Mkumbuke Mungu siku ya tabu yako

Mkumbuke Mungu siku ya tabu yako

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Yon 2:7 SUV
[7] Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

Sisemi siku nyingine tukiwa katika raha tusimkumbuke Mungu wetu, ninachomaanisha hapa ni kwamba hata ile siku ya tabu yako kumbukumbu zako zisije zikafikiria kutafuta msaada sehemu nyingine nje na Mungu.

Yona anasema roho yake ilipozimia, alimkumbuka Mungu wake, hii inaonyesha vile tunapaswa kufanya pale tunapokutana na shida/changamoto yeyote ile.

Tunapokutana na mambo magumu, tunapaswa kuelekeza maombi yetu kwa MUNGU, na hupaswi kuzimia moyo wako katika mapito yako.

Usikate tamaa mpaka ukafika mahali ukaona Mungu hana msaada kwako, hata kama unaona kila kitu kimeanguka, mkimbilie Mungu ndiye ana jawabu lako.

Imani yako haipaswi kutoka kwa Mungu, bila kujalisha uzito wa jambo unalopitia au lililokupata, endelea kusimama imara katika BWANA.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
🫡
 
Nice message... Naomba mstari ule wa ZABURI YA 39 na unipe mstari unaosema "mkumbuke Mungu siku za ujana wako...."
Zaburi : 39 : 1 - Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.

Mhubiri : 12 : 1 - Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
 
Ubarikiwe mama mchungaji wangu😎😎
 
Yer 17:5 SUV
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mchungaji mmoja alianzisha huduma yake katika moja ya vijiji(Ukerewe)..eneo hilo lilikuwa na nguvu za giza kwa kiasi kikubwa na idadi kubwa ya washirikina.

Huduma yake ikafanikiwa kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwafungua wengi waliofungwa na vifungo vy kishirikina uchawi..akapata waumini wengi sana kanisa likaendelea kukua kila siku na idadi ya waumini kuongezeka kila uchwao.

Washirikina wa eneo hilo wakapata pigo kubwa maana wanakijiji wengi waliponywa.

washirikina hao hawakufurahi wakaweka kikao wakamtengenezea UGONJWA wa kansa...wakamtupia ukampata..

Na Mungu aliruhusu hilo jaribu limpate kama ilivyokuwa kwa AYUBU wa kwenye biblia (Jaribu ni mtaji wa kuongeza imani)
Mungu hataruhusu jaribu lililo nje au juu ya uwezo wa mwanadamu,majaribu tinayopata ni yale ambayo ni ya kawaida kwa mwanadamu,na Mungu huwa anaweka na njia za kutokapo,mlango wa kutokea kwenye hilo jaribu..

Sasa mchungaji yule alipopata huo uginjwa wa KANSA alipokwenda hospitali madokta wakamwambia huu ugonjwa hauponi hauna tiba hospitali..

Mchungaji akahuzunika sana akakata tamaa ,akamkasirikia Mungu...akasema yani Mungu umeruhusu huu ugonjwa wa kansa unipate mimi mtumishi wako pamoja na kikutumikia kwa kiasi hiki chote..kujitoa kwangu kote ..kufanya kazi yako ina maana huioni ..ndio ukaamua ukubali nipate huu ugonjwa...akamchukia sana Mungu..

Katika wale wachawi mmoja wapo ni mtu wake wa karibu kanisani..

Akamfuata mchungaji akamahauri...kama hospitali wamwshindwa kukutibu..jaribu nikupeleke kwa MTAALAMU anaweza kukuponya kama huko kwingine wameshindwa ...

Mcgungaji akamkasirikia Yesu akasema ..Kama wewe Yesu umeruhusu niumwe basi ..acha nijarubu kwingine..

Akaenda kwa mtaalamu sangoma mganga wa kienyeji..ambaye naye ni mshirikina ..ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu kwakua ..kanisa lake na maombi ya kanisa lake yalikuwa yanaleta uharibifu mkubwa katika kuathiri nguvu zao na mambo yao ya kishirikina ..alikuwa maombi ya walokole yanavuruga na kuharibu kabisa kazi zao za kishirikina..

Siku ya nne tu toka aende kwa mtaalamu mchungaji akafariki..
 
Attachments

  • images - 2026-03-09T191936.340.jpeg
    images - 2026-03-09T191936.340.jpeg
    13.9 KB · Views: 3
Mungu ni Mwaminifu: 1 Wakorintho 10:13 inasisitiza kuwa Mungu hataacha ujaribiwe kupita uwezo wako, bali atafanya mlango wa kutokea.

Yer 17:5 SUV
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mchungaji mmoja alianzisha huduma yake katika moja ya vijiji(Ukerewe)..eneo hilo lilikuwa na nguvu za giza kwa kiasi kikubwa na idadi kubwa ya washirikina.

Huduma yake ikafanikiwa kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwafungua wengi waliofungwa na vifungo vy kishirikina uchawi..akapata waumini wengi sana kanisa likaendelea kukua kila siku na idadi ya waumini kuongezeka kila uchwao.

Washirikina wa eneo hilo wakapata pigo kubwa maana wanakijiji wengi waliponywa.

washirikina hao hawakufurahi wakaweka kikao wakamtengenezea UGONJWA wa kansa...wakamtupia ukampata..

Na Mungu aliruhusu hilo jaribu limpate kama ilivyokuwa kwa AYUBU wa kwenye biblia (Jaribu ni mtaji wa kuongeza imani)
Mungu hataruhusu jaribu lililo nje au juu ya uwezo wa mwanadamu,majaribu tinayopata ni yale ambayo ni ya kawaida kwa mwanadamu,na Mungu huwa anaweka na njia za kutokapo,mlango wa kutokea kwenye hilo jaribu..

Sasa mchungaji yule alipopata huo uginjwa wa KANSA alipokwenda hospitali madokta wakamwambia huu ugonjwa hauponi hauna tiba hospitali..

Mchungaji akahuzunika sana akakata tamaa ,akamkasirikia Mungu...akasema yani Mungu umeruhusu huu ugonjwa wa kansa unipate mimi mtumishi wako pamoja na kikutumikia kwa kiasi hiki chote..kujitoa kwangu kote ..kufanya kazi yako ina maana huioni ..ndio ukaamua ukubali nipate huu ugonjwa...akamchukia sana Mungu..

Katika wale wachawi mmoja wapo ni mtu wake wa karibu kanisani..

Akamfuata mchungaji akamahauri...kama hospitali wamwshindwa kukutibu..jaribu nikupeleke kwa MTAALAMU anaweza kukuponya kama huko kwingine wameshindwa ...

Mcgungaji akamkasirikia Yesu akasema ..Kama wewe Yesu umeruhusu niumwe basi ..acha nijarubu kwingine..

Akaenda kwa mtaalamu sangoma mganga wa kienyeji..ambaye naye ni mshirikina ..ambaye alikuwa anamsubiri kwa hamu kwakua ..kanisa lake na maombi ya kanisa lake yalikuwa yanaleta uharibifu mkubwa katika kuathiri nguvu zao na mambo yao ya kishirikina ..alikuwa maombi ya walokole yanavuruga na kuharibu kabisa kazi zao za kishirikina..

Siku ya nne tu toka aende kwa mtaalamu mchungaji akafariki..
Yakobo 1:2-18
Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote

1 Kor 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Mwanzo 22:1-2 ”Ikawa baada ya mambo hayo MUNGU alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

Mathayo 24:13 ” Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”

Zaburi 11:5 ‘’BWANA humjaribu mweyehaki Bali nafsi yake humchukia asiye haki na mwenye udhalimu’’
Jaribu la MUNGU ni kipimo tu cha MUNGU kama kweli unampenda.

AYUBU ALIJARIBIWA AYUBU NI MFANO BORA WA MWANADAMU ALIYESTAHIMILI MAJARIBU NANKUSHINDA ...soma kitabu cha AYUBU katika biblia.
 
Mathayo 11:28 SRUVDC
Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

1 Petro 5:7
Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.
 
Attachments

  • Screenshot_20260324-113242.jpg
    Screenshot_20260324-113242.jpg
    75.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom