Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini: REA haijawahi kupata fedha za MCC

dadoliz

Member
Jul 27, 2015
59
40
Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania

MCC.png



Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REA‘ Lutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo

‘REA haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya fedha zote tunazofanyia kazi na hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’

’Shughuli za REA haziwezi kusimama na Serikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’

Chanzo:
MillardAyo
 
Hiyo 10% mbona hasemi inatoka kwa wahisani gani?!
Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania

MCC.png



Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REA‘ Lutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya fedha zote tunazofanyia kazi na hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’

>>>’Shughuli za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.

Source: Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania - TZA_MillardAyo


Asante mama kwa ufafanuzi, nadhani tuvute subira hii MCC itakuja kuwa ni JIPU LILILOJIFICHA na pesa zilikuwa zinaliwa na wachache, KAMUA MJOMBA MAGUFULI inawezekana una taarifa sahihi za fedha za wahisani kuwa zilikuwa zikiliwa na wachache matokeo yake wanaishia kukopa kwenye mabenk ya kibiashara ili kuwaziba midomo wahisani. Hapa naanza kunusa kitu tuvute subira. Wapi pesa ya MCC ilikuwa inaenda??????? ndiyo maana watu kila kukicha Marekaniiiiiii
 
Hili suala linahitaji busara sana.Kujifanya kujibu kila kitu bila busara haitatusaidia.Ni heri ya Dr.Maiga alilalamika kidiplomasia .
 
Kinachoniumiza mimi nchi imekuwa ikikopa sana, eti miradi ya maendeleo, misaada tumepokea sana eti wahisani wa maendeleo.Hayo maendeleo yako wapi???.Mwisho tumeachiwa deni la 40trilion
Sasa na hii ya MCC inakanushwa kuwa haijatumika kwa maendeleo ya umeme vijijini. Wapi gereza la Kunyonga wahujumu uchumi????

Nimeamini Magufuli ni Geneus and a good scientist
 
Kama hizo hela zilikuwa hazisaidii REA basi endeleeni kusambaza umeme vijijini, ila mbele ya safari tusianze kusikia mara Serikali inajipanga!
 
Wakala wa nishati vijini REA wamesema hawajawahi kupata pesa za shirika la MCC la Marekani lililokatisha msaada wa Trilioni moja kwa Tanzanihivyo haitowaathiri.
 
mabango ya umeme wa MCC mbona yamejaa huku mitaani alafu huyu afsa analonga NN??
 
Safi kabisa tutasimama kwa miguu yetu na kufanya kazi kwa mikono yetu. Serikali ya magufuli ina mission na vission ya kututoa kuwa omba na tegemezi. Wanaodhani tutaathirika kwa mcc imekula kwao kwa uvivu wao wa kufikiri na kuchapa kazi.
 
Back
Top Bottom