Mkulo: Uchumi unazidi kukua

Duuh siyo mchezo....kuna hadithi niliwahi kuisikia ya miaka ile ya kilimo cha kufa na kupona. Kuna kabila moja walipoambiwa wapanue mashamba na uzalishaji, wao wakaongeza kupanua masikio yao kwa ajiri ya kuongeza urembo. Pengine labda uchumi unakua kwenye mashavu ya baadhi ya watu na siyo uchumi wa nchi. Who knows kama kila asubuhi mashavu yanazidi kunona!!!
 
Mkulo apigwa kombora (Nipashe)


  • Aambiwa kazi imemshinda ajiuzulu
  • Ni ndani ya kamati ya Fedha na Uchumi
  • Wamwambia uchumi wa nchi uko hoi

Wabunge wameibana serikali kuhusu taarifa yake ya hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2009 na mwelekeo katika kipindi cha muda wa kati (2010/11-2012/13), kwa madai ya kuwa na mipango mizuri isiyotekelezeka, huku baadhi yao wakitaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kujiuzulu iwapo ameshindwa kusimamia uchumi wa nchi.

Kauli ya kutaka Waziri Mkulo aachie ngazi na kukaa pembeni, ilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Devota Likokola (CCM), alipokuwa akichangia hoja katika mjadala kuhusu taarifa hiyo ya serikali.


Taarifa hiyo ilisomwa na Mkulo katika kikao kati ya viongozi, watendaji na wataalamu wa wizara hiyo na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.Iligusia malengo ambayo serikali ilijiwekea mwaka jana kwa kuzingatia athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia na maeneo ya vipaumbele kitaifa kwa kuwekeza katika shughuli za kiuchumi na kijamii zinazoweza kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa mapana zaidi katika muda wa kati wa mwaka wa fedha wa 2010/2011 hadi 2012/2013.


Katika mchango wake kuhusu taarifa hiyo ya serikali, Likokola alihoji sababu za kutokuwapo kwa utekelezaji katika mipango mizuri inayowekwa na serikali na kusababisha kubaki kwenye makaratasi.“Kama kuna wataalamu, ambao hawasimamii ipasavyo utekelezaji wa mipango mizuri ya serikali, basi wawajibike, hata kama waziri atakuwa ameshindwa kusimamia uchumi akae pembeni,” alisema Likokola.


Kauli hiyo ilirejewa na Mbunge wa Morogoro Mjini, Dk. Omari Mzeru (CCM), wakati akichangia hoja kuhusu taarifa hiyo ya serikali, ambaye alisema: “Tatizo la Watanzania, tunaandika vizuri, lakini hakuna utekelezaji.”Likokola alisema kumekuwa na ubaguzi katika umiliki wa uchumi nchini, ambapo wageni, ndio wanaomiliki uchumi peke yao na kuhoji:

“Inakuwaje Watanzania halisi wasimiliki uchumi, badala yake wamiliki Watanzania weupe peke yao kama Mheshimiwa (Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Harry) Kitillya?”

Pia, alisema licha ya kuwapo kwa Mpango wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na za Umma (PPP), sekta binafsi na zisizo rasmi, zimekuwa zikitengwa na serikali katika ukuzaji wa uchumi licha ya kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

“Hivi PPP ni kitu gani? Kiko kwenye makaratasi, lakini kwenye utekelezaji hakipo,” alisema Likokola na kumtaka Waziri Mkulo akamuulize Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ili amweleze namna PPP inavyotekelezeka India.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema serikali imekuwa ikiweka mipango mizuri ya kukuza uchumi, lakini viwanda vingi vilivyobinafsishwa, ama vimekufa au vinafanya kazi chini ya kiwango.

“Kwa mfano, Morogoro kulikuwa na viwanda 38, leo havifiki hata saba. Kwanini tumefika hapa? Tatizo miundo tunayo, lakini hatuna mbinu. Sasa lazima tutekeleza wenyewe yale tuliyokubaliana,” alisema Ndassa.Alisema miongoni mwa vikwazo vya kukua uchumi, ni pamoja na kuwapo kwa matumizi makubwa katika ofisi ya waziri. Hata hivyo, hakutaja takwimu za matumizi hayo ya ofisi ya waziri.“Pamoja na hayo, matumizi ya waziri ni makubwa, ni balaa. Unakula fedha za ndani na za wafadhili. Matokeo yake hupeleki fedha kwenye shughuli za maendeleo,” alisema Ndassa.


Sababu nyingine, alisema ni ukosefu wa umeme wa uhakika viwandani na msongamano wa magari uliokithiri, hususan katika jiji la Dar es Salaam, ambao unatishia kudumaza utendaji makazini.Alisema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti tatizo la msongamano wa magari, itafika wakati watu watafika makazini saa 5 asubuhi na kufika majumbani baada ya kazi saa 4 za usiku na kwamba, wenye magari watakuwa wanaegesha magari yao barabarani.


Kutokana na hali hiyo, aliishauri TRA kuongeza kasi ya kukagua magari yanayoingia nchini ili kujua kama yana uhalali au la na kuwekwa utaratibu kwa yeyote anayetaka kuegesha gari katika maeneo ya mjini, kutozwa Sh. 5,000, ikiwa ni njia mbadala ya kudhibiti hali ya msongamano wa magari mijini.


Mbunge wa Mwibara, Charles Kajege (CCM), alishauri kupigwa marufuku uingizaji wa mafuta ya kula kutoka nchini Malaysia kwa vile wazalishaji wa ndani wanashindwa kushindana katika soko kutokana na mafuta yanayotoka nje ya nchi kuuzwa kwa bei ndogo.


Naye Dk. Mzeru alilaumu ripoti ya msajili wa viwanda, ambayo ilikitaja kiwanda cha zamani cha mafuta ya kula cha Moproco cha mkoani Morogoro kuwamo katika orodha ya viwanda vinavyofanya kazi wakati hakifanyi kazi tangu mwaka 2004.“Mimi ningekuwa rais wa nchi ningekuwa nimeshamfukuza kazi, kwa sababu hii kama si rushwa ni nini?” alihoji Dk. Mzeru.Kiwanda hicho kinamilikiwa na mfanyabishara na mwanasiasa, Aziz Abood, ambaye anatajwa kuwa katika mkakati wa kuwania jimbo la Morogoro Mjini analoshikilia Dk. Mzeru.

Dk. Mzeru alisema kumekuwa na madai kwamba Moproco imeshindwa kujiendesha kwa sababu ya kodi kubwa.

Mwenyekiti wa kikao cha jana, Hamza Mwenegoha, alishauri kuundwa kwa kamati ndogo kupata maelezo kutoka Moproco juu ya madai ya kodi kubwa ambayo imewafanya washindwe kuendelea na uzalishaji.


Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega, alisema serikali imekuwa na tabia ya kutotumia vyanzo vyake vyote vya mapato. Alitoa mfano wa mkoa wa Kilimanjaro ambao una vyanzo 317 lakini ni vitano tu vinatambulika.


Akijibu hoja hizo, Waziri Mkulo alisema baadhi ya hoja zinagusa sera, hivyo zitafanyiwa kazi na nyingine aliwaruhusu wataalamu wa wizara kuzijibu katika kikao cha jana.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Enos Bukuku, akijibu hoja ya Likokola kuhusu kutoshirikishwa kwa sekta binafsi na zisizo rasmi, alisema ziko kwenye maeneo maalum, hivyo kama kutakuwa na faida au hasara, wanaonufaika ni wale, ambao wako katika eneo husika iliko sekta binafsi.

Kuhusu mfumko wa bei, Bukuku alisema BoT inafanya kila mbinu kuhakikisha hali hiyo inaondoka; aliainisha baadhi ya hatua kuwa ni kupunguza fedha zilizoko kwenye mzunguko, kwamba ifikapo mwisho wa mwezi ujao mfumuko wa bei utakuwa umerejea chini.Awali Waziri Mkulo alisema maeneo ya kipaumbele ya kitaifa kwa sasa ni pamoja na kilimo na maendeleo ya mifugo na uvuvi; miundombinu; uendelezaji wa ardhi na makazi; vitambulisho vya kitaifa; nishati; viwanda na sekta za fedha.


Waziri Mkulo alisema sekta ya kijamii (elimu, afya na maji), zitaendelea kupewa umuhimu katika mgawo wa fedha. Alisema kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu hivyo kipaumbele cha kipekee kitazingatiwa ili kuhakikisha kuwa unafanyika kama ulivyopangwa.

Awali, aliyataja malengo, ambayo serikali ilijiwekea mwaka jana kwa kuzingatia zaidi athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kuwa ni pamoja na pato la taifa kukua kwa asilimia 5.0 mwaka 2009, asilimia 5.7 mwaka 2010 na kuongezeka hadi kufikia asilimia 7.2 mwaka 2011 na 7.5 mwaka 2012.

Pia, kasi ya mfumuko wa bei kupungua na kufikia chini ya asilimia 10, mwishoni mwa Juni, mwaka huu, kuongezeka kwa mapato ya ndani kufikia uwiano na pato la taifa kwa bei ya mwaka husika kwa asilimia 15.9 mwaka 2008/09; asilimia 16.4 mwaka 2009/10; asilimia 17.2 mwaka 2010/11; na asilimia 18.3 mwaka 2011/12.


Vilevile, kudhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa tafsiri pana katika wigo utakaowiana na malengo ya ukuzaji wa uchumi, na kasi ya upandaji bei na kuwa na akiba ya fedha za kigeni itakayoweza kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma toka nje kwa kipindi kisichopungua miezi mitano, kuwa na kiwango cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha na kuondoa vikwazo vya kimfumo na kimuundo katika sekta ya fedha ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi.


Waheshimiwa wabunge nawashukuru kwa kuona upopopo wa Mkula, ila nanyi mnaongea sana bila kutenda, kwani huu upopopo wa Mkula kauanza leo? Mpigieni kura ya kutokuwa na imani nae bungeni ili ang'oke au mnaogopa atawabania posho zenu? Wabunge muajibike ipasanyo.
 
Huyo kashiba atakukumbukaje weye!
Wanadhani kila mtu hafahamu maana halisi ya ukuaaji uchumi ndo maana hana aibu anatangaza yale anayotaka myasikie!
Hali ilivyo sasa na hayo maneno yake...
Ni kama kumtusi mamamkwe mbele ya halaiki!
 
Mkuu asante kwa kuniuliza swali hilo let me explain nimeipata wapi figure hiyo kwanza unakubaliana nami kwamba GDP Growth rate ya Tanzania ilikuwa 7.1% 2008-to 7.3%

Tunakuta kwamba mwaka 1995-1999 Tanzania ilikuwa katika constant economic growth rate ya 4.0 (See IMF archive for this). Kutokana na figure hii tunaitumia kama base rate toa na rate ya mwaka 2009 unakuta kwamba uchumi watanzania unategemewa kushuka by 3.1%. Pia IMF walitoa figure ya kwamba GDP ya Tanzania itakuwa 4.5%.

Hivyo basi ukiangalia figure yangu na figure ya IMF GDP growth rate is between 4.0-4.5% na hilo ni anguko la uchumi from 3.1-3.6%.

Upo hapo mkubwa?

Tunamuomba mkulo atupe figures zake amezitoa wapi?

Kwanza naafikiana na wewe kuhusiana na swala la kumuuliza Mh. waziri ni wapi alipotoa takwimu zake. Haya ndio matatizo ya kutokuwa na mtu anayeelewa maana ya misamiati na hesabu za kiuchumi kuwa kiongozi wa wizara kama ile.

Naomba kukusahihisha kidogo mkuu, kwanza kwa mahesabu yako uchumi haujaanguka. Hiyo asilimia 4-4.5 bado ni ukuaji toka kwa mwaka uliopita. Pili matumizi hayo ya wastani wa viwango wa ukuaji si sahihi kuwa kama base rate. Ukitaka base rate basi deflate takwimu kutumia prices za a chosen base year. Pia kumbuka ya kwamba structurally uchumi wa nchi umebadilika sana na hivyo kulinganisha takwimu za leo hii na zile za miaka ya 1990 bila ya kutumia an indentical base year ni makosa makubwa sana. Ukifanya a simple OLS regression ya expenditure based GDP utaona hii structural instability ya multipliers zako.

Kingine pia, ingawa kama mwanataaluma natambua ya kwamba takwimu hizi za IMF na WB huwa mara nyingi ni bora kushinda za kwetu za NBS na BoT ILA hawa wenzetu wa serikalini hugoma kuzitambua kama ni takwimu rasmi za nchi.

Hapa tunahitaji forum na Mh. Mkulo tumpike tumchambue kama karanga
 
Kwanza naafikiana na wewe kuhusiana na swala la kumuuliza Mh. waziri ni wapi alipotoa takwimu zake. Haya ndio matatizo ya kutokuwa na mtu anayeelewa maana ya misamiati na hesabu za kiuchumi kuwa kiongozi wa wizara kama ile.

Naomba kukusahihisha kidogo mkuu, kwanza kwa mahesabu yako uchumi haujaanguka. Hiyo asilimia 4-4.5 bado ni ukuaji toka kwa mwaka uliopita. Pili matumizi hayo ya wastani wa viwango wa ukuaji si sahihi kuwa kama base rate. Ukitaka base rate basi deflate takwimu kutumia prices za a chosen base year. Pia kumbuka ya kwamba structurally uchumi wa nchi umebadilika sana na hivyo kulinganisha takwimu za leo hii na zile za miaka ya 1990 bila ya kutumia an indentical base year ni makosa makubwa sana. Ukifanya a simple OLS regression ya expenditure based GDP utaona hii structural instability ya multipliers zako.

Kingine pia, ingawa kama mwanataaluma natambua ya kwamba takwimu hizi za IMF na WB huwa mara nyingi ni bora kushinda za kwetu za NBS na BoT ILA hawa wenzetu wa serikalini hugoma kuzitambua kama ni takwimu rasmi za nchi.

Hapa tunahitaji forum na Mh. Mkulo tumpike tumchambue kama karanga

Itakuwa wazo la busara maana kimtazamo wangu ukuaji wa uchumi wa asilimia 7% mh sidhani kwakweli sijui labda kuna information zengine zipo hatuzijui but I am skeptical on that.

Kuhusu kutumia constant GDP as a base year nimeassume that before uchumi haujaanza kukua rapidly we had constant economic performance for five consecutive year (Hapa Mkapa nampa heko sana tu). If we assume that external markets and economies zimechangia kukua kwa uchumi wetu kwasasa then ilipokuja recession 2008-2009 most cash economy tunaweza kusema hazijawa affect kwasababu we are mainly a cash economy. Sasa kwa mtazamo huo tukiondoa externalities unakuta kwamba uchumi wetu unakuwa kwa asilimi 4.0% kwasababu ya zile indicator za mwanzoni zilizokuwa consistent for a certain time.

But nakubaliana nawewe ni muhimu tukapata base year but that inabidi tupate data zaidi which hawa waungwana wa BOT, NBS na wengineo sidhani kama watakubali kwani tunaweza kuona usanii unaoendelea. Ila mzee huyu inawezekana akitufafanulia tunaweza kufahamu kinachoendelea venginevyo these figures zinapendeza sana!!!!!
 
Serikali yajifilisi
Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 26 May 2010
Printer-friendly versionSend to friend
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo

SERIKALI imeumbuka. Inahaha kukopa fedha benki kujazia bajeti, wakati inatuhumiwa kutumia mabilioni ya shilingi bila maelezo mwafaka.

Taarifa za kuaminika ambazo pia zinathibitishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zinauweka utawala wa rais Jakaya Kikwete kitanzini.

Wakati serikali imekopa karibu Sh. 270 bilioni kutoka benki, CAG amethibitisha matumizi mabaya ya serikali yanayofikia Sh. 344.1 bilioni katika mwaka wa fedha uliopita.

Kiasi ambacho CAG anasema kimetumiwa vibaya au bila maelezo mwafaka, kinazidi fedha ambazo serikali inakopa kutoka benki kwa zaidi ya Sh. 74.1 bilioni.

Wiki iliyopita serikali ilisema imekopa Sh. 270 bilioni kutoka benki ya Stanbic ya jijini Dar es Salaam kujazia kwenye bajeti yake ya mwaka 2010/2011.

Hatua hiyo ya serikali inatokana na wafadhili kukata kiasi cha dola za Marekani 220 milioni sawa na Sh. 270 bilioni kutoka kwenye ahadi zao za kusaidia bajeti ya Tanzania kwa mwaka huo.

Wafadhili wameeleza kwamba kiasi hicho kimekatwa kutokana na serikali kutokuwa makini katika kukusanya mapato na kukosa nidhamu katika matumizi. Wameeleza kwamba serikali haitekelezi ahadi zake hasa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia kwa ujumla.

Kwa mujibu wa CAG, ofisi ya rais ni miongoni mwa zilizotumia vibaya fedha za serikali. Ripoti inaoyesha kuwa mwaka wa fedha wa 2008/2009 utumishi, iliyo chini ya ofisi ya rais, imetumia vibaya Sh. 282 milioni.

Fedha hizo zimetumika kulipia matumizi ya watumishi wake kulala hotelini, wakati watumishi hao tayari walilipwa na serikali fedha za kujikimu.

Aidha, CAG anasema ofisi hiyo imetumia kiasi cha Sh. 705 milioni bila ya kuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi yaliofanyika.

Katika kile kinachoonekana kuchota kila kinachopatikana, ofisi hiyo ya rais imelipa ofisa wake mmoja kiasi cha Sh. 13.3 milioni ikiwa ni asilimia 30 ya posho ya nyumba, huku akiwa amepewa nyumba na serikali.

MwanaHALISI lilipomuuliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo kuhusu matumizi ya ikulu na mengine ya serikali, alisema "ni mapema mno kuzungumzia suala hilo."

Alisema, "Sisi tumeipata ripoti hiyo ya CAG kwenye mkutano uliopita wa Bunge na bado hatujaidili. Kwa kweli katika mazingira haya nitakuwa napayuka tu kama nitazungumza lolote."

Cheyo alisema sharti kamati yake ipate maelezo kamili ndipo iweze kutoa maoni yake.

Wizara nyingine ambazo CAG anasema zimetumia fedha vibaya au bila vielelezo sahihi, ni pamoja na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi.

Katika wizara hiyo, CAG amegundua Sh. 3.6 bilioni zilizohamishwa kutoka fungu la matumizi ya kawaida kwenda katika fungu la ukarabati na manunuzi zilitumiwa vibaya.

CAG anasema katika ripoti yake kuwa, fedha hizo zilizohamishiwa fungu la ukarabati na manunuzi, hazikutumika kwa kazi iliyotajwa.

"…Hakukuwapo na ukarabati wala manunuzi yaliyofanyika. Mpango wa mwaka wa manunuzi na taarifa ya manunuzi, vilionyesha manunuzi hayo hayakufanyika kutokana na ukosefu wa fedha," anasema CAG.

Matumizi mengine ya kutisha ni yale yaliyofanywa na wizara ya fedha yenyewe. Watendaji wa wizara hiyo, walipeleka kiasi cha Sh. 15 bilioni katika halmashauri mbalimbali ambazo hazikujulikana zilivyotumika.

Fedha hizo zimepelekwa bila ya kufahamisha Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) jambo lililosababisha "kutumika vibaya" au kuibwa, taarifa inasema.

Ripoti ya CAG inasema serikali ilitumia vibaya takribani Sh. 68 bilioni, ambazo hazikuwapo katika bajeti.

Aidha, serikali imetumia Sh. 23.7 bilioni ambazo zilitumia kuwekea dhamana Shirika la Umeme nchini (Tanesco). Shirika hilo lilishindwa kulipa deni lake na serikali ikalazimika kulilipa.

Lakini, kubwa kuliko yote, ni uamuzi wa serikali kubadili deni la Sh. 135 bilioni kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kuwa dhamana itakayolipiwa riba ya Sh. 11.50 kwa mwaka.

Kutokana na uamuzi huo, CAG anasema, "serikali italazimika kulipa kiasi cha Sh. 230 bilioni katika kipindi cha miaka 20 ijayo."

Matumizi mengine ya Sh. 2 bilioni yamelipwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii inayomiliki kampuni ya M/S Pensions Properties Limited (PPL).

Mifuko hiyo imechotewa na serikali na washirika wake kiasi cha Sh 2, 845, 637,096 kama faini ya ucheleweshaji malipo yaliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa "ukumbi mdogo wa Bunge - Dodoma."

Mifuko iliyolipwa fedha hizo ni Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).

Kama hiyo haitoshi, CAG anasema serikali imelipa kiasi cha Sh. 4 bilioni kwa wamiliki wa hoteli ya Travertine ya jijini Dar es Salaam, kutokana na kushindwa katika shauri lililofunguliwa mahakamani na menejementi ya hoteli hiyo.

Menejementi ya Hotel Travertine ilifungua kesi Na. 350 ya mwaka 2002 kutokana na serikali kuvunja mkataba wake na hoteli ambao CAG anasema, "haukuwa na manufaa yoyote kwa serikali."

Serikali pia imepoteza kiasi cha Sh 17.8 bilioni zilizokusanywa na Idara ya Uhamiaji Zanzibar ambazo hazikuwasilishwa katika serikali ya Muungano.

Ripoti hiyo imeeleza pia namna wizara ya fedha ilivyofanya manunuzi makubwa yenye thamani ya Sh 1.6 bilioni ili kuepuka fedha zilizokuwa hazijatumika hadi wakati huo zisirejeshwe kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari, wiki iliyopita, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema mapato ya serikali yameshuka kwa wastani wa asilimia sita.

Mkulo alisema Mamlaka ya Mapato (TRA) haikusanyi kama awali na uuzaji wa bidhaa nje umepungua.

Hata hivyo, Mkulo alijitetea kuwa uchumi wa nchi umeimarika kiasi cha kuwa na nguvu ya kukopa fedha hizo na kwamba hata washirika wa mawandeleo - Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) hawana kikwazo kwa maamuzi hayo.

Wakati Waziri Mkulo akipiga siasa katika suala nyeti la uchumi, taarifa zinasema sarafu ya taifa imeporomoka kwa kasi ambayo haijawahi kufikiwa.

Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, sarafu hiyo imeshuka thamani yake kwa wastani wa Sh. 60.

Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu serikalini aliliambia MwanaHALISI kuwa ripoti ya CAG imeiumbua serikali, kutokana na mabilioni hayo ya shilingi kutojulikana yalivyotumika.

Katika Wizara ya Miundombinu, CAG amekutana na msururu wa madai ya wizara na idara za serikali zilizoagiza magari kupitia wizara hiyo, lakini yakiwa bado hayajafika.

Hata Ofisi ya Msajili wa Vyama imeguswa. Katika hali ambayo haijaweza kutosheleza ofisi ya CAG, msajili ametumia takribani Sh. 17 milioni kumlipia mtumishi wake mmoja fedha za kujikimu wakati wa mafunzo yake ya mwezi mmoja nchini Swaziland.

Kwa upande mwingine, CAG anasema wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imefanya manunuzi yenye thamani ya Sh. 103.06 milioni nje ya "mpango wa manunuzi wa mwaka" na bila manufaa.

Aidha, wizara ilitumia kiasi cha dola za Marekani 151,000 kukarabati jengo ililolinunua kwa dola za Marekani 10.5 milioni nchini Marekani, wakati kwa mujibu wa mkaguzi wa majengo, jengo hilo halikustahili kukarabatiwa.

Source: Mwanahalisi

Mtazamo: Hivi kweli uchumi utakuwa kukiwa na matumizi mabaya kama haya ya pesa, ukusanyaji mbovu wa mapato. Hivi uchumi unakua wakati nchi ina crisis ya liquidity mpaka tunakopa? Hivi uchumi unakuwa wakati pesa nyingi zinaenda katika sekta zisizokuwa zinazalisha? Sijui but labda waungwana mnaweza kutusaidia!!!!
 
Back
Top Bottom