Mkurugenzi Mwanza anusurika kipigo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,251
2,000
VURUGU zimeibuka katika kikao baina ya Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na wafanyabiashara wanaodai kupandishiwa kwa kiwango cha kodi ilihali biashara zao haziendi vizuri,

Wafanyabiashara hao ambao walifika katika ofisi za jiji leo saa asubuhi, wakiongozwa na Hamad Nchora, mwenyekiti wao kwa lengo la kufanya mazungumzo na mkurugenzi huyo kuhusu ongezeko la kodi la vyumba vya maduka yao.

Wafanyabiashara hao hufanya kazi zao Soko kuu, Makoroboi na Sahara waliingia katika ukumbi wa jiji kwa ajili ya mazungumzo kufuatia bei ya pango ya sasa ni Sh. 200,000/= kwa maduka ya ndani na 250,000/= kwa maduka ya nje. Mazungumzo ambayo yalitawaliwa na mabishano makali.

Wafanyabiashara hao walidai kwamba bei inayoelekezwa na mkurugenzi huyo ya Sh. 300,000/= maduka ya ndani na Sh. 417,000/= kwa maduka ya nje katika soko hilo si halali kwani biashara kwa sasa sio nzuri.

Walidai mikataba yao inatarajiwa kuisha Julai 2017 lakini mkurugenzi wa jiji hilo ameisimamisha kwa madai kuwa faida wanayoipata wafanyabiashara hao ni kubwa ikilinganishwa na fedha inapelekwa jiji.

Msimamo huo wa mkurugenzi dhidi ya wafanyabiashara uliibua vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya dakika 10 huku wengi wakitoka nje kwa hasira huku wakitupia maneno makali na kumnyooshea kidole Kibamba.

“Kesho utatuona airport (uwanja wa ndege Mwanza), wewe mkurugenzi unafanya siasa na maisha ya watu,” walifoka kwa hasira wafanyabiashara hao.

Kibamba aliwasihi wafanyabiashara hao kutulia na kurudi ndani ya ukumbi ili majadiliano yaendelee ambapo baadhi walikubali kurudi na mkurugenzi huyo kuwaangukia akisema;

“Nendeni mkaedelee na biashara zenu mpaka Julai 2017 lakini muda huo ukifika bei iliopangwa itabaki kama ilivyo, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali alifanya uchunguzi na kubaini sisi tunapoteza fedha nyingi kwenye maduka yetu ya Soko kuu na Sahara hivyo lazima tudhibiti upotevu huo wa mapato.”

Hamad Nchora, mwenyekiti wa wafanyabiashara hao amesema hatua zilizochukuliwa na mkurugenzi huyo kuwaacha waendelee mpaka Julai mwakani ni nzuri na wafanyabiashara wameridhia na kwamba muda huo ukifika watakaa na kuangalia kufanya.


Chanzo: Mwanahalisi Online
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,562
2,000
Kwani rais bado hajatoa tamko leo..Mkurugenzi kua makini hao watu wa Mwanza wapo ofisi kuu shauri yako
 

Nzingambemba

Member
Dec 10, 2016
75
125
contingency is inevitable when the condition is worse busara hushinda nguvu ni vema mkulugenzi umeliona hilo na kufikia consensus. Sote tunania ya kujenga nchi yetu moja
 

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Kesho JPM yuko mwanza akielekea mapumzikoni chato,
Atafungua daraja na TFDA nyakato

Mkurugenzi aangalie kodi yake,asiangalie faida ya mfanyabiashara
 

Kikinga

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
1,285
2,000
KAMA BEI HIZO NI KWA MWEZI, NI KWELI BEI KUBWA LAKINI KAMA NI KWA MWAKA, AAAAAAAAA!!! JAMAAAAANI NI PESA NDOGO SANA HIYO, HAPO KAZI TU MBELE KWA MBELE.
 

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,230
2,000
Uyo DED hana kazi watu wa kanda Hile si watu wamchezo mchezo awamu hii wako secured na Mkulu
Kama machinga wanawafnya watu wafanye kazi kwa hofu je hao Walipa kodi.......?
 

Salamanders

JF-Expert Member
Oct 31, 2016
365
250
Serikali makini na Djibouti ni ile inayokusanya kodi. Ndicho tunachotekeleza hakuna namna. Hapa Kazi tu. Bora punda afe lkn mzigo ufike.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom