tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,008
- 1,955
Jana kuna wanajeshi kutoka Nigeria walitembela TBC..(nimefupisha).)nilimshangaa mkurugenzi (A. Rioba) aliposema kuwa Watanzania wana utamaduni wa kubeza kila kitu, akataja taja vitu vinavyobezwa na Wa TZ, lengo la kauli zake ilikuwa ni kuutarifu umma kuwa wa nje (wa nigeria) wanathamini vyetu ila sisi hatufanyi hivyo sasa Mh Rioba, si kweli kwamba sisi tunabeza vya kwetu kama ulivyo uaminisha umma na wageni waliokuwamo studio, ukweli unajua ni kwanini Watanzania wanabeza vya kwetu hasa TBC ila unajitoa ufahamu tu,
TBC kwanza unapaswa ujue kuwa si chombo cha mtu binafsi bali ni chombo cha jamii nzima ya Watanzania, 1) ila chombo hiki kimefanywa kuwa chombo cha watu binafsi haswa CCM, 2)Taarifa zinalala upande mmoja kana kwamba wote tuko mlengo mmoja, tanzania inavyama vya siasa kibao, madhebu mengi, makabila kibao, watu wenye sura,itikadi tofauti tofauti nk ila habari za CCM tu ndo hupewa kipau mbele, itikadi fulanifulani ndizo upewa kipaumbele n.k
3) Usomaji wa taarifa za habari ni wa ajabu sana, taarifa inapitiwa juu tu, igeni mifano ITV na AZAM tv, taarifa haichambuliwi walau kidogo, taarifa kama vile mnasoma mhutasari tu,
4) Ubora wa muonekano, hapa TBC sijui kinakosa kitu gani, haiwezekani TV za mtu/watu binafsi wakawa na uwezo wa kuwa na Technolojia nzuri kuliko serikali hili haliwezekani bali hapa kuna udhaifu wa makusudi.
3 asilimia 99.99% ya taarifa na makala pia na mijadala za TBC yetu zinalenga kusifia tu! Huu si weledi bali ni udhaifu, si maanishi lazima mpinge ila walua tumieni taaluma zetu vizuri. Kwa hali hii ni Mtanzania gani ataweza kuisifia TBC? Jaribuni walau kufuatilia TV za watu binafsi hapa TZ kama Azam na ITv.
Mbona taarifa za Kimataifa mnazichota kule Al Jazeera zinakuwa na ka mvuto kidogo? walau mtakuwa na la kujifunza, aidha usiwashangae Wa TZ kususa na kuibeza hii Tv maana inawauma kwani ni TV ya Watanzania wote ila mmeigeuza kama ya mtu binafsi, hata CHANNEL TEN, inafanya hovyo tu ila hiyo hatuwezi kusumbuka nayo maana si mali ya umma ni mali za watu binafsi. Vilevile kwa kuwa wewe unaweza kufikisha ujumbe kwa wakubwa washaurini CCM km inawezekana wafungue TV yao, watuachie TBC yetu, pia km mmeshindwa ku balance taarifa zenu ni bora baadhi ya mambo kama ya siasa za CHADEMA ,CCM, CUF nk zisitangazwe humo.
Natamani hii TV yetu ifanye vizuri kuliko zote na huu ndo uzalendo uanohitaji Mh Rais. Najua Mkurugenzi Rioba we ni member wa Jf utapata ujumbe huu na hata usipoupata kuna watumishi wa TBC wataupata, jitahidi walau baadhi ya mapungufu yapungue ili na sisi Watanzania tutembee kifua mbele tukijivunia TBC maana mimi ni mdau mzuri sana wa TBC wala siigizi kwanini tuzidwe na RTV?
Kwanini tuzidiwe na MBC? Kwanini KBC Ituzid? yaani TBC inafanana karibiana na UBC na ZBC 2, tu basi.