Mkurugenzi atishia kumshitaki mahakamani DC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi atishia kumshitaki mahakamani DC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 2, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKURUGENZI Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, Ephrem Kalimalwendo, ametangaza kumburuza mahakamani mkuu wa wilaya hiyo, Halima Dendego kwa madai kuwa, amemzulia tuhuma za uongo za kununua Power Tillers zenye thamani ya Sh milioni 225 ambazo hazina ubora.

  Kalimalwendo amempa siku 21 DC huyo kutoa vielelezo vya namna alivyohusika kwenye ununuzi wa power tillers hizo na iwapo atashindwa kufanya hivyo, atalazimika kujisafisha kwa kutumia vyombo vya sheria.

  Amesema, atafanya hivyo kwa kuwa taarifa hizo ni nzito na zimemwaibisha na kumvunjia heshima mbele ya umma wa Watanzania hadi nje ya nchi.

  Dendego alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi ili kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma alizozitoa dhidi ya DED wake, ilikuwa imefungwa muda wote.

  Akifafanua juu ya tuhuma hizo, Kalimalwendo alisema Aprili 13, mwaka huu DC Dendego alitoa tuhuma za yeye (DED) kwa kushirikiana na watumishi wengine waliingia mkataba wa kununua power tillers 50 kutoka kwa Kampuni ya Millystel Distributors ya Dar es Salaam kwa bei ya Sh milioni 4.5 kila moja.

  Anadaiwa kusema kuwa power tillers zilizonunuliwa hazina ubora, zinafifia rangi na baadhi ya vifaa havikuwepo, kitendo kilicholeta kasoro katika vifaa hivyo na kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

  “Kwa kauli yake, Dendego aliagiza mimi na watumishi wengine tukamatwe na kufunguliwa kesi ya wizi na taarifa hizi zilitangazwa na vyombo vya habari,” alisema Kalimalwendo.

  Amesema, alipokea taarifa hizo kwa masikitiko kwa sababu hahusiki na chochote katika ununuzi wa power tillers hizo. Alikiri halmashauri hiyo kuingia mkataba na kampuni hiyo wa ununuzi wa matrekta hayo 50.

  Alisema Kampuni ya Millystel Distributors ilishinda zabuni kihalali kwa vigezo vyote vilivyopo kwenye Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 na kanuni zake ilizingatiwa.

  Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia masharti ya mkataba, halmashauri yake ililazimika kuvunja mikataba yote miwili na yeye Kalimalwendo kwa nafasi yake kama DED, alilazimika kutekeleza hilo kwa barua ili kutoa fursa ya kupata mzabuni mwingine.

  Alisema kuanzia Novemba 3, 2010 alilazimika kuwa nje ya ofisi na alifanya makabidhiano yote kama inavyotakiwa. Licha ya kuwa hakueleza alikoenda, lakini DED huyo alienda kugombea ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Rukwa.

  Alisema akiwa ameondoka ofisini, nyuma yake kwa taarifa alizozipata Kampuni ya Millystel Distributors ilipeleka matrekta hayo.

  “Utaratibu uliotumika siujui kwani mimi niliishia hatua ya kuvunja mkataba na kukabidhi ofisi,” alieleza.

  Hivyo alisema anashindwa kuelewa namna alivyohusishwa na mchakato wa ununuzi wa matrekta hayo na kwa nini DC amwite mwizi na kumtangaza kwenye vyombo vya habari wakati hakuhusika na ununuzi huo.
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kama kweli ana uhakika kuwa hakufanya hayo manunuzi,na kwa kuwa vyombo vya habari vilimchafua kwanini atoe siku zote hizo? au anataka wayamalize kishikaji? kwanini kama kachafuliwa asitoe angalau siku 3-7 na baada ya hapo ampeleke Mahakamani haraka iwezekanavyo.
   
 3. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  well said hata mimi hof yangu ni hiyo hiyo, zinaweza kupita hizo siku 21, then akaibua sababu nyingine za kuongeza siku ili mambo yaishe kinyemela
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  zikiisha wataongeza tena ndio mtindo wao hawa kwanza wataitwa na kukalishwa chini kimyakimya
   
 5. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  jamani hivi kauli hii
  Alisema Kampuni ya Millystel Distributors ilishinda zabuni kihalali kwa vigezo vyote vilivyopo kwenye Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 na kanuni zake ilizingatiwa
  na hii

  Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia masharti ya mkataba, halmashauri yake ililazimika kuvunja mikataba yote miwili na yeye Kalimalwendo kwa nafasi yake kama DED, alilazimika kutekeleza hilo kwa barua ili kutoa fursa ya kupata mzabuni mwingine.

  mbona haziko wazi sana? kama walishinda kwa vigezo vyote, kwa nini wavunje kwa kuzingatia masharti ya mkataba, angeanza kufunguka hapo tungeelewa ukweli
   
Loading...