Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ajikita Katika kuboresha Elimu

kwedikwazu

Member
Dec 17, 2016
18
15
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia amezindua na kukabidhi vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Murriet sambamba na kukabidhi madawati zaidi ya 100 Katika Shule hiyo.

Katika Hafla hiyo Ndg. Kihamia amesema lengo la Halmashauri ni kuboresha utoaji wa Elimu Msingi ili kuleta matokea Chanya katika ufaulu na kujenga
Misingi Imara ya watoto wa Jiji la Arusha.

"Tumekwishamaliza changamoto ya madawati na sasa tumeanza na vyumba vya madarasa hatutaki kuona watoto wanalundikana Katika vyumba vya madarasa, idadi ya wanafunzi Katika Chumba iwe kwa Mujibu wa muongozo na si vinginevyo na tutaendelea kujenga vyumba hivi Katika Shule zote zenye upungufu" Aliongeza Kihamia.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongizi wa Kata na Mtaa, bodi ya Shule pamoja na wazee wa Kimila Kaimu Afisa Elimu Msingi Bi. Eunice Tondi amesema zaidi ya wanafunzi zaidi ya 200 watanufaika na madarasa hayo kufuatia changamoto ya kukosa vyumba vya madarasa hali iliyopelekea wanafunzi kupokezana wengine kuingia darasani asubuhi na wengine mchana na upatikanaji wa madarasa hayo utaongeza ubora wa Elimu na bila Shaka kuongeza kiwango cha ufaulu.

Vyumba hivyo vilivyogharimu zaidi ya Tsh Mil 110 vimejengwa ili kukabiliana na changamoto ya Uhaba wa vyumba vya madarasa na chanzo cha Fedha ni kutoka Katika Mapato ya ndani.
27732bd837904691cba8ee4f46354eca.jpg
dc22de2e5cd3ce4464d072d4e4c017d0.jpg
ef6c7bf773be984d653ff1bcb8ebb020.jpg
528bf8f227b735b44f98b399da12a101.jpg
 
Ni jambo jema,ila wakafikirie namna ya kuongeza masilahi ya waalimu pia,kujaza madawati na kujenga madarasa pekee haitoshi kuboresha elimu.
 
Back
Top Bottom