Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Siha, hili la Mh Claudia Muro limekaaje

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,493
2,000
Wilaya ya Siha ni moja ya wilaya mpya nchini, iliyo gawanywa toka wilaya mama ya Hai.

Moja ya chanzo cha mapato yar Halmashauri ya Siha ni mashamba ya Narco ambayo Halmashauri imeyarithi toka Narco.

Kwa kutambua umuhimu wa ardhi na matumizi yake, halmashauri ya wilaya ya Siha iliazimia kuyagawa mashamba hayo kwa wananchi kwa maana ya kuyakodisha kwa wananchi ambao ni wakulima.

Nimpongeze sana Mkurugenzi na uongozi mzima wa wilaya hii kwa kujua thamani ya ardhi kwa wananchi kutokana na uhaba wa ardhi, ambayo ni changamoto kwa wananchi hawa.

Kila jambo lina changamoto zake, lakini kwa hili la ukodishaji ardhi, changamoto yake ni kubwa sana.

Kwanini changamoto ni kubwa;

Ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya ardhi, iliratibu zoezi zima la ukodishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba kwa mkataba wa muda mfupi (season contract)

Lakini zoezi hili limekuwa na utata mkubwa sana kutokana na tamko la mwenyekiti wa CCM Taifa kuwataka wana CCM kuisimamia serikali.

Utata huo una gubikwa na uingiliaji wa ugawaji wa maeneo ya kilimo yanayo fanywa na Mh. Diwani wa viti maalumu kutoka Karansi kupitia CCM.

Tatizo si ugawaji, wananchi wanagaiwa maeneo hayo baada ya kulipia 40,000/ kwa Acre na kupewa risiti ya malipo halali ya ardhi kwa matumizi ya ardhi kwa msimu wa kilimo, lakini mh. Cláudia Muro akitumia mwamvuli wa udiwani, amekuwa akiingilia maeneo hayo na kuyagawa kwa watu wasio kidhi vigezo, kwa maana ya waliokodishiwa na kupewa uhalali wa umiliki wa muda mfupi kwa msimu wa kilimo.

Hali hii imesababisha utata mkubwa na mwingiliano unao sababisha chuki miongoni mwa wakulima kugombania maeneo ambayo wamekwisha kuyalipia kihalali.

Kwa sakata hili nashauri yafuatayo:

Nilitake baraza la madiwani kuhoji uhalali wa madam Cláudia kuingilia mchakato wa ugawaji mashamba bila idhini ya vikao halali.

Ni muhimu Mh. Huyu kulipa fidia ya usumbufu kwa wananchi alio wanyang'anywa ardhi na kuikodishia kwa bei ya ulanguzi inayo pingana na bei elekezi iliyo pangwa na halmashauri.

Ajiuzuru kwa kuwa amekiuka taratibu na kanuni za maadili ya utumishi wa umma.

Mwisho, lazima kuwepo mipaka ya kiutendaji kuepusha mwingiliano usio na tija.
 

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
6,396
2,000
Ukimuona huyo diwani mwambie hivi asiingilie kazi isiyo muhusu, asiwachonganishe raia maana huo Ni uchochezi, mwambie asubirie mafao ya udiwani na sio kuwa dalali wa mashamba ya serikali...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom