Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,231
Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amewakumbusha wanahabari wajibu wao wa kuhakikisha vyama vya siasa na wagombea wanapata nafasi ya kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura katika kipindi cha kampeni.
Aidha, Bw. Kailima amewataka wanahabari kutoa taarifa sahihi kwa umma na kuepuka kusambaza taarifa potofu katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na maadili ya taaluma ya habari.
Kailima ameyasema hayo leo Agosti 2, 2025, jijini Dar es Salaam kwenye kikao kati ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na waandishi wa habari, ikiwa ni muendelezo wa vikao vyao na wadau wa uchaguzi nchini.
Amewahimiza waandishi hao kutumia kalamu na nyenzo zao kueneza ujumbe wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ili kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha misingi ya demokrasia.
Pia amewaasa kuepuka kuchapisha au kurusha habari zinazoweza kuwavunja moyo wananchi na kuwafanya waone kama hakuna umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi, iwe ni kama wapiga kura au wagombea.