina lolote la maana basi..
 
Huyo Mkurugenzi PPRA wanamuonea tuu,Doctor aghushi muhtasari wa kikao haingii akilini.Pia kazi yao ni kutoa ushauri tuu juu ya manunuzi.Bora ingeshtakiwa bodi ya atcl
Mbona JK ni Prof Mwenye PhD 7 lakini ndilo lijizi lililokubuhu.
 
Wanasiasa nao wakianza kufikishwa mahakamani na kuwajibishwa ndipo nitaamini akifanyacho Magufuli.Maana nafikiri wanasiasa ndo wameneemeka sana na nchi hii kuliko hao watendaji waandamizi.
Duuh, Brother Mlinga pole sana, tunakukumbuka ulivyosimamia Richmond Scandal. Ulionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kusimamia misingi ya manunuzi na kuanianisha hatua kwa hatua jinsi taratibu za manunuzi zilivyokiukwa. Kinachoangaliwa ni soft spot. Yapo madumbwana meengi ya kutisha yaliyofanywa na serikali iliyopita lakini mpaka leo hayaguswi.
 
Back
Top Bottom